Naomba kuchangia mjadala huu kidogo,kama mtanzania huru!
Kwanza,si dhambi wala ajabu mbunge au mwanachama mwingine yeyote kuhama chama chake,iwe kwa kushawishiwa au kwa hiari yake!
Watu tunaghadhibika juu ya gharama zinazotumika kurudia uchaguzi,ni sahihi kabisa kuumia kwa sababu pesa hizo zingeweza kutumika kwa mambo mengine ya muhimu zaidi kuliko uchaguzi,lakini hizo ndiyo gharama za demokrasia!(tumechagua mfumo huu,tusilalamike)
Watu wanasema hawa watu wamenunuliwa,inaweza kuwa kweli lakini wameshawishiwa,nao wakashawishika,na siasa ni pamoja na kuhakikisha unashambulia safu ya mpinzani wako kwa namna yoyote isiyovunja sheria za nchi!
Kama wabunge wa upinzani wakashawishika,(kwa sababu yoyote ile) iwe fedha,vyeo,au hiari yao tu,wananchi tunapaswa kumlaumu nani?? Je,tumlaumu anayehama au anayemshawishi kuhama? Kama ni gharama,ni nani hasa anayepeswa kulaumiwa kwa kutuingiza kwenye gharama hizo,ni mbunge anayeacha ubunge!au yule aliyemshawishi ahame?
Tukilitazama kwa jicho la ushabiki,hatutatenda haki kwenye jambo hili,inahitaji tafakuri ya kina kujua ni Nani haswa anapaswa kulaumiwa kwa hali tunayoipitia kama taifa,vinginevyo tutajikuta tunaharibu sanaaa!!!