Mbunge wa Jimbo lilipo daraja la Wami, msaidie huyu mama

Huyu Mama sio mpiga kura, kwa namna yoyote hawezi kupata kutoka kwa mbunge
 
Hivi serikali haina kitengo cha maafa?
Japo huyu mana alitakiwa kuwa na bima kubwa lakini serikali haiwezi kuweka mkono?
Ridhiwani naye alikuwa pale naye kashindwa kusolve tatizo dogo hivi hata kumdhamini?

Sent using Jamii Forums mobile app

Enzi za rizone ilikuwa ni baba yake akiwa madarakani. Sasa hivi naye na anamsujudia tu Yesu.
 
Mama anahitaji msaada wa psychological intervention kuliko kingine.

Bado yupo kwenye state ya shock and denial ni kawaida sana inapotokea ‘significant life event’ baadhi yetu kukataa ukweli kwanza.

Lorry limeshapotea ata likitolewa probabilities za kurudi barabarani ndogo.

Inabidi apatikane mtaalamu atakae tumia lugha na mbinu sahihi kumpa ukweli vinginevyo tusishangae mama anapata uchizi bila ya psychological intervention kwa hali yake.
 
Nashangaa pia Viongozi wahusika wa Eneo mbona kama hawaoni hiyo opportunity aisee. Wamsaidie yule mama
 
Haliwezi faa tena???
Duh!
 
Haliwezi faa tena???
Duh!
Kuna urefu wa mita kadhaa kutoka darajani mpaka kwenye mkondo wa mto sidhani impact ya kuanguka urefu huo gari alitahitaji matengenezo.

Sasa kama kulitoa tu 7m; vipi kuhusu kulivuta, parts na gharama za kulitengeza hadi lirudi barabarani.

Ndio maana kuna mmoja wa wale wavuvi akasema kuna lorry lingine pembeni ya gari la mama, na mwenyewe kawapa ruhusa ya kuchukua chochote wanachoweza bure lakini wameshindwa kutoa ata matairi.

Hali ya mama ni kama mgonjwa wa cancer anapoambiwa kwa mara ya kwanza, mtu anapopata upofu, kilema au wazazi wanaopoteza mtoto bila ya kutarijia it takes time kukubali ukweli. Ndipo alipo mama gari limepotea.
 
Na yeye hana pesa ya maana anaingiaje kwenye biashara ya malori? Auze hilo Lori likiwa huko huko chini ya maji akatafute biashara nyingine isiyokuwa na risk kubwa. Mbunge wetu hana pesa
 
Hivi serikali haina kitengo cha maafa?
Japo huyu mana alitakiwa kuwa na bima kubwa lakini serikali haiwezi kuweka mkono?
Ridhiwani naye alikuwa pale naye kashindwa kusolve tatizo dogo hivi hata kumdhamini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Sidhani kama kitengo cha maafa cha serikali kina husika na maafa binafsi ya mtu mmoja mmoja
 
RiziMoko ni bahiri nakumbuka kipindi Niko chuo tuliwahi kumfuata tufanye nae kazi kwenye project moja hivi , daah sitasahau
Anaonekana kbs....mie mbunge nayemwelewa Sana hana ubahili ni bashe!.. bashe mwombe msaada ni chap!
 
Watanzania mlio wengi hamzijui au hamtambui majukumu ya wabunge.
Kuna wakati unajiongeza sio lazima ufuate majukumu yako ya kikatiba au kinyadhifa , kwasababu tukisema tufuate majukumu ya kikatiba au kinyadhifa basi wengi watakua wanakosea na kuvunja utaratibu , kwa mfano hizi milioni kumi kumi zinazotolewa katika kwaya za makanisa na ujenzi wa makanisa , vimilioni milioni vinavyotolewa tolewa katika ziara za mkulu sizani kama vipo katika majukumu.... ila kujiongeza tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…