PreGE2025 Mbunge Sekiboko: Nilipohitimu Digrii ya Ualimu, nilijifunza kushona viatu VETA

PreGE2025 Mbunge Sekiboko: Nilipohitimu Digrii ya Ualimu, nilijifunza kushona viatu VETA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
18 March 2025
Arusha, Tanzania

SHUHUDIA WENYE DEGREE ZAO WALIVYOFURIKA KWA MAKONDA ILI KUJIUNGA NA VETA WAFUNGUKA MAGUMU YA MTAA​


View: https://m.youtube.com/watch?v=59KOm9Y8_6U


Naona raia wasomi wamegundua kuwa maofisa usafirishaji kwa kuendesha bajaj na bodaboda siyo dili tena.

Wamejiongeza na kuamua kuachana na propaganda uchwara wa kuvika kilemba cha ukoka kwa vyeo uchwara vya maafisa wasafirishaji.

Na sasa wanaenda VETA kupata ujuzi unaoweza kuwafanya wajiajri na kuajiri kupitia kampuni ndogo ndogo watakazoanzisha ziwe sekta ya kilimo kukausha matunda embe, nanasi, nazi, chips kavu za ndizi mkono wa tembo, mbilimbi n.k kisha kuvitia ktk vifungasho

Mazao ya uvuvi na nyama kupikwa na kukaushwa kisha kutiwa katika vifungashio tayari kwa kuliwa moja kwa moja badala ya mazao ya uvuvi na nyama kuharibika vikiwa vibichi.

View: https://m.youtube.com/watch?v=H0-DmFhP_UU
Pongezi kwa kujitambua na kujisahihisha kuwa fursa siyo pekee, ni katika kuendesha bodaboda, bajaj au kuwa machinga barabarani.
 
Kwahiyo Wakitoka VETA, wanaingia mjengoni kugonga Meza?

Tuelewane mapema, sio wengine wakitoka huko VETA waanze kuranda randa mtaani kusaka ridhiki. Lol

Viongozi wa hii nchi, mshipa wa aibu ulikatika kabisa.
Mxxxiiieeew.
Hiyu kabla alikuwa DAS wilaya ya Nachingwea
 
Tunakoelekea wazazi wataacha kusomesha watoto degree. Kwanini upoteze pesa zote hizo, muda mwingi na energy nyingi kupata degree. Halafu uje ukae darasa Moja na na mtoto wa miaka 12 VETA?

Bora kuanza mapema VETA!
 
Na sasa wanaenda VETA kupata ujuzi unaoweza kuwafanya wajiajri na kuajiri kupitia kampuni ndogo ndogo watakazoanzisha ziwe sekta ya kilimo kukausha matunda embe, nanasi, nazi, chips kavu za ndizi mkono wa tembo, mbilimbi n.k kisha kuvitia ktk vifungasho

Mazao ya uvuvi na nyama kupikwa na kukaushwa kisha kutiwa katika vifungashio tayari kwa kuliwa moja kwa moja badala ya mazao ya uvuvi na nyama kuharibika vikiwa vibichi.
Chuo cha VETA cha Mafunzo ya Hotel na Utalii VHTTI kijiongeze kwa kutoa mafunzo ya kuhifadhi vyakula vya kuvipika, kuvikausha na kuvitia ktk vifungashio vyenye ubora na salama mazao yake ya nyama na samaki kuweza kuliwa na kuuzwa ktk masoko, supermarket, maduka n.k


View: https://m.youtube.com/watch?v=1ASLCrb14kQ
 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo Husna Sekiboko akizungumza mkoani Dar es Salaam wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 30 tangu kuanzishwa kwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) amesema yeye baada ya kuhitimu Shahada yake ya kwanza ya ualimu aliamua kwenda VETA kupata ujuzi wa kushona viatu.

Soma: Mbunge Sekiboko: Nilipohitimu Digrii ya Ualimu, nilijifunza kushona viatu VETA

"Mimi wakati nimemaliza digrii yangu ya kwanza ya ualimu Mheshimiwa Waziri Mkuu niliamua kwenda VETA na nilikwenda kujifunza nipate ujuzi wa kushona viatu ". amesema Sekiboko

View attachment 3275026

VETA na Ualimu, same entry qualification. Kwa yeye kufanya hivyo ni sawa tu. Ningeshangaa kama angesema alihitimu Law au Engineering halafu kaenda VETA kushona viatu.
 
What is next ? Kujifunza kuziba pancha ?

Hizo kazi wengine tulikuwa tukijifunza kila wikiendi tukiwa primary..., hawa hawachelewi kuongelea na kujifunza kuziba pancha..., na kuona kwamba they do not mean what they say, kipindi ambacho kila kitu kipo wazi online wao ndio wanasababisha bundle halishikiki...

 
Siungi mkono hili jambo. Haina tofauti na wanaosema kiswahili kiwe lugha ya kufundishia huku watoto wao wanasoma shule za kimataifa. Kumuunga mkono PM kwenye hili inahitaji uwendawazimu wa hali ya juu.
 
Alisomeaje ualimu wakati hana hata shule ya chekechea yeye na familia yake hana akili mjinga mkubwa

Wahindi mtoto akisoma ualimu mzazi lazima awe na shule au ukoo

Kusoma ni uwekezaji husomi tu kama mwehu

Akili hana kapoteza miaka mitatu bure
 
Hapo golini kwangu patawaka hatari, shishi na mashost zake watakoma.
😂😂😂😂😂
Kila ijumaa unatuwekea live band wateja wako 😹😹
Kijiwe hakipoi hakiboi ni heya heya, hiya hiya..!!
 
Back
Top Bottom