Huyu Mama sio mpiga kura, kwa namna yoyote hawezi kupata kutoka kwa mbungeKuna wakati wabunge sijui wanawaza nini hawajui kujichanganya na matatizo japo madogo tu ya wananchi , tarehe 5 mwezi huu , katika daraja la mto wami lori lilitumbukia mtoni na dereva wake , dereva alifanikiwa kutolewa na wataalam wa kuogelea , lakini lori bado mpaka leo lipo ndani ya maji , kwa mujibu wa mmililiki wa lori Mama mmoja ambaye ni mzee kwa kweli gari hili alilinunua baada ya kudunduliza hela zake na kupata kiasi cha milioni 18 akaamua kununua hilo gari ikiwa ndio safari yake ya kwanza likapata ajali , toka ajali itokee yule mama kapiga kambi pale wami akiomba msaada , mpaka jana kiasi cha milioni mbili kilichangwa na wamama ili kumsaidia , na zinaitajika kiasi cha milioni tano ili kutoa lori hilo katika mto.
NIMSHAURI MBUNGE WA ENEO HILO FANYA JAMBO KUMSAIDIA HUYO MAMA HATA KAMA SIO MPIGA KURA WAKO , ILA AJALI IMETOKEA KATIKA ENEO LAKO.
Hivi serikali haina kitengo cha maafa?
Japo huyu mana alitakiwa kuwa na bima kubwa lakini serikali haiwezi kuweka mkono?
Ridhiwani naye alikuwa pale naye kashindwa kusolve tatizo dogo hivi hata kumdhamini?
Sent using Jamii Forums mobile app
Sema YethuEnzi za rizone ilikuwa ni baba yake akiwa madarakani. Sasa hivi naye na anamsujudia tu Yesu.
Mbunge ni Rizwani kikwete , alikuepo eneo la tukio amepiga selfie akaondoka
Rizwani ni mbahili sijawahi kuona Duniani, hawezi Kucha ngoja hata senti tano
Haliwezi faa tena???Mama anahitaji msaada wa psychological intervention kuliko kingine.
Bado yupo kwenye state ya shock and denial ni kawaida sana inapotokea ‘significant life event’ baadhi yetu kukataa ukweli kwanza.
Lorry limeshapotea ata likitolewa probabilities za kurudi barabarani ndogo.
Inabidi apatikane mtaalamu atakae tumia lugha na mbinu sahihi kumpa ukweli vinginevyo tusishangae mama anapata uchizi bila ya psychological intervention kwa hali yake.
Hiyo ilitakiwa kuwa kazi ya polisi na zima moto.
LORY MILIONI 18???
Kuna urefu wa mita kadhaa kutoka darajani mpaka kwenye mkondo wa mto sidhani impact ya kuanguka urefu huo gari alitahitaji matengenezo.Haliwezi faa tena???
Duh!
Sidhani kama kitengo cha maafa cha serikali kina husika na maafa binafsi ya mtu mmoja mmojaHivi serikali haina kitengo cha maafa?
Japo huyu mana alitakiwa kuwa na bima kubwa lakini serikali haiwezi kuweka mkono?
Ridhiwani naye alikuwa pale naye kashindwa kusolve tatizo dogo hivi hata kumdhamini?
Sent using Jamii Forums mobile app
tatizo mihemko ikizidiJamaa kachapia tu. Huyu mama amesema mara kadhaa kuwa alinunua lori kwa shillingi milioni 83.
Hana Comrehensive insuarence?
RiziMoko ni bahiri nakumbuka kipindi Niko chuo tuliwahi kumfuata tufanye nae kazi kwenye project moja hivi , daah sitasahauHaliwezi faa tena???
Duh!
Anaonekana kbs....mie mbunge nayemwelewa Sana hana ubahili ni bashe!.. bashe mwombe msaada ni chap!RiziMoko ni bahiri nakumbuka kipindi Niko chuo tuliwahi kumfuata tufanye nae kazi kwenye project moja hivi , daah sitasahau
Kuna wakati unajiongeza sio lazima ufuate majukumu yako ya kikatiba au kinyadhifa , kwasababu tukisema tufuate majukumu ya kikatiba au kinyadhifa basi wengi watakua wanakosea na kuvunja utaratibu , kwa mfano hizi milioni kumi kumi zinazotolewa katika kwaya za makanisa na ujenzi wa makanisa , vimilioni milioni vinavyotolewa tolewa katika ziara za mkulu sizani kama vipo katika majukumu.... ila kujiongeza tuWatanzania mlio wengi hamzijui au hamtambui majukumu ya wabunge.