Kosa ni liko kwa wana wa nchi. Tumelala fofofo kiasi ambacho hata kama mtu ana nia ya kututetea anakatishwa tamaa njiani. Trust me. Ukiamua kumtetea mtanzania kukata tamaa njiani ni rahisi mno mno. Mwananchi atafanyiwa unyama mbaya sana na vyombo vya dola au kiongozi halafu atamwendea mtetea haki yeyote na kusema nimefanyiwa hivi na vile, naomba unisaidie kupiga kelele lakini usitaje kama mimi ndiyo nimelalamika, zungumza kijumla jumla tu. Sijui una umri gani lakini mimi enzi za Mtikila kuichachafya nilikuwa nimeshapata akili. Lakini mpaka anafariki alikuwa tayari ameshakata tamaa na kupungza kabila ule moto na wakati mnwingine kuwa upande wa serikali.