Mbunge Tarimba apendekeza TANESCO kufumuliwa na kuwepo kampuni 3 kwa ajili ya Uzalishaji, Usafirishaji na Ugawaji umeme

Mbunge Tarimba apendekeza TANESCO kufumuliwa na kuwepo kampuni 3 kwa ajili ya Uzalishaji, Usafirishaji na Ugawaji umeme

Tatizo la tanesco kwa sasa siyo kusambaza umeme bali hakuna umeme wa kutosha. Hivyo hata ukiigawa tanesco katika mashirika matatu utapata wapi umeme wa kusambaza?

Jitihada ielekezwe katika kutafuta vyanzo vipya na vingi zaidi vya umeme, usambazaji hauna tatizo kubwa!
Kwa kifupi matatizo ya umeme kwenye nchi hii yako everywhere, kwenye uzalishaji, usafirishaji na usambazaji. Au haujawahi kusikia watu wamelipia gharama za kuunganishwa umeme na hawajaunganishiwa huduma kwa hadi miezi sita ?
Kijijini kwetu transformation iliungua tulikaa siku 45 ndipo tukafungiwa nyingine.

Mkuu, au tunazungumzia Tanzania mbili tofauti ?
 
TANESCO ya sasa kwa namna ilivyo haitatufikisha mbali kama taifa.

Zipo options mbili za kuiboresha.

1. Kuboresha utendaji wa vitengo vyake vya uzalishaji, usafirishaji na usambazi wa umeme kama ulivyoeleza hapo.

2. Kuligawa shirika ili tupate mashirika mawili au matatu yatakayoshughulikia kikamilifu kazi hizo tatu.

In both two cases maboresho yanahitajika ili kuleta tija na ufanisi zaidi.
Mwenzetu Tarimba Abbas kaona approach ya pili ndio inafaa zaidi na kashauri hivyo.

Yote kwa yote, nyakati zijazo zinazihaji huduma ya kuaminika ya umeme (umeme uwe mwingi, usambazaji uwe wa uhakika).

Kwa muundo wa sasa TANESCO inabeba risks and responsibilities nyingi mno.

1. Maji yamekauka Kidatu - TANESCO
2. Visima vya gesi vinahitaji matengenezo - TANESCO
3. Nguzo zimeanguka Mafinga - TANESCO
4. Mfumo wa kununua LUKU una shida - TANESCO
5. Bibi Chausiku amelipia umeme hajaunganishwa - TANESCO
6. Kutengeneza nguzo za zege, kukata miti chini ya nguzo - TANESCO
7. Kubadili tariffs kwenda kwenye matumizi madogo - TANESCO.
8. Tunataka kuwauzia Malawi umeme - TANESCO
This is so much to do.

Tuiboreshe TANESCO kwa kweli, whatever the means, vinginevyo tutazidi kumlalamikia tu J. Makamba kila kunapokucha.
Umeme wa kusambaza haupo hata kama utaligawa shirika hili.

Kazi zote ulizoorodhesha hazina athari katika usambazaji wa umeme kwa sababu zina idara na vitengo vinavyojitegemea.
 
[emoji871]Wabunge aina ya Abbas Tarimba ni wabunge walioingia bungeni kusaka maslahi zaidi kuliko kuwakilisha wapiga kura.

[emoji871]Ukiona hivyo ujuwe kabisa kuna maslahi binafsi anawakilisha kutoka genge la kipigaji,ambalo linaiona kama fursa.

[emoji871]Binafsi hawa wabunge wafanyabiashara sampuli ya Tarimba,Musukuma,Abood nk,huwa nawachukulia kama wametafuta ubunge ili kujiweka karibu na michongo ya kibiashara zaidi.
Kama nitakua sijakosea, kwenye aya zako zote tatu "umemjadili Tarimba na wabunge aina ya Tarimba".

Tunaomba maoni yako juu ya hoja iliyopo mezani kama hautojali ndugu mtanzania mwenzetu.

Ahsante
 
Kwa kifupi matatizo ya umeme kwenye nchi hii yako everywhere, kwenye uzalishaji, usafirishaji na usambazaji. Au haujawahi kusikia watu wamelipia gharama za kuunganishwa umeme na hawajaunganishiwa huduma kwa hadi miezi sita ?
Kijijini kwetu transformation iliungua tulikaa siku 45 ndipo tukafungiwa nyingine.

Mkuu, au tunazungumzia Tanzania mbili tofauti ?
Tatizo siyo management bali ni investment. Tuwekeze vya kutosha ili tanesco ipate uwezo.
 
Ukubwa wa shirika unahusiana vipi na ufanisi wake ? Hata ukiligawa kuwa mashirika matatu kama utendaji wake katika hayo mashirika matatu utabaki hivyo hivyo, hakutakuwa na ufanisi wowote!! Inaelekea mbinu ya kuligawa shirika sio kulipatia ufanisi bali kutaka kuliuza kwa private operator.!! Huu ni mchongo wa Msoga Gang! Ndio maana wamemuweka Omar Issa kama Mwenyekiti wa TANESCO!!!

Remember Tanesco is very crucial to the success of other investments like the STANDAD GAUGE RAILWAY such that to put it into the hands of private operators can easily compromise national security!!

Argument kama hii ilitumika kuuza National Bank of Commerce kuwa ilikuwa inapata hasara kwasababu ilikuwa kubwa na watu wakapiga Pesa pale na Kaburu akachukua benki na assets zake kwa bei ya bure!!! We Shule learn from our past mistakes. KUFANYA KOSA SIO KOSA, KOSA KURUDIA KOSA.
Argument yangu ime base kwenye mahitaji yajayo ya umeme, ongezeko la wateja, uwezo wa TANESCO wa sasa, wingi wa majukumu waliyonayo, n.k

TANESCO inahitaji maboresho makubwa. Tena sana ili kuongeza ufanisi na tija.

Hayo ya Msoga, sijui nani anataka kumuuzia nani, naomba nisi comment chochote.
 
TANESCO inahitaji maboresho makubwa. Tena sana ili kuongeza ufanisi na tija.

Je huo ufanisi unapatikana kwa kuivunja TANESCO katika mashirika matatu? Je ni Kweli Kuwa mashirika yakiwa madogo yana ufanisi kuliko makubwa? IS EFFICIENCY A FUNCTION OF SIZE?
 
Dili lingine linapangwa, ukigawa maana yake menejimenti tatu, hapo tayari umemuongezea mlaji gharama. Pili mafisadi yatapewa ugawaji maana ndiko faida iliko uzalishaji itaachiwa umma.
Huoni ni fursa ya watz kupata ajira?
 
Ukubwa wa shirika unahusiana vipi na ufanisi wake ? Hata ukiligawa kuwa mashirika matatu kama utendaji wake katika hayo mashirika matatu utabaki hivyo hivyo, hakutakuwa na ufanisi wowote!! Inaelekea mbinu ya kuligawa shirika sio kulipatia ufanisi bali kutaka kuliuza kwa private operator.!! Huu ni mchongo wa Msoga Gang! Ndio maana wamemuweka Omar Issa kama Mwenyekiti wa TANESCO!!!

Remember Tanesco is very crucial to the success of other investments like the STANDAD GAUGE RAILWAY such that to put it into the hands of private operators can easily compromise national security!!

Argument kama hii ilitumika kuuza National Bank of Commerce kuwa ilikuwa inapata hasara kwasababu ilikuwa kubwa na watu wakapiga Pesa pale na Kaburu akachukua benki na assets zake kwa bei ya bure!!! We Shule learn from our past mistakes. KUFANYA KOSA SIO KOSA, KOSA KURUDIA KOSA.
Una uhakika kuwa ukubwa wa shirika na ufanisi wa shirika havina uhusiano? achana na causal relationship, lakini hata correlation hakuna? are you certain dude?
 
Tatizo siyo management bali ni investment. Tuwekeze vya kutosha ili tanesco ipate uwezo.
Tatizo la TANESCO ni investment and management.
Hapo juu nimeshauri (kwa maoni yangu) kwamba iwe tunaligawanya au hatuligawanyi, tunatakiwa tuliboreshe kwa maana ya:-
Rasilimali watu
Teknolojia
Miundombinu
Fedha (Vitendea kazi, maslahi, n.k)

NB: Naheshimu maoni yako kwamba rasilimali watu (management) imeshatosha.
 
Naunga Mkono hoja maana monopolity of TANESCO ndo inafanya hata utendaji na uwajibikaji kushuka sana
 
Would like to know shareholders katika hizo kampuni tatu ?

Sidhani kama suggestion yake itakuwa ziendelee kuwa Mali ya UMMA

Hii inanikumbusha story ya kumchemsha Chura unaanza na moto kidogo kidogo akija shituka temperature ishakuwa kubwa na kukimbia hawezi
 
Una uhakika kuwa ukubwa wa shirika na ufanisi wa shirika havina uhusiano? achana na causal relationship, lakini hata correlation hakuna? are you certain dude?

Give evidence if the contrary is the case! Weledi wa management una correlation na ufanisi wa shirika; kama management ni poor hata uvunje vunje shirika vipande vingapi huwezi kuwa na ufanisi. Kumleta Maharage kutoka DSTV na kumuweka TANESCO unategemea improvement au failure to justify breaking up of Tanesco?
 
Tatizo la TANESCO ni investment and management.
Hapo juu nimeshauri (kwa maoni yangu) kwamba iwe tunaligawanya au hatuligawanyi, tunatakiwa tuliboreshe kwa maana ya:-
Rasilimali watu
Teknolojia
Miundombinu
Fedha (Vitendea kazi, maslahi, n.k)

NB: Naheshimu maoni yako kwamba rasilimali watu (management) imeshatosha.
Naomba uninukuu vizuri, sijasema rasilimali watu inatosha bali inawiana na investment iliyowekwa! Endapo investment itaongezwa na rasilimali watu pia itaongezwa kulingana na teknolojia na miundombinu itakayojengwa.
 
xx
Wazee wa kuchungulia michongo hao usikute katumwa huyu kila kitu kimeshapangwa.
Alichosema Abbas Tarimba sio kipya kabisa...

Hata ukisoma Tanzania Power Syetem Mster Plan (TPSMP) hivyo imependekeza kwa miaka mingi sasa!!

Kama kumbukumbu zangu zipo sawa (TPSMP) ilianzishwa ama awamu ya Mkapa au KIkwete!

Wakati wa JPM nao ikawa updated lakini versions zote bado zinazungumzia suala alilosema Tarimba!

Hata suala la uwepo wa independent power producers kwa sasa ni kutokana na hiyo Tanzania Power System Master Plan!

Katika awamu zote, serikali imekuwa na kigugumizi kwenye
 
Tatizo la TANESCO ni investment and management.
Hapo juu nimeshauri (kwa maoni yangu) kwamba iwe tunaligawanya au hatuligawanyi, tunatakiwa tuliboreshe kwa maana ya:-
Rasilimali watu
Teknolojia
Miundombinu
Fedha (Vitendea kazi, maslahi, n.k)

NB: Naheshimu maoni yako kwamba rasilimali watu (management) imeshatosha.
Naomba uninukuu vizuri, sijasema rasilimali watu inatosha bali inawiana na investment iliyopo.

Endapo investment itaongezwa rasilimali watu itaongezwa kulingana na teknolojia na miundombinu itakayojengwa.
 
Moja imewashinda tatu mtaweza?

TANESCO walipaswa wapate mshindani mmoja tu kutoka nje ya nchi awafunze adabu.

Wangeoneshwa namna ya kutoa huduma sio ujinga walionao sasa.
Lengo la hiyo plan ni kuondokana na hilo ulilosema "moja tu inawashinda"

Kwamba, kuzalisha.... wao

Kusafirisha.... wao

Kusambaza... wao!

Kinyume chake, ikaonekana kwenye hizo functions ziingie hata kampuni binafsi! Ndo maana hata wewe kama una pesa, hivi sasa unaruhusiwa kuzalisha na kuwauzia umeme TANESCO... kwahiyo sio jambo jipya!

Sehemu ambayo bado serikali inasita sita ni hilo suala la usafirishaji na usambazaji, huku pia kukiwa na concerns za usalama na hujuma!!
 
Je huo ufanisi unapatikana kwa kuivunja TANESCO katika mashirika matatu? Je ni Kweli Kuwa mashirika yakiwa madogo yana ufanisi kuliko makubwa? IS EFFICIENCY A FUNCTION OF SIZE?
You don't get it.

Tanesco haifanyi vizuri kwenye uzalishaji wa umeme, haifanyi vizuri kwenye usafirishaji, haifanyi vizuri kwenye usambazaji.

Kuiongezea uwezo (ambao ndio tunaita ufanisi na tija) tunahitaji kuifanyia maboresho.

Kivipi, zipo njia mbili.

1. Kuligawa kwenye subunits na kuziongezea uwezo hizo subunits (More manpower, advanced technology, infrastructure, etc). Lengo la kugawa ni kuyafanya haya mashirika yanayozaliwa ku focus na ku concentrate kwenye eneo dogo (uzalishaji, usambazaji n.k) ili kuongeza ufanisi.

2. Kuliboresha kwa structure ambayo linayo sasa hivi. Kuliongezea uwezo kwa aspects nilizozitaja hapo juu na zaidi ili liweze kuongeza ufanisi.

Na hii approach ya kugawa ili kuongeza ufanisi sio ngeni kabisa, tumeona wizara zinagawanywa, (wizara ya mifugo na kilimo zamani zilikua pamoja, wizara ya habari na michezo zilikua pamoja, wizara ya afya na maendeleo ya jamii zilikua pamoja), maeneo ya utawala (sina haja hata kutaja), taasisi zinagawanywa (SUMATRA iligawanywa sasa tuna TASAC na LATRA).

Inaonekana ukiwa Rais tutakua na wizara mbili tu
1. Wizara ya elimu, afya, mifugo, ajira, madini, uvuvi, maji, uchukuzi, ardhi, maliasili, utumishi na muungano.

2. Wizara nyingine itajumuisha yote yaliyosalia.
 
Naomba uninukuu vizuri, sijasema rasilimali watu inatosha bali inawiana na investment iliyowekwa! Endapo investment itaongezwa na rasilimali watu pia itaongezwa kulingana na teknolojia na miundombinu itakayojengwa.
Nadhani hapa kwenye hili tuko pamoja.
 
Nishati sio Kitu cha Kuchezea kabisa, Tanesco iendele kuwa State Owned Entity kwa Masilahi mapana ya Nchi, Katika Vitu nyeti Nchi hii ambayo si vya kuchezea ni Nishati acheni masihala wazee
 
Back
Top Bottom