Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tukiacha kumjadili huyu Mbunge na kuchambua falsafa ya anachoshauri utaona huwa anapinga watawala kwa staili mpya na kupendekeza solutions kwa shadow effect. Tujadili inakuwaje mpaka RPC anajiibia au judge anajihukumu!?
It's a question of language interpretation! Ametumia lugha ya wizi lakini kinachoitwa antifraud ni kile kile. Wahasibu wakifundishwa kwa makini juu ya antifraud wanajitambua wanavyobiwa au wakaguzi watajua wahasibu wanavyoiba.
Ipo, lakini iko kwenye mfumo wa uchunguzi wa makosa na siyo ktk mfumo wa kawaida wa ukaguzi.Mkuu unataka kutuaminisha kuwa hadi karne hii bado kama taifa hatuna Ant fraud?
😅😅😅, wanyonge wa akili itakula kwao.Hapo atakaye kuwa vizuri darasani ndiye atakuwa anashinda mpambano
Na hapo ndipo balaa litakapoanziaHahahahaa, itabidi atumie elimu yke kujikimu mkuu
Akifikia hatua ya kuiomba serikali ianzishe kilimo cha bangi mnishtue. Huenda nikapata ajira ya Plantation manager [emoji38][emoji38][emoji38][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2445][emoji2445][emoji2445][emoji377][emoji377][emoji377]
[emoji2398]ᵃʳᵉᵉᵐ [emoji769]
Unatakiwa kuwa na akili ya hali ya juu kumuelewa Mhe. huyu. Huyu Mhe. pamoja na kujiita darasa la saba mimi namuona kama kahitimu PhD!
Mbunge wa Kahama Mjini kupitia CCM Jumanne Kishimba, ameiomba Serikali ifungue chuo cha wizi kwa kuwa matukio ya wizi katika sekta za umma na Halmashauri nyingi umeshamiri kwa kiasi kikubwa na kwamba chuo hicho kitasaidia wale watu wanaoenda kuchunguza wezi, kuzijua mbinu zao na kuwabaini.
Hayo ameyabainisha leo Mei 28, 2020, Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa 19, kikao cha 39, wakati wa uchangiaji wa hoja ya Kamati ya Kudumu ya Huduma za Serikali za Mitaa, na kueleza kuwa ni vyema chuo hicho kikawekwa japo kwa kutumia jina lingine ili kukomesha suala hilo.
"CAG na Waziri wa Fedha yuko hapa hawa vijana wanaoajiriwa lazima wanatoka shule inayofundisha maadili mema na uaminifu, sasa wanaenda kupambana na wizi wengine wamesoma Seminari, kwanini serikali haifikirii sasa kuanzisha chuo cha wizi, kwa maana mtu anapochaguliwa kwa sifa ya uaminifu kwenda kupambana na wezi anaenda kupambana nao namna gani? afadhali apite kwenye chuo hicho kwa miezi mitatu ili ajue akili ya wizi, hawa vijana wetu tutawamalizia magerezani na hali ya wizi ni mbaya sana" amesema Mbunge Kishimba.
Credit: EATV
Mwaka jana, Kishimba alitaka kilimo cha bangi kihalalishwe nchini Tanzania Mbunge Jumanne Kishimba (CCM) ataka kilimo cha bangi kuhalalishwa nchini Tanzania
Maoni Yangu
Kumbukeni huyo mbunge alishawahi kuomba Serikali iruhusu bangi itumike kihalali.
Daaaa hao ndiyo wabunge wetu ambao ni watunga sheria na wapitisha miswaada na mikataba mbali mbali.
Kama taifa bado tuna safari ndefu.
Duuuh wee jamaa acha kujifanya hamnazo bhana...wp duniani serikali iliwahi kuwa na chuo cha uharifu???ccm mna nn jamani???Unatakiwa kuwa na akili ya hali ya juu kumuelewa Mhe. huyu. Huyu Mhe. pamoja na kujiita darasa la saba mimi namuona kama kahitimu PhD!
Ni yeye Tajiri kamili.lkn ndiyo hivyo tenaHivi Kishimba huyu ni yule wa Imaraseko super Market?
Itakuwa hata utajiri wke umetokana na uharifu [emoji23][emoji23][emoji23]Ni yeye Tajiri kamili.lkn ndiyo hivyo tena