Tetesi: Mbunge wa Arusha Mjini pamoja na Meya wasakwa na Jeshi la Polisi

Tetesi: Mbunge wa Arusha Mjini pamoja na Meya wasakwa na Jeshi la Polisi

Mm nashauri itafutwe njia ya wawili hao Lema na Gambo wakae na kuzika tofauti zao na kila kiongozi afanye majukumu yake bila kuingilia majum ya mwingine tunataka arusha isonge mbele kimaendeleo bila malumbano ya viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa
Hawawezi kuzika tofauti zao mgambo ana baraka zote kutoka kwa magu
 
Kwa mikoa yote tanzania AR ni pagumu,panatakiwa kiongozi aliye pelekwa hapo atumie akili na si kutaka ajulikane kuwa mimi ndo mimi hakuna mwingine.
MAGESA alishindwa vijana wa dotcom ndo watauweza?.
Wakubwa walifanya makosa makubwa sana kumtoa mtangulizi wa huyu jamaa,hakika angeifuta CDM AR na 2020 ingekuwa ni historia,ila maji yakisha mwagika..................na tayari ni aibu kumtoa huyu jamaa na kumrudisha aliyetoka.
 
Gambo analazimisha kuchota mapesa halmashauri kupitia mkurugenzi ila Lema na madiwani wamem'bananisha sasa Gambo anajaribu kurusha miguu
 
Gambo analazimisha kuchota mapesa halmashauri kupitia mkurugenzi ila Lema na madiwani wamem'bananisha sasa Gambo anajaribu kurusha miguu
Gambo kwa Lema atapiga salute mwenyewe amuulize Magesa Mulongo kuhusu Lema atamwambia
 
Kinachotakiwa kufanya ni kila mtu kufanya kazi kwa kuheshimu mipaka yake ya kazi bila kuingilia mwenzake
Arusha ilitulia wakati fulani hadi mikutano mikubwa ya kimataifa ikarudi ......sasa hivi mmeanza tena siasa zenu za kipuuzi.....

Siasa za nani zaidi hazitatufikisha popote.!
 
Shida hapo ugomvi wao hawa wawili unachochewa na mkulu na ndio tatizo kubwa ktk mkoa huo
Huo mgogoro hauna faida kwa wananchi kila mtu afanye kazi kwa kuheshimu mipaka yake.
Gambo anatakiwa kujua huu siyo muda wa siasa
 
Yupo Mkuu mmoja wa wilaya nayeye hakuteuliwa safari hii,

nilikutana nae kwenye basi la mwendokasi nae kashika bomba,

Mpaka anatia huruma uwa wanajisahau sana hawa jamaa.
Wanajisahau sana wakishatumika wanatupwa huko namwonea huruma sana Gambo huko Arusha nguvu anayotumia kupambana na Lema badala ya kufanya kazi
 
Arusha ilitulia wakati fulani hadi mikutano mikubwa ya kimataifa ikarudi ......sasa hivi mmeanza tena siasa zenu za kipuuzi.....

Siasa za nani zaidi hazitatufikisha popote.!

Jamaa katumwa kazi..... Ni suala la muda tu...
 
Gambo ni tatizo arusha na ameletwa kwa mpango maalum muwe nae makini kuna dogo mmoja ananyemelea ubunge hapo arusha gambo kaletwa ili amtengenezee mipango.
 
Wengi labda wanafikiria watadumu kwenye nafasi hizo aisee Magesa Mulongo alikuwa anapambana sana na Lema leo hayupo tena ameshasaulika
Alikuwa anatafuta kazi kwenye kampuni lakini wenye kampuni wanasema 'hawa waliofikia ngazi kubwa serikalini siyo wa kuwaajiri, huwa ni wasumbufu'.

Vijana wanaoteuliwa kwenye nafasi kubwa serikalini ni wa kuwaonea huruma:
1) Uwezekano wa kubakia kwenye nafasi zao ndani ya serikali mpaka uzeeni ni finyu sana
2) Wakitemwa serikalini, ni ngumu sana kuajiriwa kwenye sekta binafsi
3) Wengi wao huwa hawana uzoefu wala uwezo wa kuendesha shughuli binafsi kutokana na kutokuwa na uzoefu katika masuala ya ujasirimali
4) Uzoefu wao katika kutoa amri, huwaondolea werevu wa kitaalam
 
Back
Top Bottom