Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE SINGIDA MASHARIKI MHE. MIRAJI MTATURU AISHUKURU SERIKALI YA RAIS SAMIA KWA MRADI WA SWASH
MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka kiasi cha Shilingi Milioni 245,535,791.86 kwa ajili ya ujenzi wa vyoo bora kupitia mradi wa SWASH.
Akizungumza akiwa katika ziara zake jimboni humo Mtaturu amesema kupitia ziara zake amekuwa akipewa kero na ameziwasilisha serikalini.
"Huu ni ushahidi wa ahadi zilizotolewa na serikali kuboresha mazingira ya kujifunzia pamoja na afya za watoto wetu, tukiangalia kwa takwimu fedha za Programu ya SWASH ya vyoo bora Shule ya Msingi Aghida imepata Sh Milioni 38,480,965.31, na Shule ya Msingi Inang'ana imepata Shilingi Milioni 41,880,965.31" amebainisha.
Aidha, amesema Shule ya Msingi ya Makiungu imepata Shilingi 38,730,965.31, Matongo Shilingi Milioni 42,680,965.31, Mkiwa Shilingi Milioni 39,680,965.31 na Ulyampiti Shilingi Milioni 44,080,965.31 na hivyo kufanya jumla kuu kuwa Shilingi Milioni 245,535,791.86.
Pamoja na kuishukuru Serikali kwa miradi ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa, Zahanati, Barabara na Umeme, Mbunge Mhe. Miraji Mtaturu amesema vyoo hivi vimekuja kuboresha mazingira ya afya shuleni.
Mbunge Mhe. Miraji Mtaturu amewaomba viongozi na wananchi katika maeneo hayo kusimamia kwa karibu miradi hiyo ili thamani ya fedha ionekane.
Mwisho.