Mbunge wa Kahama Mjini ashauri Vyuo Vikuu kuwajibika kutafuta ajira kabla ya kusajili Wanafunzi

Mbunge wa Kahama Mjini ashauri Vyuo Vikuu kuwajibika kutafuta ajira kabla ya kusajili Wanafunzi

Huyo mzee yupo sawa, kupoteza muda kwenye masomo yasiyo ya practical ni ujinga na kuendekeza uvivu, na huyo mzee anajua umuhimu wa experience ya maisha na kazi na siyo hizo theory hata wanaufundisha hawazielewi na hawawezi kuzitumia, kinachotakiwa ni muda mfupi tu darasani wa kufanya practical na kujua vitu kwa vitendo mtu anaenda kufanyia kazi alichosoma akiwa na experience yake na siyo hizo theory za kizamani wakati lecture anachezea chaki na siku hizi ni mambo ya vitini tu hata hao malecture hawaingii madarasani kila siku maana wanajua hakuna umuhimu ila wanachohitaji ni mishahara tu, wanachuo wafundishwe practical muda mfupi warudi mtaani watasaidia na training za mara kwa mara makazini na iwe ni lazima kwa kila muajiri hata wanaweza wakaweka ofisi za labor kitengo cha training maofisi iwe ni lazima kwa kila mtumishi na anafanya mtihani anapewa certificate ya hiyo training kadili utaalamu utakavyokuwa unabadilika na hao walimu vyuoni wakapunguzwa, kuna mmoja alipewa kazi ya store wakati kasoma degree ya procurement kwamba siyo hazi yake na hawezi kufanya kazi ya kuchafuka, sasa anasoma masters hiyo hiyo akiamini ndo atafanikiwa kazi tofauti bila kukaa store wala kusimamia wapakiaji.
 
High thinking capacity huyu jamaa na while ajaenda

Ndio maana wasioenda shule uwa wanakuwa matajiri huku walioenda shule wanabaki kukimbizana na vibarua
Umeongea point mkuu..jamaa yupo vizuri kichwani lkn 'sisi wasomi' tunamshambulia badala ya kujibu hoja zake zenye mashiko

Na ni kweli hawa watu ndy huwa matajiri zaidi kuzidi wao waliosoma
 
Elimu inahitaji marekebisho makubwa sana@ haliwezekani mtu ana bachelor ya economics, lakini bado mia tano ya vocha inampiga chenga mpaka apige mzinga kwa mdogo wake aliyemaliza la Saba tu.
 
Nilicheka Sana aliposema wanaosomea taaluma km ya udaktari ni Sawa Tu wakisoma chuo miaka mitatu maana anachokisomea anafanya practical kwenye hospitali,Hilo wwnanchi hatuna tatizo nalo,sasa wenzangu na mie mfano mtu anasomea procurement sijui wenyewe mnaita manunuzi unasomaje chuo miaka mitatu..unanunua nn miaka yote hiyo km siyo kupoteza muda tu..yaani unasomaje miaka mitatu manunuzi alafu unarudi nyumbani unamwambia mzazi nimesomea manunuzi Nani sasa atakuajiri kwenye Duka,miezi name inatosha degree

Huyu Mwamba na msukuma wananifurahisha sn
Hivi huyu naye ni kampuni ya std 7?
 
Elimu inahitaji marekebisho makubwa sana@ haliwezekani mtu ana bachelor ya economics, lakini bado mia tano ya vocha inampiga chenga mpaka apige mzinga kwa mdogo wake aliyemaliza la Saba tu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hii kitu alikua anaifanya dkt Richard masika akiwa mkuu wa chuo pale ATC.

Vijana wa mwaka wa mwisho walikua wanaenda interview mara kwa mara hata chuo hawajamaliza.

Wakimaliza tu,
wananyakuliwa juu kwa juu.

ALIKUJA KUONDOLEWA PALE KIHUNI SANA kwa KUTOFAUTIANA MTIZAMO NA JIWE
Kabisa, hata wakati yupo DIT, kipindi namaliza watu walikuwa tayari wameshapata ajira, ukimaliza mtihani wa mwisho, unaenda kupiga kazi
 
Huyu dingi nae inaelekea kichwani hamnazo... Vyuo viwatafutie wanafunzi ajira kwani ni kazi yao hiyo? Inawahusu nini.
Kuna vyuo duniani vinavyofanya hivyo. Kwa mfano kama unasomea Nursing, chuo kinakuwa na uhusiano maalum na mahospitali huko na wanafunzi wake wanakwenda huko mahospitalini mara kwa mara kwa ajili ya practicals na mambo mengineyo. Wanaanza mapema wakiwa mwaka wa kwanza. Wakija kufika mwaka wa 3 wanakuwa wameshajenga mahusiano na hospitali hizo na inakuwa rahisi sana kwao kuajirika moja kwa moja. Na unakuta hospitali zingine zinaanza kuwatumia hata kabla hawajamaliza chuo.

Hii wanaita job placement na ukiangalia kwenye profiles za vyuo hivyo utakuta chuo kinajigamba kuwa kina job placement nzuri kwa wahitimu wake hasa wa nyanja fulani fulani.

Njia nyingine ni kwa chuo kuweza kuzalisha wahitimu wazuri sana walioiva sawasawa; wahitimu ambao wanaajirika. Hii ndiyo silaha ya vyuo vikubwa kama Harvard na vinginevyo. Watu wakiona tu una shahada ya uongozi au sheria kutoka Harvard wanajua umeiva, Engineering ya MIT au caltech, udaktari ya John Hopkins n.k.

Tatizo sisi tumefungua vyuo lukuki bila kujali ubora matokeo yake tunazalisha watu ambao hawaajiriki na ukiwaweka katika kiwango cha kimataifa wanashika mkia.

Hili ni tatizo kubwa na suluhisho lake siyo rahisi kama Kishimba anavyotaka kutuaminisha hapa.
 
Mimi nimemuelewa kwamba ...vyuo viwe vinashirikiana na waajiri, viwanda, makampuni etc katika uaandaaji wa mafunzo wanayotoa.......badala ya kusoma notes za lecture za tangu 1980!.....Hii idea yake nimeiona katika mji niliosoma ...viwanda na waajiri wote wanaoendesha shughuli zao katika mji ule kilipo Chuo walikuwa wanahusika katika uandaaji wa nini kifundishwe ...walikuwa wanatoa mapendekezo ya aina ya mhitimu wanayemtaka. Kulikuwa na ushirikiano mkubwa sana kati ya chuo na waajiri.
 
Ukiwa na mbunge msomi lazima aongee kisomi na ukiwa na mbunge kanjanja Ni lazima aongee kiukanjanja,dunia nzima upo utaratibu wa kusoma elimu ya juu,sio miezi 8 urudi nyumbani,huyu mzee upeo wake upo hivo.
Mkuu Pilot wa Ndege za Jeshi la Marekani ana 21 years of age... je kwa Mtanzania anahitaji umri gani aendeshe dege la Bilion za Kitanzania angani na itue salama waeza Tafuta Pilot wa umri huo Tanzania? ndio ujue huyo mzee kuna vitu anavielewa so anatumia Siasa kufikisha ujumbe... Tanzania tunadeal na ufuata fuata wa kizamani wakati watu wanasomea ajira sio tunasomea sifa... Ndio Maana Ma prof wengi kazi zao ni kufundisha tu kwani wanapenda elimu... So Kwa maisha ya sasa tunatakiwa kufanikiwa kimaisha na sio kufanikiwa kielimu so elimi tusome kufahamu tunachokihitaji kwa 100% Mzee yupo right
 
Shida yetu ukiweka maandishi mengi na mwingine akiweka kipeperushi chenye sentensi moja walio wengi hujadili kipeperushi ambacho aliyekiandaa lengo lake ni kutrend kwenye mtandao.

Hoja za msingi 10 zinauliwa kwa kujadili kipeperushi chenye sentensi moja. This is Tanzania.
 
Vyuo kutafuta Ajira kwa Graduates ni sawa na Mentors wa wanafunzi sehemu za kazi/field na wao kulipwa.
Wasio na Elimu na wenye Fedha wanafikiri Elimu ni Fedha, walionayo wanaona Fedha sio kitu kuliko Elimu/Maarifa.
Hii ndiyo Tanzania.
 
Asamehemwe, hajui alisemalo. Yaani elimu ya miaka mitatu itolewe kwa miezi nane? Hayuko siriasi kabisa huyo Mbunge
Wewe ndio wa kusamehewa mzee kachana live na fact... mfano Gahrib Bilal kasomea Nuclear hadi sijui phd kuna kampuni ya kumpa kazi Tanzania? ilibidi akimbilie Siasa tu.
So kwa Tanzania yupo sawa na waezaa sema hata nchi zilizoendelea pia... Kusoma sana ni kuwa Mwalimu,Leacture n.k
 
Huyu dingi nae inaelekea kichwani hamnazo... Vyuo viwatafutie wanafunzi ajira kwani ni kazi yao hiyo? Inawahusu nini.
Nafikiri anamaanisha vyuo vifanye tafiti upya juu ya idadi ya fursa za ajira zilizopo kwenye kozi wanazofundisha. Sio kuzalisha wasomi wengi kwenye kada ambazo practically hazina soko kwenye jamii yetu.

Pia baadhi ya kozi amekosoa kwa watu kusoma muda mrefu wakati uhitaji wa soko la ajira unahitaji mambo machache tu mfano kozi ya manunuzi and the like.

Hoja anazo ila tatizo bongo wengi tunasoma vipeperushi vya summary ya sentensi moja ya alichokiongea mtu nusu saa.
 
Kuna watu wenye Sifa za Degree, Masters na PHD lakini si watu wa kuona future sifa ya cheti huwapumbaza hupambana kutafuta kazi kisha hujiona wao ndio wao... Tizama Mitifuano ya Elimu enzi za Jackson Makweta kiswahili au english Mashuleni haswa shule za Msingi ndio Matokeo ya Font Fent na kiongozi akiongea kiswahili watu wanashukuru sana maana angeongea English ingekuwa gumzo na kashfa kuwa haujui english... Kuna mtu alisema huko nje mtu anapewa mike kwenye mikutano wanaosikiliza wanaangua vicheko tu kwa lugha mbovu iliyovunjika kiingereza cha mtanzania.. Elimu fumueni kama english basi iwe hivyo na foundation zake elimu ya msingi and kama ni kiswahili basi iwe hivyo... Ndio maana wasomi wa TZ wanaishia kukariri tu na kuwa na elimu bila kuelimika... Ndio maana hakuna Slogan yeyote ya Mwanasiasa mwenye nia nzuri ya maendeleo ikafanikiwa eti Viwanda au Kilimo... and zana hakuna bulshait
 
Msomi Gani.wewe unaye shindwa kumwelewa hapa,na kuishia kutuletea hapa tuhuma zisizo na.ushahidi,hapakuwa na Serikali kipindi hicho!?Kwa Taarifa Yako hii ni aina ya uwasilishaji wa ujumbe ya kiwango Cha juu kabisa,wasomi wa makaratasi anawaacha hewani wakielea
Kiwango chako cha elimu ni sawa na Kishimba?
 
Back
Top Bottom