Tetesi: Mbunge wa Arusha Mjini pamoja na Meya wasakwa na Jeshi la Polisi

Nahisi wewe ndo Lema mwenyewe na kama siyo basi wewe unaweza kua unawatetea watu bila kuwajua,mtu hawezi nyanyuka tu bila sababu eti akaenda kuliamulu jeshi limkamate Lema,lazima kuna shida mahala,umeeleza ukiegemea upande mmoja na kumlaumu mkuu wa mkoa lakini yamkini kuna jambo,siku hzi waTanzania tunaakili tunaweza kuyapima maneno mnayotoa
 
Kwa jinsi anavyomuombea mabaya Rais wetu hakika Lema anatakiwa kunyea debe ili ajifunze adabu kwa wakubwa
 
AR ina wenyewe ndugu yangu hakuna cha gamba au mbaga,Kuna wazawa.
Ukimgusa mzawa yeyote wa AR alafu ukiwa ni idokooo hapo imekula kwako hata kama unafanya kazi ikulu ya Obama lazima itakula kwako.
jpm kama anasikia piga huyu mtu chini umweke mzawa,hapo utakuwa umepatia.
 
Afadhali hivyo viwanja vianzishwe manake mbuga ya Serengeti ipo huko lakini watalii wanatua KIA wanaenda kuona wanyama na kurudi hawalali huko. Kiwanja cha serengeti kikiwa kizuri basi midege itakuwa inatua huko na watalii watalala huko na ni karibu kwenda kuona fisi na nyumbu wa serngeti kwa gharama nafuu. Uchumi wa wana Serengeti utaimarika na watafaidi matunda ya maliasili aliyowamegea muumba. Nyie mtaendelea kufaidi matunda ya Mlima Kilimanjaro.
 
Tuliaminishwa mda wa siasa na mambo ya uchaguzi yamepita na kuwa sasa ni muda wa "HAPA KAZI TU" lakini sasa imekuwa ni muda wa mtafutano,visasi na dhuluma za ajabu ajabu.Maendeleo yatakuja vipi kama sehemu zinazochangia kodi kubwa kwa njia ya Utalii zinavurugwa kila leo.Wakati mwingine mtu unapata mawazo ya ajabu sana kuhusu viongizi wa hili Taifa na watu wake.
 
Arusha ilitulia wakati fulani hadi mikutano mikubwa ya kimataifa ikarudi ......sasa hivi mmeanza tena siasa zenu za kipuuzi.....

Siasa za nani zaidi hazitatufikisha popote.!
Siasa za kipuuzi zitaimaliza Arusha. Lema anapaswa kujitafakari upya kama anastahili kuendelea kuwa mbunge
 
Mzawa!!!!
 
Japo mara nyingi huwa ushauri haufuatwi lakini nadhani ka ccm haitaki kujifuta yenyewe Arusha na sehemu nyinginezo Tz wateule wa rais waliopelekwa huko waende kuitengeneza ccm iliyo kwisha haribika sana machoni mwa Watz.
Picha mbaya haiondolewi kwa matendo mabaya. Wateule wa rais, hebu onesheni mambo mema saana ya ccm. Heshima, utu, na haki kwa kila mtu bila ubaguzi.
Mh Gambo, twajua kuwa una imani kuwa Chadema hawawezi lolote, sasa, tafuta mbinu ya kuonesha zaidi makubwa ya ccm. Hospitali ziongezewe uwezo, barabara zipanuliwe vizuri, projects zinazofanyika Ar sasa hivi uzisimamie zionekane kweli ni bora. Achana na kushindana kimwili na Lema, shindana naye kwa kuonesha mema ya ccm.
Kamata kamata ni kumwongezea umaarufu Lema &Co. Sikio la kufa halisikii dawa. Usiwe sikio la kufa Gambo.
 
Nyie ndio hamnazo kabisa. Hata kama lema angechaguliwa na kura asilimia mia ya watu wa arusha bado yuko chini ya mamlaka ya serikali kuu inayowakilishwa na rc na dc. Chadema lazima watambue serikali kuu inaongozwa na ccm. Maneno ya kumkejeli rais au kumtakia balaa kama alivyofanya lema juzi yanaonyesha jinsi lema asivyokua na busara na alivyokua mtu wa shari.
 
Siasa za kipuuzi zitaimaliza Arusha. Lema anapaswa kujitafakari upya kama anastahili kuendelea kuwa mbunge
Tatizo lipo kwa Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo kufanya mambo kwa kuingia mipaka ya wenzake bila sababu za msingi
Kwa jinsi anavyomuombea mabaya Rais wetu hakika Lema anatakiwa kunyea debe ili ajifunze adabu kwa wakubwa
 
Wazungu huwa wakifika arusha wanahisi kama wako kwao(climate condition),sasa szan kama chato wataweza kukaa
 
..wasije tu wakamkaza mkewe huko kwenye vituo vya polisi...si jambo la kujuvunia kukamatwa na hawa majamaa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…