Mbunge wa Gairo, Shabiby ataka fedha za bima kwa wote zikatwe kwenye laini za simu

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008

Mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Shabiby ameishauri Serikali kukata Sh2,000 kila mwezi kwenye laini za simu huku wabunge, wafanyabiashara na wafanyakazi wakikatwa Sh10,000 ili fedha hizo ziwe chanzo cha mapato kwa Bima ya Afya kwa wote.​


Amesema kuna wamiliki wa laini za simu milioni 72 nchini ambao makato yao kwa mwaka yataingiza Sh1.72 trilioni na zikijumlishwa za Sh10,000 kwa mwezi za wabunge, wafanyabiashara na wafanyakazi, Serikali itapata kwa mwaka takribani Sh2 trilioni.

Shabiby amesema hayo leo wakati akichangia mapendekezo ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Pia, ameshauri vituo vya kutolea huduma – hospitali, zahanati na vituo vya afya – vinavyomilikiwa na Serikali vibinafsishwe kama ilivyo Abu Dhabi na Korea Kusini.

Ameshauri madaktari na wauguzi waliopo nchini wajiunge na kubinafsishiwa hospitali badala ya kuwa chini ya Serikali. Shabiby alisema maana ya kutaka laini za simu zitumike kama chanzo cha mapato ni kutokana na anavyoona baada ya Bunge kupitisha muswada wa Bima ya Afya kwa wote na kusainiwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa sheria, kuna hatari bima hiyo ikachangisha wananchi ambao awali walishindwa kuchangia hata Sh10,000 na Sh30,000 za mfuko wa CHF.

Kwa mujibu wa Shabiby, wanufaika wa bima katika Watanzania 100 ni watu wanane ambao wanalipa bima.

“Hasa ukiichukulia hii hatuna chanzo maalumu cha kupata pesa ambazo zinaweza zikasaidia wananchi wa vijijini na watu masikini pamoja na wananchi wa mijini, hata mijini wapo masikini wengi tu, tena hata zaidi ya hao wa vijijini,” amesema na kuongeza:

“Nimeona tulizungumzie bila woga, najua kuna mawazo tutatoa na watu watatukana kwenye mtandao, lakini acha watukane. Hii bima ya afya, ushauri ninaotoa tupende tusipende lazima tuingize chanzo cha muhimu ambacho tutakipata kwa urahisi,” amesema.

Amesema fedha hizo zinaweza kusaidia wananchi hasa wa vijijini ambao kipato ni kidogo kwa kutowawekea ukomo wa matibabu, kwamba wenye fedha ndogo na matibabu yao yanakuwa hayahusu magonjwa mengine makubwa.

Shabiby alishauri baada ya vyanzo hivyo, Serikali ihamie kwenye vyanzo vingine kama mazao kwa kutoza kila kilo moja Sh1 au Sh2.

“Kama mtu hana laini ya simu ina maana huyo masikini wa kutupwa, huyo hafai hata kuchukuliwa Sh200, atatibiwa kutokana na mifuko,” amesema.

“Sasa hiki kinachokuja, najua wengi mtanishangaa lakini ndio ukweli. Hizi hospitali, zahanati na vituo vya afya vijijini vifikie hatua ya kubinafsishwa. Huo ndiyo ukweli, tuige habari ya Korea Kusini, tusiwe wavivu, nendeni mkaangalie Korea Kusini wanafanya nini Abu Dhabi wanafanya nini,” amesema.

“Korea Kusini hakuna hospitali ya kijijini ambayo ni ya Serikali, hakuna kituo cha afya ambacho ni cha Serikali, zahanati zote zimeingizwa kwenye mfumo mmoja, vituo vya afya vyote vimo kwenye mfumo mmoja,” alisema.

“Lipo jengo kubwa wamejenga watu wa intaneti wapo hapo, ripoti zote zinakwenda kule mtu mwenye zahanati akitaka kulipwa na bima, wale lazima wanakague ile zahanati ilimtibu nini X hapa, kwamba nilimpiga x-ray, lakini nikaona nimtibu malaria nikampa Kwinini (Quinine), wale hawatalipa gharama za x-ray kwa sababu ni utapeli na watalipa gharama za matibabu ya malaria pekee,” alisema.

Alishauri Serikali iwe na mfumo wa aina hiyo utakaobaini wenye vitendo vya utapeli kwenye hospitali na zahanati. Shabiby alisema hospitali zinazopaswa kubaki chini ya Serikali ni zile za rufaa kama Hosptali ya Taifa ya Muhimbili.

Alisema utaratibu huo pia utaondoa tabia ya baadhi ya madaktari wa hospitali za Serikali na ambao wanafanya kwenye hospitali binafsi kuwa madalali wa kupeleka wagonjwa kwenye hospitali binafsi kwa kuziponda za Serikali kwamba hazina vifaa vya kutosha.

Mipango iliyopo ya Serikali ni kuwezesha huduma za bima kwa wote kwa mapato yatokanayo na ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji vyenye kaboni, vinywaji vikali, bidhaa za vipodozi, michezo ya kubahatisha, ada ya vyombo vya moto, na mapato yatokanayo na ushuru wa miamala ya kielektroniki kwa kadri itakavyopendekezwa.

PIA SOMA
- Mbunge Santiel Kirumba: Kila laini ikatwe 50 tujenge barabara
Your browser is not able to display this video.
 



MY TAKE:

huyu mbunge kwanza hana njaa! magari yake mpaka nauli Tsh 49,000 kutoka Dar kwenda dodoma yaan kila sku yeye anaingiza mamilioni ya hela

Anachukulia poa kuwakamua maskini ili wasaidie maskini wenzao!

yeye anapata mshahara 17Milioni kwa mwezi - Mwalimu anapata laki 3 kwa mwezi! halafu wote mkatwe kwenye simu

Namuombea afe mdomo wazi kama vile anafosi kutoa haja kubwa iliyokaza

 
Laini zangu mbili kwa mwezi 4000 kwa mwaka 48000...fine tunaweza tukakubaliana na hoja yake lakini hizi Hela nazitoa kwa bima hii hiii ambayo serikali inajikopesha Kila kukicha? Bima ilojaaa Kila aina ya ubadhirifu
 
Wao wanalipwa mamilioni kila mwezi hivyo kukatwa 10,000 sio kitu lakini sisi makapuku huku mitaani tunakaa wiki hatujaweka vocha je hiyo 2,000 tutaitoa wapi?

Lakini serikali kwa upande wake kama wana dhamira ya kweli kuhusu hiyo bima ya afya kwa wote haiwezi kushindwa,

inawezaje kuwalipa wenza wa viongozi pesa ya bure ikashindwa kutoa pesa kwa ajili ya bima ya afya kwa wananchi wake?
 
Kashiba Shabiby, hamjui mwenye njaa. Tumelalwmika tozo kwenye miamala ya simu juzi juzi tu hapa yeye anataka watukate na bima ya afya tena??

Lkn kwann tumnyonye mwananchi kwenye simu wakati tuna rasilimali kibao??

Mbali na rasilimali, serikali inaweza:-
1. Kupunguza mshahara ya wabunge kutoka milioni 18 kwa mwezi na kuwa milioni 10 kwa mwezi.
2. Kupunguza posho za vikao vya bunge kutoka laki 3 kwa siku na kuwa elfu 50 kwa siku

Yakifanyika haya, hata vichaa watakatiwa bima.
 
Mbunge wa Gairo kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Ahmed Shabiby ameishauri Serikali kukata Tsh 2,000 kila mwezi kwenye laini za simu kwa watu wa kawaida, na wabunge, wafanyabiashara na wafanyakazi wakatwe Tsh 10,000 ili fedha hizo ziwe chanzo cha mapato kwa Bima ya Afya kwa wote.

"Kuna wamiliki wa laini za simu milioni 72 nchini ambao makato yao kwa mwaka yataingiza Tsh Trilioni 1.72 na zikijumlishwa za Tsh 10,000 kwa mwezi za wabunge, wafanyabiashara na wafanyakazi, Serikali itapata kwa mwaka takribani Tsh Trilioni 2". - Shabiby

Amesema hayo leo Bungeni wakati akichangia mapendekezo ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
-LemutuzUpdates
-Tusiache kumuombea kwa mungu aliyekuwa member mwenzetu.
Blogs yake bado inasonga mbele!
Apumzike kwa amani.
 
Wakipunguza pesa zao kutoka 18m mpaka laki tano tutakuwa tumesave ngapi ?

Hivi hawa watu wapo out of touch anajua ni wangapi hizo line zao ni kupokea pekee na kupiga mpaka wajukuu zao au watoto wao wawatumie ?!!!

Aisee the audacity of these people !!!
 
Kwani Wafanyakazi na Wafanyabiashara kodi tunazolipa hazitoshi au mnaanza tena uhuni.
 
Hao wabunge mnawachagua nyinyi walala hoi kisa mmepewa t-shirt [emoji153] na kofia za kidumu
 
Yule mwalabu koko alisema tukatwe tozo kwenye wakaweka ma tozo ya kutufilisi bado huyu nae mwalabu koko mwingine anasema tukatwe buku mbili na serikali hapo ikija haitaweka buku mbili wataweka 5000 ama 4000 wanaona ni kitu poa tu kama walivoweka tozo.Kama wanataka kutusaidia wakate mia tano kwa mwezi hiyo ni poa tu
 
Serikali haishindwi kutenga fedha kwa ajili ya bima ya afya kwa wote na pia bima ya afya nao wanakusanya fedha nyingi sana tatizo la nchi hii ufisadi wa kutisha unaofanywa kwenye mfuko wa bima hata wananchi tukitoa 10000 kila mtu bado fedha haitatosha mwarobaini hapa ni KATIBA MPYA kila kitu kitakaa sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…