Tetesi: Mbunge wa Arusha Mjini pamoja na Meya wasakwa na Jeshi la Polisi

Tetesi: Mbunge wa Arusha Mjini pamoja na Meya wasakwa na Jeshi la Polisi

Gambo ni tatizo arusha na ameletwa kwa mpango maalum muwe nae makini kuna dogo mmoja ananyemelea ubunge hapo arusha gambo kaletwa ili amtengenezee mipango.
Gambo namwonea huruma sana hata Magesa Mulongo alikuwa kama yeye leo hayupo
 
Jeshi la polisi mkoani Arusha linajipanga kumkamata mbunge wa Arusha Mjini na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha leo usiku au alfajiri sana kesho
Taarifa za uhakika zinasema kuwa polisi wanashinikizwa na Mkuu wa mkoa wa Arusha Bwana Mrisho Gambo kumkamata mbunge huyo kutokana na mgogoro mkubwa uliopo kati ya wawili hao.Shinikizo la RC Gambo limewachukiza baadhi ya maofisa wa polisi hasa kitengo cha upepelezi kwa kuwa wao polisi hawana sababu ya kumkamata,hata hivyo Bwana Mrisho Gambo amesisitiza kuwa lazima wakamatwe kutokana na kile yeye RC anachodai kuwa Mbunge amemkosea yeye binafsi na mh Rais.
Katika mikutano ya hadhara aliyofanya mbunge pamoja na madiwani akiwepo Mstahiki meya walitangaza kutompa ushirikiano wowote RC na DC kwa kile walichoita matumizi mabaya ya madaraka yanayofanywa na RC na DC.Tamko hilo limeungwa mkono na wananchi mbalimbali katika jiji la Arusha na viunga vyake.Kufuatia uungwaji mkono huo RC amekosa amani na imani ya kutembea bila ulinzi mkali wa polisi.
Itakumbukwa kuwa mke wa Mh. Mbunge wa Arusha mjini Bi. Neema Lema alishikiliwa na jeshi la polisi kwa masaa manne juzi Jumatano wiki hii Octoba 26 . Neema Lema alishikiliwa kwa amri ya mkuu wa mkoa wa Arusha Bwana Mrisho Gambo! Inadaiwa kuwa Neema amekuwa nguzo kuu ya ujasiri wa mumewe na katika kila hatua amekuwa na mchango mkubwa sana kwa mumewe ambaye ni mbunge aliyechaguliwa kwa zaidi ya kura 65,000. Taarifa zinazidi kusema kuwa mkuu wa mkoa amechukizwa na kitendo cha line ya simu ya Mbunge kuwa na jina la Neema ambaye ni mkewe.
Baada ya kuhojiwa kuhusu line inayohisiwa kutuma sms yenye neno *Shoga* Bi Neema Lema alikana kuhusika na kumiliki line iliyotuma sms hiyo,hata hivyo alisema neno Shoga sio tusi bali ni rafiki,na akatoa mfano kuwa kwa utamaduni wa wanawake huitana Shoga!
Baada ya kushikiliwa kwa muda wa masaa manne Bi. Neema ametolewa bila masharti, wala bila kuwa na kesi yoyote ya kujibu.

My take
RC acha kutumia madaraka vibaya,je ni hasira ya kuzomewa kula burka ulikotaka kupotosha umma?Je ni hasira ya hotuba kali za Mbunge?Hizi hotuba zinaeleza ukweli?je utaweza kushindana na Ukweli?
Kamwe mtu aliyeteuliwa na mtu mmoja hawezi kushinda mbunge mwenye kura 65,000 ni swala la muda tu.
Acha kuandika vitu vya hovyo hovyo, mkuu wa mkoa awalazimishe polisi wamkamate lema ili iweje,kama anaitajika na jwshi la polisi taratibu zipo
 
Kwa jinsi anavyomuombea mabaya Rais wetu hakika Lema anatakiwa kunyea debe ili ajifunze adabu kwa wakubwa
Tangu lini maombi huwa ni jinai? Kuna waislam wakati Mrema akiwa Waziri Mambo ya Ndani, walisema watafanya ibada kjmwombea mabaya lakini sikuwahi kusikia walishtakiwa au hata kusikia kulikuwa na mipango ya kumshtaki.

Jukumu kuu la serikali ni kuhakikisha maendeleo ya watu yanapatikana.
 
Dah ila mwandishi kanifurahisha yaani ameonesha mahaba makubwa sana kwa kamanda, kijana shupavu na kiboko ya ccm mkoani arusha. Kweli ifike sehemu wakuu wa mikoa kama kuna haja ya kuwepo basi wachaguliwe na wananchi wa mikoa husika maana ni kero wakati mwingine. Huyu gambo atashindana na lema ila nina hakika hatashinda.
 
Alikuwa anatafuta kazi kwenye kampuni lakini wenye kampuni wanasema 'hawa waliofikia ngazi kubwa serikalini siyo wa kuwaajiri, huwa ni wasumbufu'.

Vijana wanaoteuliwa kwenye nafasi kubwa serikalini ni wa kuwaonea huruma:
1) Uwezekano wa kubakia kwenye nafasi zao ndani ya serikali mpaka uzeeni ni finyu sana
2) Wakitemwa serikalini, ni ngumu sana kuajiriwa kwenye sekta binafsi
3) Wengi wao huwa hawana uzoefu wala uwezo wa kuendesha shughuli binafsi kutokana na kutokuwa na uzoefu katika masuala ya ujasirimali
4) Uzoefu wao katika kutoa amri, huwaondolea werevu wa kitaalam
Tatizo wanajisahau sana wakiwa kwenye madaraka bado hawajifunzi mimi nilipokutana naye kwenye gari moja niliongea naye sana lakini nimefunza viongozi wengi wakiwa madakani huwa wanajisahau sana wakitoka ndo wanakuwa na akili.
 
Arusha imeshavurugika hata watariii hawaendi tena. Naomba wana arusha mchague mbunge mwingine ili arusha itengamaeee
 
Alikuwa anatafuta kazi kwenye kampuni lakini wenye kampuni wanasema 'hawa waliofikia ngazi kubwa serikalini siyo wa kuwaajiri, huwa ni wasumbufu'.

Vijana wanaoteuliwa kwenye nafasi kubwa serikalini ni wa kuwaonea huruma:
1) Uwezekano wa kubakia kwenye nafasi zao ndani ya serikali mpaka uzeeni ni finyu sana
2) Wakitemwa serikalini, ni ngumu sana kuajiriwa kwenye sekta binafsi
3) Wengi wao huwa hawana uzoefu wala uwezo wa kuendesha shughuli binafsi kutokana na kutokuwa na uzoefu katika masuala ya ujasirimali
4) Uzoefu wao katika kutoa amri, huwaondolea werevu wa kitaalam
Kwahyo anakumbuka shuka kukishakucha hata ningekuwa Mimi sikuajiri kijana kujiingiza kwenye vyeo vya kuteuliwa ni hatari kwa future yako maana uhakika wakubaki ni mdogo, au ukiingia utawala mpya kutemwa nje NNE.
 
Unashindwa kujionea huruma wewe Rofa
Umuonee huruma mkuu wa mkoa !!!
Hazikutimu
Wewe hujui chochote bora ungenyamaza kimya kila kwako ni siasa hatuko kwenye siasa hapa niambie Magesa Mulongo kwa sasa ni nani kwenye utawala wa JPM?
 
Mmmmh!...watu waliokua wakiendeshwa na ma vx saiv wanakimbizana na mabasi.maisha ni noma haya!..future is a mystery umdhaniae kumbe badae anaweza kukuomba msaada hata ww.ishini vizuri na watu wandugu hata kama leo una cheo na madaraka
 
Kwa taarifa yenu kuna mpango mkakati wa kuhakikisha kuwa jiji la Arusha linadhohofishwa na "rire lijiji retu kure kwetu" kupandishwa chati...

Kuna kamati maalum imeundwa kufanikisha zoezi hilo...
Wataanza na vurugu ili wazoroteshe sekta ya utalii Arusha.
Kilele kitakuwa ufunguzi wa viwanja vikubwa vya ndege Mwanza (Serengeti Intl. Airport) na Chato (Rubondo Intl. Airport)..

Wao wanasema ware jamaa wamekura sana sasa ni zamu yetu..!!
Mimi humu ni mjumbe tu kuwafikishieni hizi dondoo...
Arusha inabebwa na Geographical location....Arusha ni kati kati ya Mlima Kilimanjaro, Serengeti na Nairobi...hapo bado uwepo wa Mbuga za Ngorongoro, Tarangire, Manyara, Arusha National park n.k

Sasa kama kuna mikakati basi ijumuishe na kuihamisha Arusha hapo ilipo...otherwise ni matumizi mabaya ya rasilimali kwa kupaka upepo rangi.

Hili ombwe la uongozi likemewe tu kwa bidii zote ili tubaki salama.
 
Huyo lema ndio mandazi kweli,jitu halijielewi hilo wangelitia ndani hata mwaka litie adabu,team makengeza ni shida sana shule kichwani zero kazi kusumbua watu tu
 
Back
Top Bottom