Tetesi: Mbunge wa Kibamba ( CHADEMA) , Mheshimiwa John Mnyika kuongea na wanahabari Jijini Dsm

Tetesi: Mbunge wa Kibamba ( CHADEMA) , Mheshimiwa John Mnyika kuongea na wanahabari Jijini Dsm

Sikuwai kumwamini Mnyika tangu kipindi cha cha pili cha Keenja mpka ushindi wake pale Loyola hata asipohama si wa kumwamini sana.
Hao Wengine ni wasanii wa kawaida.
 
Naomba kuchangia mjadala huu kidogo,kama mtanzania huru!

Kwanza,si dhambi wala ajabu mbunge au mwanachama mwingine yeyote kuhama chama chake,iwe kwa kushawishiwa au kwa hiari yake!

Watu tunaghadhibika juu ya gharama zinazotumika kurudia uchaguzi,ni sahihi kabisa kuumia kwa sababu pesa hizo zingeweza kutumika kwa mambo mengine ya muhimu zaidi kuliko uchaguzi,lakini hizo ndiyo gharama za demokrasia!(tumechagua mfumo huu,tusilalamike)

Watu wanasema hawa watu wamenunuliwa,inaweza kuwa kweli lakini wameshawishiwa,nao wakashawishika,na siasa ni pamoja na kuhakikisha unashambulia safu ya mpinzani wako kwa namna yoyote isiyovunja sheria za nchi!

Kama wabunge wa upinzani wakashawishika,(kwa sababu yoyote ile) iwe fedha,vyeo,au hiari yao tu,wananchi tunapaswa kumlaumu nani?? Je,tumlaumu anayehama au anayemshawishi kuhama? Kama ni gharama,ni nani hasa anayepeswa kulaumiwa kwa kutuingiza kwenye gharama hizo,ni mbunge anayeacha ubunge!au yule aliyemshawishi ahame?

Tukilitazama kwa jicho la ushabiki,hatutatenda haki kwenye jambo hili,inahitaji tafakuri ya kina kujua ni Nani haswa anapaswa kulaumiwa kwa hali tunayoipitia kama taifa,vinginevyo tutajikuta tunaharibu sanaaa!!!
 
Niwakumbushe tuu walobaki upinzani,dirisha letu la usajiri liko mbioni kufungwa,
 
Habari ambazo zimenifikia mimi Hivi Punde kutoka kwa Mnyetishaji wangu ndani ya CHADEMA ni kwamba, Mh John Mnyika , Mbunge wa Kibamba ( CHADEMA ) ataongea na waandishi wa habari wakati wowote kuanzia jumatatu ya October 15,2018.

Atakuwa na Mh. Joshua Nassari na Joseph Haule, wote kutoka CHADEMA.

Mbowe atakula nyama zake.

Muda utaongea.
Kwa maana hiyo wewe ndiye uliyemwandalia hotuba? Kama siyo, umejuaje kama watatangaza kujiuzulu? Na kama hawakujiuzulu utafanya nini? Hizi prediction za kishamba sana na zinaonyesha jinsi mlivyo weupe upstairs! Yaani hamjui hata namna ya ku-propagate zaidi ya kukurupuka na kuweka madhanio yenu as if unamjua sana mnyika na hata anayowaza! Usihamishe goli hapa mleteni Mo wa watu!
 
Wawachukue wote Kisha waone wapigakura misimamo yao iko wapi.
Mbunge Ni mtu mmoja. Ambaye alichakuliwa na watu zaidi ya elfu hamsini
Sasa hao waliomchagua wapo fungi gani. Kahama nao ?????????
Naona bado hujaelewa kuwa watz wanachagua mtu siyo chama kwa sasa ndiyo maana wanaoihama chadema bado wanashinda chaguzi za marudio
 
Sasa hivi imekuwa too common...!

Mtu akihama hata hushtuki yaani.
Wanaodai kuwa uhamaji umekuwa kitu cha kawaida wanajidanganya sana. Matukio ya kuhama bado yanaendelea kusumbua vichwa vya watu. Kama ingekuwa kitu kidicho cha kawaida tusingeona kuhamia kwa Mkundi wa Ukerewe kukiongelewa humu wakati alihama siku moja ambayo ndo habari za Mo kutekwa zilibamba sana.
Aje ahame Mnyika kweli halafu udai ni suala la kawaida kweli?
 
Wanaodai kuwa uhamaji umekuwa kitu cha kawaida wanajidanganya sana. Matukio ya kuhama bado yanaendelea kusumbua vichwa vya watu. Kama ingekuwa kitu kidicho cha kawaida tusingeona kuhamia kwa Mkundi wa Ukerewe kukiongelewa humu wakati alihama siku moja ambayo ndo habari za Mo kutekwa zilibamba sana.
Aje ahame Mnyika kweli halafu udai ni suala la kawaida kweli?
Hivi mkuu wabunge na madiwani wangapi wamehama ...

Kitu ambacho baadhi ya watu hatuoni jipya sana...ni kuwa huu uhamaji umekuwa in series...akihama mtu leo baada ya mwezi anahama mwingine..

Sasa ukiangalia sababu ya wao kuhama; wengi wao ni sababu moja tuu..hakuna jambo la tofauti sana..: wote wanaunga mkono hoja

At the end wanarudi kwenye majimbo na kata zao zile zile.

Sasa unataka nione nini kipya kwa mtu mwingine kuhama?

Bahati mbaya mimi sio muumini wa siasa sana..! Kwa hiyo personal nachukulia pouwa tuu...labda kwako lipo tofauti mkuu [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom