Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mbunge wa Tanganyika (CCM), Seleman Kakoso amependekeza Serikali kuongeza tozo kwenye mawasiliano ya simu ili zisaidie kujenga miundombinu ya barabara.
Kakoso ametoa mapendekezo hayo leo Jumatatu April 13, 2026 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu ambapo amedai mpango huo unaweza kukusanya hadi Sh1 trilioni.
"Mheshimiwa mwenyekiti, mimi nina mapendekezo mawili, kwanza Serikali iendelee kudhibiti mapato lakini tukubaliane kuanzisha chanzo kipya cha mapato kwenye muda wa maongezi katika simu zetu," amesema Kakoso.
Soma Pia: TOZO ZA SERIKALI kwenye MIAMALA ya Simu zimerejeshwa tena?
Mwenyekiti huyo wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ametaka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kuweka tozo ya Sh100 kwenye muda wa maongezi ambayo itasaidia kukusanya zaidi ya Sh1 trilioni.
Amesema fedha hizo zikikusanywa zigawiwe katika mafungu mawili yaani Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (Tarura) na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) kiasi alichoeleza kitakuwa msaada kwenye matengenezo ya miundombinu.