Mbunge Tarimba apendekeza TANESCO kufumuliwa na kuwepo kampuni 3 kwa ajili ya Uzalishaji, Usafirishaji na Ugawaji umeme

Mbunge Tarimba apendekeza TANESCO kufumuliwa na kuwepo kampuni 3 kwa ajili ya Uzalishaji, Usafirishaji na Ugawaji umeme

TANESCO ya sasa kwa namna ilivyo haitatufikisha mbali kama taifa.

Zipo options mbili za kuiboresha.

1. Kuboresha utendaji wa vitengo vyake vya uzalishaji, usafirishaji na usambazi wa umeme kama ulivyoeleza hapo.

2. Kuligawa shirika ili tupate mashirika mawili au matatu yatakayoshughulikia kikamilifu kazi hizo tatu.

In both two cases maboresho yanahitajika ili kuleta tija na ufanisi zaidi.
Mwenzetu Tarimba Abbas kaona approach ya pili ndio inafaa zaidi na kashauri hivyo.

Yote kwa yote, nyakati zijazo zinazihaji huduma ya kuaminika ya umeme (umeme uwe mwingi, usambazaji uwe wa uhakika).

Kwa muundo wa sasa TANESCO inabeba risks and responsibilities nyingi mno.

1. Maji yamekauka Kidatu - TANESCO
2. Visima vya gesi vinahitaji matengenezo - TANESCO
3. Nguzo zimeanguka Mafinga - TANESCO
4. Mfumo wa kununua LUKU una shida - TANESCO
5. Bibi Chausiku amelipia umeme hajaunganishwa - TANESCO
6. Kutengeneza nguzo za zege, kukata miti chini ya nguzo - TANESCO
7. Kubadili tariffs kwenda kwenye matumizi madogo - TANESCO.
8. Tunataka kuwauzia Malawi umeme - TANESCO
This is so much to do.

Tuiboreshe TANESCO kwa kweli, whatever the means, vinginevyo tutazidi kumlalamikia tu J. Makamba kila kunapokucha.
TANESCO ndiko wakubwa wanakopigia pesa
 
Tatizo la tanesco kwa sasa siyo kusambaza umeme bali hakuna umeme wa kutosha. Hivyo hata ukiigawa tanesco katika mashirika matatu utapata wapi umeme wa kusambaza?

Jitihada ielekezwe katika kutafuta vyanzo vipya na vingi zaidi vya umeme, usambazaji hauna tatizo kubwa!
TANESCO wakubwa wanapigia pesa
 
Hivi mbona enzi za Mwendazake is like matatizo ya umeme yalikua ni kama yameisha? What is wrong now??? Tunataka kujisahaulisha hata kwa jambo ambalo hata mwaka halijamaliza? Shida ya Tanesco sio hi ambayo bwana mbunge wa Kinondoni anataka tuijue, tatizo la umeme Tanesco linaeleweka, mwendazake aliisha twambia. BAdo najiuliza, hi akili ya Watanzania kusahau vitu kwa muda mfupi namna hi inatokana na nini yaani?
 
Swali lako la kwanza:
Kwa sababu ni mashirika ya umma, anaye finance anapaswa kuwa anafahamika. Ni serikali.

Lengo hapa sio kubana matumizi, ni kuongeza tija na ufanisi. Unaongeza bajeti ili huduma iwe bora na pato liwe kubwa zaidi kutoka katika huduma ya umeme kwa ujumla wake.
Zamani tulikua na kitu inaitwa SUMATRA, ikagawanywa tukapata LATRA na TASAC, bila shaka hujawahi kuuliza nani ana finance LATRA na TASAC, hivyo ndivyo itakavyokua (kama TANESCO ikigawanywa).

Swali lako la pili:
Nani atapokea malipo ya luku.
Kwa akili tu ya kawaida, kati ya kuzalisha (production), kusafirisha (transmission) na kusambaza (supply) umeme, kitendo kinachoshabihiana zaidi na mauzo (sales) ni KUSAMBAZA.
Nadhani nimejibu swali hili.

NB: Tunaomba ieleweke wazi kwamba tunao support kwamba TANESCO igawanywe sio kwamba tunataka ikigawanywa isiongezewe chochote, hapana. Tunapendekeza ikishagawanywa ipewe uwezo (watu, fedha, teknolojia na miundombinu) ili tuone matokeo chanya kwa maana kila shirika litawajibika kwa umma katika angle yake.
Leo maji yakipungua Mtera, (TANESCO), Mpesa inashindwa kununua umeme (TANESCO), bibi kalipa elfu 27 yake hajaunganishiwa umeme TANESCO, miti imeota kwenye njia kuu ya umeme kwenye milima ya Kitonga TANESCO, Kigoma hawajauganishwa na gridi ya taifa TANESCO, Wamakonde wameiba koki ya kwenye kisima cha gesi kwenye mtambo wa kuzalisha umeme TANESCO,

Kazi kwelikweli.
Kwanini hiyo budget isiongezwe kwa Tanesco ya sasa? Kwanini rasilimali watu, technology na miundombinu isiongezwe kwa Tanesco ya sasa. Kwanini Tanesco ya sasa isiwajibike kwa umma na hiyo iltakayogawanywa ndio iwajibike?
 
Kwanini hiyo budget isiongezwe kwa Tanesco ya sasa? Kwanini rasilimali watu, technology na miundombinu isiongezwe kwa Tanesco ya sasa. Kwanini Tanesco ya sasa isiwajibike kwa umma na hiyo iltakayogawanywa ndio iwajibike?
Mkuu, nadhani nitachoka kulielezea hilo.
Nimeshasema uzi mzima huu kwamba kuna options mbili, moja kuliongezea uwezo likiwa moja hivyo hivyo, au kuligawa na kuliongezea uwezo.

Nimeshatoa ufafanuzi kwenye comments zangu za juu.

Hapa pia nilikua najaribu tu kutetea uhuru wa maoni ya Tarimba kwamba yeye anaona approach ya kuligawa ni bora zaidi.
Cha ajabu ni sisi "watanzania wenzake" tunaona kama kaleta wazo la ajabu, geni na ambalo halijawahi kutokea duniani.
Haiwezekani watanzania wote milioni 60 tukawa na mawazo yanayofanana. Suala la kugawa taasisi ili kuongeza tija na ufanisi sio geni, mifano iko mingi.

Bottom line ni kwamba TANESCO inatakiwa kuboreshwa, whatever the means.
 
Moja imewashinda tatu mtaweza?

TANESCO walipaswa wapate mshindani mmoja tu kutoka nje ya nchi awafunze adabu.

Wangeoneshwa namna ya kutoa huduma sio ujinga walionao sasa.
Hii kwangu ndio comment bora zaidi.
 
You don't get it.

Tanesco haifanyi vizuri kwenye uzalishaji wa umeme, haifanyi vizuri kwenye usafirishaji, haifanyi vizuri kwenye usambazaji.

Kuiongezea uwezo (ambao ndio tunaita ufanisi na tija) tunahitaji kuifanyia maboresho.

Kivipi, zipo njia mbili.

1. Kuligawa kwenye subunits na kuziongezea uwezo hizo subunits (More manpower, advanced technology, infrastructure, etc). Lengo la kugawa ni kuyafanya haya mashirika yanayozaliwa ku focus na ku concentrate kwenye eneo dogo (uzalishaji, usambazaji n.k) ili kuongeza ufanisi.

2. Kuliboresha kwa structure ambayo linayo sasa hivi. Kuliongezea uwezo kwa aspects nilizozitaja hapo juu na zaidi ili liweze kuongeza ufanisi.

Na hii approach ya kugawa ili kuongeza ufanisi sio ngeni kabisa, tumeona wizara zinagawanywa, (wizara ya mifugo na kilimo zamani zilikua pamoja, wizara ya habari na michezo zilikua pamoja, wizara ya afya na maendeleo ya jamii zilikua pamoja), maeneo ya utawala (sina haja hata kutaja), taasisi zinagawanywa (SUMATRA iligawanywa sasa tuna TASAC na LATRA).

Inaonekana ukiwa Rais tutakua na wizara mbili tu
1. Wizara ya elimu, afya, mifugo, ajira, madini, uvuvi, maji, uchukuzi, ardhi, maliasili, utumishi na muungano.

2. Wizara nyingine itajumuisha yote yaliyosalia.
Nimekuelewa vyema mkuu japo hujanijibu mimi, nimesoma pia comments zako toka huko juu.

Sasa mm najiuliza swali moja tu, TANESCO anafeli wapi kuajiri watu, fedha za miradi kujiendesha ktk miundombinu, Uzalishaji n.k ikiwa yeye ndo muuzaji mkubwa wa umeme Tanzania?

Mbona mimi naona hakuna shirika ambalo linapaswa kuingiza fedha nyingi hapa Tanzania kuliko Tanesco?

Naomba kueleweshwa wana JF.
 
Nishati sio Kitu cha Kuchezea kabisa, Tanesco iendele kuwa State Owned Entity kwa Masilahi mapana ya Nchi, Katika Vitu nyeti Nchi hii ambayo si vya kuchezea ni Nishati acheni masihala wazee
Dadavua kama hautajali.
 
Thinking ya Tarimba iko chini sana sidhani kama huyu jamaa hata fomfoo alimaliza , ndio wale wale tu umeme unakatika kinavunjwa kitengo cha Mawasiliano. Mkiambiwa muwe mnachagua watu angalau wanaojitambua mnakua wabishiiiiii, haya ndio matatizo yake sasa, huyui akacheze tu mamichezo yake ya kubeti kule sportspesa hana anachojua zaidi
 
1. Maji yamekauka Kidatu - TANESCO
2. Visima vya gesi vinahitaji matengenezo - TANESCO
3. Nguzo zimeanguka Mafinga - TANESCO
4. Mfumo wa kununua LUKU una shida - TANESCO
5. Bibi Chausiku amelipia umeme hajaunganishwa - TANESCO
6. Kutengeneza nguzo za zege, kukata miti chini ya nguzo - TANESCO
7. Kubadili tariffs kwenda kwenye matumizi madogo - TANESCO.
8. Tunataka kuwauzia Malawi umeme - TANESCO

Nimekuelewa...
 
Shirika linahitaji maboresho makubwa zaidi kuliko hao "mtu mmoja mmoja" hapo juu.

Management effective inahitaji kiongozi mahiri!! Kuongoza ni kuonesha njia kwa wale unaowaongoza. ! I do not see that in the current TANESCO line up!
 
Sijui unapata wapi ujasiri wa kumuuliza mwingine kwanini ana maoni X na sio maoni Y.

Nakuuliza kwasababu wewe ndio umeweka hizo options mbili na hujajenga hoja ya kuonesha ipi ndio chaguo lako!!! Unasema tu Kuwa inahitajika kuboresha technology inayotakiwa kuboresha shirika na ndio hapo unauluzwa kuwa hayo maboresho yanafanya kazi kwa kuivunja Tanesco tu? Jibu hoja iliyo mezani kwanini tuvunje shirika na kuwauzia wahuni!!

Mliuza TTCL mkapata 10% yenu; halafu mtawala mwingine akaja akalinunua shirika lile lile kutoka kwa mliemuuzia kwa bei kubwa! Huo ni ujinga usio kipimo na inawezekana Tanzania tu!!! Halafu yule yule aliyekiwa dalali wa kuiiuza TTCL ndio mnamfanya Mwenyekiti wa TANESCo ; mnataka tuwaeleweje? Hili sio Taifa la watu wote walio wapumbavu!
 
Nakuuliza kwasababu wewe ndio umeweka hizo options mbili na hujajenga hoja ya kuonesha ipi ndio chaguo lako!!! Unasema tu Kuwa inahitajika kuboresha technology inayotakiwa kuboresha shirika na ndio hapo unauluzwa Kuwa hayo maboresho yanafanya kazi kwa kuivunja Tanesco tu? Jibu hoja iliyo mezani kwanini tuvunje shirika na kuwauzia wahuni!!
Nadhani tuishie hapa. Maana tumeanza kulishana maneno sasa, sikumbuki wapi nimesema tuwauzie hao uliowaita wahuni.
Uwe na siku njema.
 
Nishati sio Kitu cha Kuchezea kabisa, Tanesco iendele kuwa State Owned Entity kwa Masilahi mapana ya Nchi, Katika Vitu nyeti Nchi hii ambayo si vya kuchezea ni Nishati acheni masihala wazee
Hilo hatujakataa ila ili kuongeza ufanisi inabidi tanesco baadhi ya sekta wawaachie kampuni binafsi kwa muongozo maaalum

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom