I get it very well. Kwanini mnalilia hiyo option ya kuligawa shirika na sio hiyo option yako ya pili? Kwani hayo maboresho ya Kufanya shirika liwe na ufanisi na tija zaidi ni lazima liwe vipande vipande? Hiyo technology unayosema , haiwezi kuwa adopted mpaka shirika liwe vipande vipande? Duniani kuna mashirika makubwa mara mbili ya TANESCO na yana ufanisi na na tija hivyo hiyo argument yako ya size is moot!!
Kuna jambo nyuma ya pazia ambalo hawa wahuni wameona huu ndio wakati wao muafaka wa kutimiza azma yao . Kwanini hawakuja na mawazo hayo miaka miwili iliyopita wakati huo tulikwisha anza kusahau shida ya mgao? They had to wait until when they artificially created the load shedding as justification for their intended plans!!
Uko negative sana, unawaza kupigwa tu 24/7.
Kama kuna options mbili to a solution, haiwezekani watu milioni 60 wote tuka chagua option moja kama unavyotaka kulazimisha.
Wapo ambao wanadhani option A ni sahihi zaidi, wapo pia wanaodhani option B ni sahihi zaidi.
Usiwape dhambi wenye maoni tofauti, hii ni nchi mkuu. Otherwise ungekua pekeyako sasa nchi nzima ili ukifanya maamuzi yanakua ni ya kufanana.
Sijui unapata wapi ujasiri wa kumuuliza mwingine kwanini ana maoni X na sio maoni Y.
Mimi nadhani unachopaswa kuonyesha ni kwanini unadhani njia unayoiamini wewe ndio chaguo bora zaidi kuliko machaguo mengine yaliyobaki. Hoja yenye mantiki zaidi ndio inapaswa kushinda.
Kama unaamini TANESCO ya sasa (bila maboresho yoyote) ndio inatufaa zaidi, weka hoja zako mezani, kama zina mashiko tuendelee nayo hivyo ilivyo.
Kama unaamini TANESCO inatakiwa kuboreshwa bila kuigawa, weka hoja zako mezani, kama zina mashiko tuendee nayo namna hiyo.
Anayetaka igawanywe, anaweka hoja zake mezani, kama zina mashiko tunaenda mwelekeo huo.
Simple.
Halafu kuhusu suala la upigaji, hivi nani kakwambia "kupiga" pale TANESCO ni hadi tu itakapogawanywa ?
Kwamba ikiwa moja watu hawawezi kupiga ?
Kuhusu swala la kugawa taasisi ili kuwatafutia ulaji "ndugu zao", hii hoja sijui hata inatoka wapi...
Kwahiyo pale LATRA kuna MD ambaye ni binamu yake Tarimba ? Abdul Mkeyenge wa TASAC ni last born wa kwa kina Tarimba ?
Katibu mkuu ya wizara ya kina Nape ni dada yake Tarimba ?
Naibu waziri wa wizara ya kina Gwajima ni shangazi yake Tarimba ?
Sio sawa.