Mbunge wa CCM apendekeza Vyuo Vikuu vianze kutoa Nusu Degree kwa Wanafunzi wanaoishia njiani

Mbona huo utaratibu upo!
Sema wanafunzi wenyewe huwa hawafuatilii kwa kuwa hajui!
 
Ana point... Inaweza kuwa mwaka WA kwanza certificate, wa pili diploma wa 3 advanced diploma wa nne degree. Kwa hiyo popote utakapoishia unaondoka na cheti chochote
Sasa alichochangia ni kipi hapo, maana huwa wanapewa.
 
Mkuu, katika globalization ya leo na ushindani wa soko la ajira bado unawaza nusu degree za kutumika Tanzania peke yake?
Naam!
Certificates zinatumika Tanzania na hakuna shida. Hivyo hizo nusu degree ambazo zitajulikana kam stashahada zilizoboreshwa, zikitumika Tanzania tu. Sioni ubaya wowote Mkuu.
 
Kama wanajitunukia ma degree kila siku ni sawa kama akili yake imemtuma hayo
Kesho watasema tuwe na ndoa nusu kama hujamalizia mahari
Wana upumbavu hawa
 
Huo ni ufinyu wa fikra na upuuzi kwa nchi yenye utajiri mkubwa kama Tanzania.

Serikali itafute chanzo cha tatizo na kulitibu ili asiwepo mwanachuo hata mmoja wa kuishia njiani kimasomo kisa tu amekosa ada na fedha za kujikimu.

Ni heri wabunge hata 100 wafutwe plus vyeo lukuki zisizo na maana pamoja na mikakati mingine ya kubana matumizi na kuongeza kipato, ili mwanachuo watimize ndoto zao kupitia elimu.
 
ALIVYOUA ELIMU ILI ATAWALE WATANGANYIKA KAMA MIFUGO YAKE:

Na,Hayati Mchungaji Christopher Mtikila

Ili kuwa Mungu wa taifa hili ,dikteta Nyerere alilazimika kuwatiisha watu wa nchi hii kwa kuwapofushwa kabisa kifikra mpaka tukawa kama mataahira,kwa kufuta elimu bora iliyotolewa awali na kubakiza kwa mfano kwa shule ya msingi ambazo alizikomeshea darasa la Saba ,masomo makuu yakawa Kiswahili,Siasa ya kuwapofusha kifikra na kuwafanya wamwabudu,na utamaduni au halaiiki ,walimu wakiwa mbumbumbu wa UPE.

Kwahiyo kila mwaka watoto takribani laki Saba wakawa wanaishia darasa la Saba na upofu huo,na hawa ndio sehemu kubwa ya Taifa letu Leo.Elimu aliifisha mpaka chuo kikuu na kuondoa hata umuhimu wa Lugha ya kiingereza,ili kuwatenga kabisa Watanganyika na Ulimwengu wa uhuru na maendeleo ya kifikra na teknolijia baada ya kuwapofusha.Vinginevyo kwa utajiri wa nchi yetu,leo kila mkoa ungekuwa na chuo kikuu na Tanganyika ingekuwa Ulimwengu wa kwanza kiuchumi.
 
Niliwahi kusikia kuwa St. Joseph University of Tanzania (SJUT) wanafanya hiyo kitu. Mtu akikosa ada au hata akifeli kuendelea na masomo ya mwaka unaofuata basi anapewa cheti kwa muda aliosoma.

Mfano mtu anasoma shahada ya uhandisi umeme (miaka 4), akimaliza mwaka wa 1 wa masomo na kuamua kutoendelea, basi anapewa cheti, akisoma miaka 2-3 anapewa diploma na akipiga miaka 4 anapewa digrii..niliona ni jambo poa kuliko mtu kukosa kitu, yaani kuonekana ni kama form 6 tu
 
Huko ccm vichaa wote sema hawajui kama wao vichaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…