saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 624
- 1,456
MBUNGE wa Babati Vijijini, Daniel Sillo Baran ameliomba Bunge liazimie watu wote waliohusika na kashfa ya kuruhusu kufanyika malipo ya shilingi Bilioni 350 kwa Kampuni ya Symbion Power LLC wachukuliwe hatua za kisheria kwa kufanya ubadhirifu huo ili iwe fundisho kwa wengine.
"Malipo yaliyofanywa na TANESCO kwa Symbion takriban bilioni 350 fedha hizi ni nyingi sana, Leo tunalia miradi ya barabara, maji kwenye majimbo yetu, nishati ya umeme haipo lakini wenzetu ambao wamepewa dhamana kusimamia fedha za umma wanachezea fedha wawe na uchungu na watanzania.
Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti amesema hayo leo Novemba 5, 2022 Bungeni wakati akichangia Taarifa za Kamati za Bunge za PAC, LAAC na PIC kuwa viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia fedha za umma wawe wanatembea vijijini kuona hali halisi ya maisha ya watanzania, tukumbuke hizi ni kodi za watanzania, tunakaa Bunge hapa miezi mitatu tunapanga bajeti, watu wachache wanakaa wanachezea fedha za umma jambo hili linaumiza sana
“Tuna miradi mingi ya kimkakati inahitaji fedha, tuna deni la Serikali linataka fedha tulipe watanzania wanashida ya maji tuna shida ya nishati ya umeme vijijini lakini wako wenzetu wameamua kucheza na fedha za umma naomba Bunge lako tukufu liazimie kuwachukulia hatua wote waliohusika na ubadhirifu wa fedha za uuma ili iwe fundisho kwa wengine sisi ni wawakilishi wa wananchi tunaelewa uhalisia wa wananchi kule” Amesema Mhe. Baran