Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Kuna hoja kwanini inatokea hivyoMbara ukinunua kitu cha thamani Zanzibar utakiacha TRA.
Yaani ni Bora ukiagize kutoka China utafanyiwa delivery hadi home.
1. Kodi za ushuru wa kuingiza bidhaa zinatofautiana. Zanzibar wana ushuru kodi ndogo na pia uchochoro wa kukwepa kodi. Wana bandari huru kwahiyo bidhaa zinaingia tu hovyo na viwango duni
TRA wapo sahihi kwasababu ukiacha vitu viingie utawaumiza Watanganyika na kuua biashara
2. Kodi za TRA za Zanzibar zinabaki huko haziji hazina Dar es Salaam. Ukiacha milango wazi TRA hawatakuwa na mapato.
Wanachofanya TRA ni kuzuia abuse! ikiwa tutaacha bidhaa ziingie hovyo basi tufungue mipaka yote
Laiti tungekuwa na ushuru sawa wa forodha na kodi, na pesa za TRA zinakusanya makao makuu hapo tungeelewa, kwa hali ilivyo TRA wapo sahihi, vingenvyo Mtanganyika utaumia kisa kuwafurahisha wananchi wa nchi jirani
TRA wapo sahihi, huyu mbunge ni wale wale!