Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,281
- Thread starter
- #41
Ushauri mzuri sana kwa Gambo
Japo mara nyingi huwa ushauri haufuatwi lakini nadhani ka ccm haitaki kujifuta yenyewe Arusha na sehemu nyinginezo Tz wateule wa rais waliopelekwa huko waende kuitengeneza ccm iliyo kwisha haribika sana machoni mwa Watz.
Picha mbaya haiondolewi kwa matendo mabaya. Wateule wa rais, hebu onesheni mambo mema saana ya ccm. Heshima, utu, na haki kwa kila mtu bila ubaguzi.
Mh Gambo, twajua kuwa una imani kuwa Chadema hawawezi lolote, sasa, tafuta mbinu ya kuonesha zaidi makubwa ya ccm. Hospitali ziongezewe uwezo, barabara zipanuliwe vizuri, projects zinazofanyika Ar sasa hivi uzisimamie zionekane kweli ni bora. Achana na kushindana kimwili na Lema, shindana naye kwa kuonesha mema ya ccm.
Kamata kamata ni kumwongezea umaarufu Lema &Co. Sikio la kufa halisikii dawa. Usiwe sikio la kufa Gambo.