Mbunge wa Gairo, Shabiby ataka fedha za bima kwa wote zikatwe kwenye laini za simu

Wakaangalie(kujifunza) ,korea kusini na Abu Dhabi

Kwamba , wanaenda walewale walioenda Dubai ,kujifunza kuhusu dp world ..... Aise!
 
Coment hii aione kabla hajalala leo
 
Linapokuja swala la pesa huwa namuamini zaidi mfanyabiashara kuliko mtu mwingine tu wa kawaida au wa fani nyingine,shabiby ana hoja.
Tatizo ni hawa mboga mboga,waliokwapua hela za wastaafu mpaka mfuko umesinyaa,wataweza kuziangalia tu 2trn zikiwa zinasubiri kuchukuliwa na wizara ya afya kulipa madeni????
 
Haya ndio mawazo ya wabunge wa CCM. Akili zao zimo tumboni. Ameongra utumbo tupu. Kwani miongoni mwa wanaomiliki simu, hakuna masikini? Mpuuzi kabisa.
 
Mawazo mazuri lakini maswali ni haya:
1. Wapigaji wameondoka?
2. Mikopo waliyokopeshana na mingine kukopeshwa kwa mashirika ya umma imerejeshwa?

Tatizo la NHIF sio fedha bali usimamizi mbovu kama ilivyo katika mashirika mengi ya umma, wakipewa matrioni usishangae serikali ikaanza kuchota fedha kama ilivyofanya kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Vv
 
Mkuu serikali pia imechota matrilioni pesa kutoka NHIF na bado haijazirejesha
 
Hii sio sawa matibabu ni swala la mtu binafsi mfano mpaka sasa nina bima yangu nimaokotoeza nikajiunga na kifurushi halafu unikate tena kwenye line yangu ya cm hiyo haiko sawa
 
Ameongea kitu muhimu tatizo hana akili..

Wazo la kuwa na chanzo cha uhakika ni bora sana ila kwenye simu amewaza bila akili..

Binafsi napendekeza vyanzo vifuatavyo

1. Posho za wabunge na Rais
2. Ununuzi wa magari
3. Wafanyakazi wageni vibali vyao viongezwe tozo kuchangia bima.
4. Vituo vya mafuta viongezewe tozo kwa sababu ya uchafuzi wa mazingira
5. Biashara za pombe na bar na kumbi za starehe ziongezewe tozo ya bima ya afya
6. Leseni za madini na mafuta ziongezewe tozo
7. Cooperate tax ijumuishe tozo ya afya

8. Mtu akilipa Tax yoyote, 1% iongezwe kwa ajili ya bima

9. Wafanyakazi wote wakatwe 0.5% kwa ajili ya bima.

10. Leseni za udafirishaji zote zijumuishe tozo ya 1% kwa ajili ya bima.

Baada ya hapo itungwe sheria kali sana ya kumanage huo mfuko.
 
Huo ufanisi wa kumudu kuendesha huo mfuko kwa ufanisi utakuwepo? Maana CAG anaeleza kwenye ripoti yake kuwa serikali imekopa pesa nyingi kwenye huu mfuko mpaka leo hii haijarejesha sasa tuendelee kuamini serikali haitarudia madudu iliyofanya huko nyuma kuchukua pesa za mfuko? Kingine kwanini matumizi ya serikali yasipunguzwe kama vile posho, mishahara hasa ya wabunge, manunuzi ya magari kila mwaka wa fedha (512 bilioni) kinachopatikana kielekezwe kwenye mfuko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…