Mbunge wa Masasi Mjini Geofrey Mwambe anusurika kifo akiwa na familia yake. Gari alilokuwa akisafiria lateketea kwa moto

Mbunge wa Masasi Mjini Geofrey Mwambe anusurika kifo akiwa na familia yake. Gari alilokuwa akisafiria lateketea kwa moto

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Mbunge wa jimbo la Masasi Mjini, Geofrey Mwambe na familia yake wamenusurika kifo baada ya gari binafsi waliyokuwa wakisafiria kushika moto na kuteketea kabisa leo Machi 27, 2022.

Mbunge huyo na familia yake walikuwa wakielekea Masasi kwenye msiba wa baba yake mzazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP Mtatiro Kitinkwi amesema, chanzo cha gari ya mbunge wa Masasi Mjini, Geofrey Mwambe kuteketea kwa moto Machi 27, 2022 ni hitilafu katika mfumo wa umeme wa Gari hilo.

Hata hivyo, ameeleza kuwa hakuna madhara kwa watu walikuwamo katika gari hilo.

FO4xGR3X0AApBfv.jpg
FO4xGwOXEAMWzxu.jpg
FO3EwTGWYAEQNGE.jpg
 
Mbunge wa Masasi Mjini, Geofrey Mwambe na familia yake wamenusurika kifo baada ya gari binafsi aina ya Lange Rover walilokuwa wakisafiria kushika moto na kuteketea kabisa leo Machi 27, 2022.

Mbunge huyo na familia yake walikuwa wakielekea Masasi kwenye msiba wa baba yake mzazi.

Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.
FB_IMG_1648394554428_1648394604550.jpg
 
Back
Top Bottom