Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Mbunge wa Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu, Simai Mohammed Said akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kupitisha bajeti kuu ya Serikali leo Juni 23, amekwepa kumtaja Yuda msaliti aliyeko Serikali, na kusema kuwa watu wazima tayari walishaelewa tafsiri yake
Pia soma Mbunge Simai: Kuna Yuda Msaliti ndani ya Serikali hili anatafuta huruma kanisani
Anasema, Nilichokisema Juni mbili. Mimi nafikiri kwanza Watanzania wengi, na nyinyi ni watu wazima, mtakuwa mmenifahamu. Tafsiri ya jambo lile nafikiri Watanzania wamenifahamu na wamenielewa vizuri.
Jambo lililozungumzwa huko nyuma ni jambo ambalo lilishapita. Kama nilivyosema, Watanzania, ni watu wazima, wamenifahamu na tafsiri yake. Kwa hiyo sasa hivi tunachokiangalia ni utekelezaji wa bajeti, kuweza kumsaidia Rais na kuishauri Serikali, na niombe Watanzania sasa tusonge mbele.
Asanteni sana."