Halaiser
JF-Expert Member
- Apr 3, 2014
- 4,230
- 6,653
Anasema kama wakiongelea habari ya sukari kwa undani, mle mjengoni hakutakalika. Betina atakuwa amepata majibu yake hata kabla kamati kuchakata.Hamna kitu kigumu maishani kama kuficha ukweli ulioko ndani yako ili kutetea ugali, roho itakusuta mwishowe utaongea tu ukweli.
Mpina anaanza kupata wafuasi taratibu..
Simply serikali ya mama Abdul ni ya hovyo, ilifanya mambo ya hovyo, na inaendelea kufanya mambo ya hovyo kila siku, huku mawaziri kama kina Mwigulu wakiwa ndio viongozi wa mambo hayo ya hovyo.
Kwa mtu mwenye akili timamu kutetea huu ujinga ni ngumu sana, unaweza kushangilia pale bungeni kwa kugonga meza lakini ndani ya nafsi yako unalia machozi, hauwezi kushangilia ufisadi unaofanywa na kina Bashe kwa watanganyika kisha unimbie una akili timamu, never.
Tulia atakuja kupata aibu ya mwaka kwa Mpina. Atajuta kwa uzembe/uchawa wake kwa serikali.