Pre GE2025 Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu, atoa msaada wa kumpyuta zenye thamani ya milioni 9 Shule ya Sekondari Ihanamilo

Pre GE2025 Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu, atoa msaada wa kumpyuta zenye thamani ya milioni 9 Shule ya Sekondari Ihanamilo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mbunge Kanyasu Akabidhi Kompyuta zenye thamani ya Tsh Mil 9.

Geita - Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini, Constantine Kanyasu, ametekeleza ahadi yake kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Ihanamilo kwa kukabidhi kompyuta tano zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tisa.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Kanyasu alisema kuwa utekelezaji wa ahadi hiyo umetokana na ombi lake kwa Naibu Waziri Mkuu, Dotto Biteko, ambaye alimsaidia kutafuta wafadhili waliowezesha upatikanaji wa kompyuta hizo. Alibainisha kuwa lengo kuu ni kusaidia walimu wa shule hiyo kuepuka changamoto ya kutembea umbali mrefu kwenda mjini kwa ajili ya kudurufu mitihani ya wanafunzi.

"Nimekuja kuwashukuru sana walimu na viongozi wa kata hii kwa maandalizi mazuri ya ziara ya awali, ambayo imezaa matokeo chanya, ikiwemo upatikanaji wa umeme katika shule hii. Nimefanya ziara pia katika vijiji vingine, na ninafurahi kuona kuwa umeme tayari umeshafika," alisema Kanyasu.

 
Back
Top Bottom