Mbunge Shabiby: Wapigaji wameongezeka serikalini, sitasifia kila kitu

Etwege

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2018
Posts
7,207
Reaction score
17,674
Mbunge wa jimbo la Gairo mh Shabiby, wakati akichangia hotuba ya bajeti kuu amemshukia kama mwewe waziri wa fedha Mwigulu Nchemba kuwa tabia yake ya kutaka kuwa mzuri kwa kila mtu na kila taasisi imesababisha awe na mipango mingi isiyo na tija kwa taifa ikiwemo hela kutopelekwa kwa wakati kwenye miradi na kulea mafisadi serikalini!

Mh Shabiby ameonya kuwa hayuko tayari kusifia kila kitu kwani kwenye serikali ya awamu ya 6 wapigaji wamekuwa wengi na wakitoka kuiba hela wanaenda kujisafisha kwa kumsifia mama anaupiga mwingi!!

Mh Shabiby amemuonya waziri Nchemba kuwa hatakuwa tayari kuona mafisadi wanalelewa kama mayai na atasema ukweli kwa wananchi.

Your browser is not able to display this video.

 
Hamna kitu kigumu maishani kama kuficha ukweli ulioko ndani yako ili kutetea ugali, roho itakusuta mwishowe utaongea tu ukweli.

Mpina anaanza kupata wafuasi taratibu..

Simply serikali ya mama Abdul ni ya hovyo, ilifanya mambo ya hovyo, na inaendelea kufanya mambo ya hovyo kila siku, huku mawaziri kama kina Mwigulu wakiwa ndio viongozi wa mambo hayo ya hovyo.

Kwa mtu mwenye akili timamu kutetea huu ujinga ni ngumu sana, unaweza kushangilia pale bungeni kwa kugonga meza lakini ndani ya nafsi yako unalia machozi, hauwezi kushangilia ufisadi unaofanywa na kina Bashe kwa watanganyika kisha unimbie una akili timamu, never.
 
Mbunge wa jimbo la Gairo mh Shabiby, wakati akichangia hotuba ya bajeti kuu amemshukia kama mwewe waziri wa fedha Mwigulu Nchemba kuwa tabia yake ya kutaka kuwa mzuri kwa kila mtu na kila taasisi imesababisha...
Kuna namna inabidi Mama aanze kuwapoteza watu katika mazingira ya kutatanisha kama mtangulizi wake la sivyo mambo yatakuwa magumu kabla na baada ya 2025.
 
Mwanangi unasemaje hapo Tlaatlaah

Ova
dosari, kasoro na changamoto za kimaadili kwa watumishi wa umma, mashirika ya kiraia, mashirika ya kidini kitaifa na kimataifa yapo, na kila uchao Serikali sikivu ya chama cha Mapinduzi itaendelea kung'ag'ana nao na wengine ambao wameshabainika wapo mahakamani,

na siku zote wito wa Serikali ni kwamba, kwenye mambo kama haya ya unadhifu kwenye rasilimali za umma, haitoshi kupiga kelele tu kwamba kuna upigaji mahali fulani ili upihiwe makofi na huku ukiunyamazia upigaji huuo bila kuripoti katika mamlaka zinazo husika, hiyo itakua ni kazi bure,

ni lazima pawe na jitihada binafsi na ushirikiano wa dhati, wa maneno na matendo kuanzia kwenye majimbo yetu, kuwasilisha vielelezo vya uthibitisho wa malalamiko yako ya upigaji kwenye taasisi na vyombo vya ulinzi na usalama vinavyohusika kushughulika na changamoto hiyo...

hata hivyo,
nampongeza sana Mh.Shabby ushauri mzuri kwa Serikali na kwa mchango wake, kwa kuchukizwa na baadhi ya watumishi wa umma, wasio waaminifu na wapiganaji mali ya umma kwa manufaa yao,
na kwa jinsi ambavyo, anawatumikia wananchi wa Jimbo la Gairo kwa uaminifu na bidii kubwa...

zaidi sana, nampongeza sana Mh.Shabiby,
kwa kuunga mkono, jitihada na hatua za makusudi, za chama na Serikali sikivu ya CCM, katika kuchochea, na kuwaletea maendeleo endelevu wanainchi wa Gairo kwenye maji, afya, elimu, kilimo, ufugaji, barabara, biashara na masoko n.k.πŸ’

kwako mrangi
 
Mbunge wa jimbo la Gairo mh Shabiby, wakati akichangia hotuba ya bajeti kuu amemshukia kama mwewe waziri wa fedha Mwigulu Nchemba kuwa tabia yake...
Shabiby Huwa hakopeshi,aliibua Ufisadi wa Kalemani Kupitia kuweka pgment Mafuta ,wizi wa Ewura nk.

Ingawa this time amekuwa too general ,alitakiwa awataje directly
 
Shabiby Huwa hakopeshi,aliibua Ufisadi wa Kalemani Kupitia kuweka pgment Mafuta ,wizi wa Ewura nk.

Ingawa this time amekuwa too general ,alitakiwa awataje directly
Hawezi kuwataja kwa majina muda hautoshi maana selikali nzima ni wezi
 
Mbunge wa jimbo la Gairo mh Shabiby, wakati akichangia hotuba ya bajeti kuu amemshukia kama mwewe waziri wa fedha Mwigulu Nchemba kuwa tabia yake ya kutaka kuwa mzuri kwa kila,,,
Mwambieni HAMSIKILZI..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…