You don't get it.
Tanesco haifanyi vizuri kwenye uzalishaji wa umeme, haifanyi vizuri kwenye usafirishaji, haifanyi vizuri kwenye usambazaji.
Kuiongezea uwezo (ambao ndio tunaita ufanisi na tija) tunahitaji kuifanyia maboresho.
Kivipi, zipo njia mbili.
1. Kuligawa kwenye subunits na kuziongezea uwezo hizo subunits (More manpower, advanced technology, infrastructure, etc). Lengo la kugawa ni kuyafanya haya mashirika yanayozaliwa ku focus na ku concentrate kwenye eneo dogo (uzalishaji, usambazaji n.k) ili kuongeza ufanisi.
2. Kuliboresha kwa structure ambayo linayo sasa hivi. Kuliongezea uwezo kwa aspects nilizozitaja hapo juu na zaidi ili liweze kuongeza ufanisi.
Na hii approach ya kugawa ili kuongeza ufanisi sio ngeni kabisa, tumeona wizara zinagawanywa, (wizara ya mifugo na kilimo zamani zilikua pamoja, wizara ya habari na michezo zilikua pamoja, wizara ya afya na maendeleo ya jamii zilikua pamoja), maeneo ya utawala (sina haja hata kutaja), taasisi zinagawanywa (SUMATRA iligawanywa sasa tuna TASAC na LATRA).
Inaonekana ukiwa Rais tutakua na wizara mbili tu
1. Wizara ya elimu, afya, mifugo, ajira, madini, uvuvi, maji, uchukuzi, ardhi, maliasili, utumishi na muungano.
2. Wizara nyingine itajumuisha yote yaliyosalia.