Jana tulionya kuhusu watu madiwani wa CHADEMA kutokujihusisha na kitendo chochote kitakachoruhusu uchaguzi ufanyike bila wao kuwepo. Uchaguzi sasa umefanyika na CCM wamechukua Halmashauri na hiyo imetoka.
Diwani wa TLP tayari sasa keshapata unaibu meya.
Narudia tena nilosema jana, CCM wanapotaka kitu na wewe ukaweka mizengwe, ama watakuhamisha, au watakuundia kesi ulale ndani wafanye wanavyotaka au watakutuma usafiri nje ya nchi au watakulaza hospitali kwa nguvu hata kama huumwi ila wapitishe wanachotaka. Nia ya CCM ilikuwa ni kuhakikisha walau madiwani wawili wa CHADEMA hawaingii kwa kikao na hilo wamefanikiwa.
CHADEMA mnapoona kuwa mnaelekea kushinda, mjitahidi sana kutokuwa na hasira. Muepuke kumshikia manati kuku wenu kwani wapita njia wanaweza wakapiga mayowe wakifikiri ni vibaka. Kila jambo lifanyiwe uchunguzi wa kina. Epukeni kumkimbiza kichaa alowanyanganya taulo. CCM inajifanya kichaa ili uikimbize watu wakushangae wakati yenyewe inakamilisha mambo yao. Ukirudi wameshamwaga maji yako na sabuni wamechukua.