Mbunge Twaha Mpembenwe akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka Mpya wa Fedha 2024-2025 Bungeni Jijini Dodoma

Mbunge Twaha Mpembenwe akichangia hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka Mpya wa Fedha 2024-2025 Bungeni Jijini Dodoma

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
"Natoa pole kwa Wananchi wa Jimbo la Kibiti na Jimbo la Rufiji kutokana na kadhia ya mafuriko, nawaomba wananchi waendelee kuwa na subira kwani Serikali ipo kazini inaendelea kuwashughulikia wananchi ambao wamepatwa na mafuriko" - Twaha Ally Mpembenwe, Mbunge wa Jimbo la Kibiti

"Namshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa na nzuri anayoendelea kuifanya ndani ya nchi na katika Sekta ya Mifugo na Uvuvi. Rais amefanya uwekezaji Kilwa, sasa inaenda kujengwa Bandari nzuri ya Uvuvi inayoenda kuwa Bandari ya kihistoria. Nampongeza Abdallah Ulega kwa Uchapakazi, Ubunifu na utekelezaji wa Matokeo"

"Uwezeshaji Vijana kiuchumi hasa kupewa Maboti, nakuomba Mheshimiwa Abdallah Ulega, pale Kibiti kuna Kata ya Salale, Kata ya Kiongoloni, Kata ya Mbochi, Kata ya Msala na Kata ya Mtunda yameathirika sana na mambo ya mafuriko. Vijana pale mazingira ya maisha siyo rafiki. Naomba tengeneza mpango kutokana na uhalisia na utoe tamko mbele ya Bunge"

"Pwani ya Kusini kuanzia Mkuranga, Kibiti, Rufiji, Kilwa, Lindi ni waathirika katika Mifugo. Naomba Waziri wa Mifugo na Uvuvi, wakati umefika kuharakisha Sera ya Mifugo ili twende kuwa na Mifugo biashara, kutenga maeneo sahihi kwaajili ya Mifugo. Maeneo ya kwetu Kibiti, ukiamka asubuhi unakutana na Ng'ombe 150. Waziri leta Sera twende tukatunge Sheria, haiwezekani tuwe na Mifugo kiholelaholela"

"Katika Kata ya Makoloni kuna Mifugo ya Ng'ombe takribani 1250 ambao wapo Visiwani, na kwa Taratibu za Visiwa Mifugo hairuhusiwi kwenda. Naomba Waziri wa Mifugo na Uvuvi harakisheni leteni Sera mpya ili iweze kutusaidia tuweze kuwa na Mifugo yenye tija"

"Natamani kuona eneo la Mifugo na Uvuvi ambalo Mheshimiwa Rais amewekeza fedha nyingi sana na anaendelea kuwekeza basi sasa iweze kuchangia ipasavyo katika Pato la Taifa (GDP). Kuna asilimia 1.8, miaka 2-3 iliyopita tulikuwa juu zaidi maana yake tunakimbia mbele huku tukirudi nyuma"

"Mhe. Abdallah Ulega, kaa vizuri na Wataalam wako, tunataka kuona sekta nzima ya Mifugo inakwenda kuchangia katika Pato la Taifa ili kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi na jitihada ambazo anaziingiza katika sekta ya Mifugo na Uvuvi" - Mhe. Twaha Ally Mpembenwe, Mbunge wa Jimbo la Kibiti.

 
Back
Top Bottom