Stori: WAANDISHI WETU
Hadi gazeti hili linaondoka kwenye Kanisa
Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa
Mkombozi, Sinza jijini Dar juzi saa 10: 00
jioni , ndoa ya Mbunge Vicky Kamata
iliyokuwa ifungwe hapo iliyeyuka .
Vicky Kamata akiwa na Charles walipokuwa
matembezini nchini China .
Vicky Kamata ambaye ni Mbunge wa Viti
Maalum kwa tiketi ya UVCCM , Mkoa wa
Geita alikuwa afunge ndoa na mwanaume
aliyejulikana kwa jina la Charles wa jijini Dar .
KATEKISTA AZUNGUMZA NA IJUMAA
WIKIENDA
Baada ya kuona muda unakwenda bila
kuwepo kwa dalili za wahusika kufika
kufunga ndoa hiyo ambayo harusi yake
ilidaiwa ingetumia shilingi milioni 96 ,
wanahabari wetu walimtafuta Baba Paroko,
Cuthbert Maganga ili kumsikia anasema nini
kuhusu hilo.
Hata hivyo , mtu aliyedai ni katekista wa
kanisa hilo alisema paroko alikwenda hija,
Buguruni , Dar .
Kuhusu ndoa ya Vicky Kamata , katekista
huyo alidai Jumapili ya Mei 18, 2014 ndani
ya ibada za kanisa hilo ilitangazwa hadharani
laivu kwamba haitafungwa.
Vicky Kamata akiwa amelazwa baada ya
kuugua ghafla katika Hospitali ya Tabata
General jijini Dar .
SABABU ZA KANISA
Habari za ndani zilidai kuwa kanisa lilibaini
upungufu mkubwa kwa bibi harusi na
kumwambia ndoa haitakuwepo .
Upungufu huo ni pamoja na Vicky Kamata
kushindwa kuwasilisha cheti chake cha
ubatizo , pia hakuwahi kupata kipaimara.
Ilidaiwa kuwa vitu hivyo kwa uchache wake
ni kikwazo kikubwa kwa mtu kufikia daraja la
Sakramenti ya Ndoa .
SABABU ZA NDANI
Ukiachana na sababu hizo za kanisa , Ijumaa
Wikienda lilichimbua na kubaini sababu kuu 3
ambazo zilikuwa kisiki cha kufungwa kwa
ndoa hiyo .
Vicky na Charles wakila bata.
SABABU YA KWANZA
Kwa mujibu wa chanzo, mwanaume aliyetaka
kufunga ndoa na Vicky ana ndoa nyingine ya
kanisa na imejaliwa kupata watoto kadhaa
hivyo isingekuwa rahisi kufungwa kwa ndoa
nyingine kwa mujibu wa maandiko ya Biblia .
Mume mmoja mke mmoja mpaka kifo
kiwatenganishe .
MKE ATINGA BUNGENI
Chanzo kilizidi kudai kuwa wiki iliyopita,
mwanamke huyo ambaye jina halikupatikana ,
alitinga bungeni na kuonana na Spika wa
Bunge , Anne Makinda ambapo alijitambulisha
ndiye mke wa Charles anayetaka kufunga
ndoa na Vicky Kamata .
Mke wa bwana harusi alikuja Dodoma juzi ,
akasaidiwa kuonana na spika na mbunge
mmoja ( jina tunalo) .
Alimwambia spika yeye ndiye mke wa ndoa
wa Charles, ila walitengana . Lakini alisema
pamoja na kutengana huko, ndoa ya Kikristo
haifungwi mara mbili labda mmoja afe. Kwa
hiyo mumewe hawezi kufunga ndoa na
Vicky , kilisema chanzo.
SABABU YA PILI
Sababu ya pili ilielezwa kuwa , Vicky
asingeweza kufunga ndoa hiyo kwani
mwanaume huyo alishatoa mahari kwa
msichana mmoja ( jina tunalo) wa jijini Dar na
ukweni anajulikana .
Alishatoa mahari kwa msichana mwingine
mbali na Vicky , ukweni anajulikana .
Vicky Kamata akiwa katika pozi na
mwanaume aliyepanga kuoana naye
anayejulikana kwa jina la Charles wa jijini
Dar .
Sasa ilipotoka ile picha yake kwa mara ya
kwanza kwenye Gezeti la Ijumaa ( Mei 16 ,
2014) yenye kichwa cha habari ndoa ya Vicky
itatumia shilingi milioni 96 ikawa kasheshe
kwa yule msichana na ukweni, ndiyo jamaa
akaamua kutangaza kubatilisha ndoa na
Vicky , kilisema chanzo.
SABABU YA TATU
Sababu ya tatu ilitajwa ni kitendo cha
kuumwa. Wikiendi iliyopita , Vicky aliugua
ghafla na kulazwa katika Hospitali ya Tabata
General jijini Dar kwa hiyo isingekuwa rahisi
ndoa kufungwa Jumamosi kutokana na hali
yake kuwa mbaya .
WAANDISHI WATINGA HISPITALI
Ijumaa iliyopita , waandishi wetu walitinga
kwenye hospitali hiyo na kukutana na daktari
mmoja ambaye alikiri Vicky kulazwa hapo
lakini alikataa waandishi wasimuone kwa
sababu hayuko katika hali nzuri kiafya . Ni
kweli Vicky kalazwa hapa lakini hamuwezi
kumwona, hayuko katika hali nzuri , anahitaji
kupumzika jamani , please , alisema daktari
huyo.
HATIHATI ILISHAKUWEPO
Katika Gazeti la Uwazi la Mei 20 , 2014
ukurasa wa mbele kulikuwa na habari ndogo
yenye kichwa kisemacho ; NDOA YA MIL . 96
YA VICKY KAMATA HATIHATI KUFUNGWA.
Katika habari hiyo ilielezwa kuwa ndoa hiyo
isingefungwa kutokana na kuibuka kwa
mizengwe kibao.
Habari za ndani zilisema mizengwe hiyo
iliibuka katika hatua za mwisho na
kusababisha mwanaume kuamua kubatilisha
ndoa hiyo ambayo ilikuwa ifungwe Mei 24,
mwaka huu jijini Dar .
KIONGOZI MKUBWA SERIKALINI
Ilidaiwa kuwa baada ya kuibuka kwa zengwe
na mume kutangaza ndoa basi , Vicky aliumia
na kuzifikisha habari hizo kwa Spika Makinda
ambapo naye alizifikisha kwa kiongozi mmoja
mkubwa serikalini , hasa bungeni.
Kiongozi huyo alichukua jukumu la kumvutia
waya bwana harusi na kumsihi kutochukua
mawazo hayo na ikibidi ndoa ifungwe lakini
mwanaume huyo alikataa katakata akisema
mambo hayo ni ya kifamilia zaidi kwa hiyo
yaachwe kwenye familia .
MAMA SITTA ASIKITIKA
Habari zinazidi kusema kuwa kati ya watu
ambao wamehuzunishwa na kutofungwa kwa
ndoa hiyo ni Mbunge wa Viti Maalum ( CCM) ,
mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta
ambaye aliposikia kuyeyuka kwa ndoa hiyo
alisikitika si kwa sababu alikuwa kwenye
vikao vya harusi , bali pia aliuona wakati
mgumu atakaoupata Mhe. Vicky .
WABUNGE WAULIZIA MICHANGO YAO
Pamoja na yote yaliyojitokeza, habari zinadai
kwamba baadhi ya wabunge waliochanga
pesa ili kufanikisha harusi hiyo tangu juzi
wameanza kuulizia michango yao wataipataje
kwa vile harusi basi tena !
Huku Dom ( Dodoma ) hakukaliki bwana.
Baadhi ya wabunge wameanza kuulizia
michango yao, wanasema kama harusi haipo
basi na chao wakipate, alisema mbunge
mmoja akiomba kuhifadhiwa jina.
WABUNGE WATAJWA KUINJINIA
Mbunge huyo alikwenda mbali zaidi kwa
kusema kuwa kuna wabunge wametajwa
kuinjia zengwe la kutokufungwa kwa ndoa
hiyo kwa sababu wanazozijua wao ambazo
Ijumaa Wikienda haikupewa lakini inaendelea
kuzichimba .
VICKY KAMATA
Vicky alipotafuwa kwa njia ya simu
Jumamosi iliyopita ili azungumze lolote
kuhusu kuyeyuka kwa ndoa yake
hakupatikana hewani .