Mbunge wa Karagwe aomba Rais Magufuli alipopigia push up ujengwe uwanja wa kumbukumbu!

Mbunge wa Karagwe aomba Rais Magufuli alipopigia push up ujengwe uwanja wa kumbukumbu!

Ijengwe pia sanamu ya Mamvi mahali zoezi la kuzungusha mikono lilipozinduliwa
 
Hizi akili za kuokoteza ni noooma! Pumba kabisa hii! wabunge wa ccm wananini? ni elimu yao au ni nini? Kuna yule mwingine 'picha ya askari iliyopo pale dsm itolewe iwekwe ya Diamond!!!! Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!
 
Wabunge nao naona wamepata ugonjwa wa Mkuu wa mkoa Makonda. Wameshindwa kuweka kipaumbele cha maendeleo. Sasa kipaumbele chao kimekuwa kujipendekeza kwa magufuli.
 
Huyu munge simjui, ila nimemjulia tu juu juu baada ya kusikia kutoka kwa Nape Nauye, kwamba wameshapanga kujenga sanamu ya Rais akipiga Push-up jimboni kwake. Hili ni swala la fedhea na aibu kubwa.

Nashindwa kuelewa. Hivi huyu mbunge alichaguliwa na Magu au alichaguliwa na wananchi? Hii sanamu ndio maendeleo anayowaletea? Majanga hayaishi Tanzania

Ndiye huyu aliyesema kwamba, wapiga kura wake hawawezi kuoa wanawake wazuri wakiofia kuchukuliwa na wanajeshi. This is absurd.

Wana Karagwe wamepata Majanga !
 
Nachoka sana...!
Hongereni ccm kwa wabunge wenye mawazo mgando.hahahaha na posho wanachukua safi sana hapa pushup tu.!
 
Duh kama mbunge yuko hivi na Waziri anajibu kwa raha mstarehe hatari. Hizo hela zingesaidia Umitashumita na Umiseta ili tupate akina Messi na Ronaldo wetu nyie mnawaza sanamu na kufuta michezo. Aibu kubwa kwa Taifa.
 
Kukaa kimya bila kuchangia bungeni si kiashiria cha ujinga. Ni muda sasa tangu niishiwe hamu ya kufuatilia mambo ya bunge. Napata hisia ile kanuni ya asiechangia bungeni hatapata posho imeshapitishwa.
 
Nilishasema, unahitaji kuwa na akili kama hizi kuwa mwanaMCC!!!!
 
Hivi innocent Bash yule ninayemjua ndio kimeo hivi? Kweli dunia hii inaniambia majanga
 
Tunataka viwanda sisi viwanja vya nini wakati hizi ni Zama za hapa kazi tu
 
Wote walewale,alieuliza swali na aliyejibu,wananchi wa jimbo la Mtama na Karagwe wapime akili
nikiwasikiliza hao jamaa wawili najiona kumbe mimi naweza hata kuwa waziri mkuu maana ni mpaka aibu kwa kweli, hivi kama kiongozi wao ni hivyo sasa hao wananchi walio wachagua wako vipi kiakili? sitaki kuwatukana watu lakini ukiona familia baba mlevi mama ndio hivyo kina kaka ndio balaa utajuwa tu hii sio familia ya kuowa. wewe sasa ni waziri bado unaleta maneno ya kumkashifu aliyekuwa mgombea wa uraisi wakati mambo ya uchaguzi yameisha na wewe ni waziri wa watu wote. usimtukane mtu mgonjwa wakati wewe uko safarini basi angemsema pia speaker wake wa bunge. katika watu nawachukia huyu jamaa ndio maana mjini alipigwa chini uchaguzi wa mchujo tu akaona akimbilie bush.
 
hahahahahahahahahahahahahahahahahahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Hivi huyu bwege alipataje ubunge? Yaani badala ya kutumia muda wa bunge kujadili mambo ya maana yeye anatoa "hoja" za kijinga. Lingekuwa jambo la maana watu wapimwe IQ zao kabla ya kuchukua fomu za kugombea ubunge.
 
Eti kumbu kumbu muhimu! Nadhani hata JPM akiyasikia hili la kujenga uwanja mahali alipopiga pushup anaweza kujiuzulu urais.
 
..... kuna wakati huwa nawaza kuwa kama ccm wangebaki peke yao tz bila upinzani labda Mungu angekuwa ameisha igharikisha nchi,......... SHAME.... SHAME... SHAME.
 
Huyu Nape hawezi hata kuwa prefect kwa nchi za wenzetu,mtu kupiga pushapu iwekwe kumbukumbu?Jamani ifike mahala ccm muwe na mtu wa editing ya maswali yenu.Ni aibu kwa taifa
 
Najua Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba, @Kigwangwala na Tibaijuka ni member hapa JF, kwa nini hawawaambi wabunge wao wanaonekanaje na jamii au hata kuwaonyesha wanavyojadiliwa?
Au na wao ndio walewale?

Umesahau kuwa Nape kalipa uzito swali na kulijibu?
 
Back
Top Bottom