Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 7,207
- 17,674
Mbunge wa jimbo la Gairo mh Shabiby, wakati akichangia hotuba ya bajeti kuu amemshukia kama mwewe waziri wa fedha Mwigulu Nchemba kuwa tabia yake ya kutaka kuwa mzuri kwa kila mtu na kila taasisi imesababisha awe na mipango mingi isiyo na tija kwa taifa ikiwemo hela kutopelekwa kwa wakati kwenye miradi na kulea mafisadi serikalini!
Mh Shabiby ameonya kuwa hayuko tayari kusifia kila kitu kwani kwenye serikali ya awamu ya 6 wapigaji wamekuwa wengi na wakitoka kuiba hela wanaenda kujisafisha kwa kumsifia mama anaupiga mwingi!!
Mh Shabiby amemuonya waziri Nchemba kuwa hatakuwa tayari kuona mafisadi wanalelewa kama mayai na atasema ukweli kwa wananchi.
Mh Shabiby ameonya kuwa hayuko tayari kusifia kila kitu kwani kwenye serikali ya awamu ya 6 wapigaji wamekuwa wengi na wakitoka kuiba hela wanaenda kujisafisha kwa kumsifia mama anaupiga mwingi!!
Mh Shabiby amemuonya waziri Nchemba kuwa hatakuwa tayari kuona mafisadi wanalelewa kama mayai na atasema ukweli kwa wananchi.
Mbunge wa Shabiby akitoa mchango wake bungeni amedokeza namna wizi ulivyoenea kwa sasa nchini huku akimtaka Waziri wa Fedha kukaa pembeni kumpisha ikiwa kama kazi imemshinda. Akifafanua hoja hiyo Shabiby anasema:
Ukiwa waziri wa Fedha unatakiwa uwe ngangari kama umeshindwa niachie mimi nafasi nije nikae hapo, unafanya kazi nzuri lakini inabidi uwe ngagari kwenye hizi vitu. Mtu akitaka kuchukua pes, na kama ukitaka kuwa mzuri kwa kila taasisi hiyo kazi haiwezekani. Nchi imefikia mahali ambapo sasa hivi lazima tuseme ukweli, wapigaji wamekuwa wengi. Wengine utasikia tu mama anaupiga mwingi, sio anaupiga mwingi kana kwamba anamsifia kwenye moyo, anaupiga mwingi yeye anaiba hela. Anatandika pesa halafu akija huku anasifia.
Mbunge wa Jimbo la Gairo Ahmed Shabiby akichangia hoja ya Bajeti Kuu ya Serikali Bungeni Jijini Dodoma amesema hayuko tayari kusifia Serikali kama vitu haviendi sawa na amesema atakuwa Mbunge wa kwanza kupinga bajeti hiyo endapo bajeti haitoongezwa Wizara ya Ujenzi na TARURA.
Shabiby amehoji pia kuhusu minada ya magari ya Serikali kutotangazwa hadharani akidai kuwa magari hayo yanauzwa kwa Watumishi kwa bei ya hasara.
“Mwaka jana ulisema Serikali inatumia zaidi ya bilioni 500 kuagiza magari lakini najiuliza hii Serikali ni tajiri sana au kuna shida gani umekuja ukalalamika na ukaleta mpango kwa kuondoa gharama hizo na kila Mtumishi atanunua gari lake ili alie na uchungu lakini najiuliza twende Halmashauri zote haya magari mabovu yanaoza mengine hayauzwi na yakiuzwa wanajiuzia wenyewe hii Nchi ina utajiri kiasi gani hadi haipigi mnada yale magari?, umewahi kusikia magari ya Serikali yanauzwa kwenye mnada?”