Mbunge wa Kahama Mjini(CCM), Jumanne Kishimba ashauri Serikali kuanzisha chuo cha wizi

Hivi yule fisadi mkata mauno aliyetumbuliwa na mkulu vipi alisha fikishwa mahakamani?
Ukiwa na chapa hizo Mambo hazikuhusu.
Kule ni kwa wasiotaka kusifu na kuabudu.
Sifu abudu kila upatapo camera sifu asubui,sifu mchana,sifu jioni ndio Kinga pekee ya utumbuzi,jela,au kupata teuzi.
 
Mtumeeeeeeeee!
Ukiwa na chapa hizo Mambo hazikuhusu.
Kule ni kwa wasiotaka kusifu na kuabudu.
Sifu abudu kila upatapo camera sifu asubui,sifu mchana,sifu jioni ndio Kinga pekee ya utumbuzi,jela,au teuzi.
 
Mbunge wa Kahama Mjini kupitia CCM Jumanne Kishimba, ameiomba Serikali ifungue chuo cha wizi kwa kuwa matukio ya wizi katika sekta za umma na Halmashauri nyingi umeshamiri kwa kiasi kikubwa na kwamba chuo hicho kitasaidia wale watu wanaoenda kuchunguza wezi, kuzijua mbinu zao na kuwabaini.

Hayo ameyabainisha leo Mei 28, 2020, Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa 19, kikao cha 39, wakati wa uchangiaji wa hoja ya Kamati ya Kudumu ya Huduma za Serikali za Mitaa, na kueleza kuwa ni vyema chuo hicho kikawekwa japo kwa kutumia jina lingine ili kukomesha suala hilo.

"CAG na Waziri wa Fedha yuko hapa hawa vijana wanaoajiriwa lazima wanatoka shule inayofundisha maadili mema na uaminifu, sasa wanaenda kupambana na wizi wengine wamesoma Seminari, kwanini serikali haifikirii sasa kuanzisha chuo cha wizi, kwa maana mtu anapochaguliwa kwa sifa ya uaminifu kwenda kupambana na wezi anaenda kupambana nao namna gani? afadhali apite kwenye chuo hicho kwa miezi mitatu ili ajue akili ya wizi, hawa vijana wetu tutawamalizia magerezani na hali ya wizi ni mbaya sana" amesema Mbunge Kishimba.

Credit: EATV

Mwaka jana, Kishimba alitaka kilimo cha bangi kihalalishwe nchini Tanzania Mbunge Jumanne Kishimba (CCM) ataka kilimo cha bangi kuhalalishwa nchini Tanzania

Maoni Yangu
Kumbukeni huyo mbunge alishawahi kuomba Serikali iruhusu bangi itumike kihalali.

Daaaa hao ndiyo wabunge wetu ambao ni watunga sheria na wapitisha miswaada na mikataba mbali mbali.

Kama taifa bado tuna safari ndefu.

Kwa bahati mbaya hukumuelewa! Alitaka kusema kuwa kuwepo na mtaala unaoelezea jinsi wizi unavyotamalaki ikiwa na jinsi ya kumkamata Mwizi . Ili wahitimu wetu wakifika kazini wataweza kugundua mapema wezi. Kuna usemi wa kiswahili usemao kuwa Mwizi hushikwa na mwizi mwenzie.
 
Kwahiyo polisi wanavyo kamata waarifu na wao ni wezi??
 
Prof Assad aliwaonesha mwizi,hawa akina kushimba sijui kisima na bunge lao dhaifu wakamshumbulia Assad badala ya kumkamata mwizi waliooneshwa
 
Yawezekana hujaielewa na kupitia maandishi yako mafupi nimepata maana pana kuhusu wewe na unachokiamini hii ndio tofauti ya mtu aliyesoma philosophy na ambaye hakusoma
Usini quote in negative sense, ni kuwa nimependa the approach nothing else
 
Nawaza siku huyo mtu atakapoikosa ajira huku akiwa amefuzu mafunzo ya wizi na kufaulu kwa kiwango cha juu.
Wajuzi wa mambo haya tusaidieni
 
ulikuwa na wazo zuri mkuu, ila umeshindwa kuchagua njia nzur ya kupangilia hoja yako, polee kwa wanaokupa majungu
 
Kishimba yuko sahihi! Kama UDSM na IFM nao wameibiwa huku kwingine sindio baraa!
Hicho chuo cha wizi nimuhimu japo kibadirishwe jina kiwe chuo cha kujua mbinu za mwizi na kumdhibiti kabla ya kuiba tanzania. Kifupi.. CKKMKKT
 
Tukiacha kumjadili huyu Mbunge na kuchambua falsafa ya anachoshauri utaona huwa anapinga watawala kwa staili mpya na kupendekeza solutions kwa shadow effect. Tujadili inakuwaje mpaka RPC anajiibia au judge anajihukumu!?
 
Mbunge wa Kahama Mjini kupitia CCM Jumanne Kishimba, ameiomba Serikali ifungue chuo cha wizi kwa kuwa matukio ya wizi katika sekta za umma na Halmashauri nyingi umeshamiri kwa kiasi kikubwa na kwamba chuo hicho kitasaidia wale watu wanaoenda kuchunguza wezi, kuzijua mbinu zao na kuwabaini.

Hayo ameyabainisha leo Mei 28, 2020, Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa 19, kikao cha 39, wakati wa uchangiaji wa hoja ya Kamati ya Kudumu ya Huduma za Serikali za Mitaa, na kueleza kuwa ni vyema chuo hicho kikawekwa japo kwa kutumia jina lingine ili kukomesha suala hilo.

"CAG na Waziri wa Fedha yuko hapa hawa vijana wanaoajiriwa lazima wanatoka shule inayofundisha maadili mema na uaminifu, sasa wanaenda kupambana na wizi wengine wamesoma Seminari, kwanini serikali haifikirii sasa kuanzisha chuo cha wizi, kwa maana mtu anapochaguliwa kwa sifa ya uaminifu kwenda kupambana na wezi anaenda kupambana nao namna gani? afadhali apite kwenye chuo hicho kwa miezi mitatu ili ajue akili ya wizi, hawa vijana wetu tutawamalizia magerezani na hali ya wizi ni mbaya sana" amesema Mbunge Kishimba.

Credit: EATV

Mwaka jana, Kishimba alitaka kilimo cha bangi kihalalishwe nchini Tanzania Mbunge Jumanne Kishimba (CCM) ataka kilimo cha bangi kuhalalishwa nchini Tanzania

Maoni Yangu
Kumbukeni huyo mbunge alishawahi kuomba Serikali iruhusu bangi itumike kihalali.

Daaaa hao ndiyo wabunge wetu ambao ni watunga sheria na wapitisha miswaada na mikataba mbali mbali.

Kama taifa bado tuna safari ndefu.

It's a question of language interpretation! Ametumia lugha ya wizi lakini kinachoitwa antifraud ni kile kile. Wahasibu wakifundishwa kwa makini juu ya antifraud wanajitambua wanavyobiwa au wakaguzi watajua wahasibu wanavyoiba.
 
Back
Top Bottom