Mbunge wa Masasi Mjini Geofrey Mwambe anusurika kifo akiwa na familia yake. Gari alilokuwa akisafiria lateketea kwa moto

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Mbunge wa jimbo la Masasi Mjini, Geofrey Mwambe na familia yake wamenusurika kifo baada ya gari binafsi waliyokuwa wakisafiria kushika moto na kuteketea kabisa leo Machi 27, 2022.

Mbunge huyo na familia yake walikuwa wakielekea Masasi kwenye msiba wa baba yake mzazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP Mtatiro Kitinkwi amesema, chanzo cha gari ya mbunge wa Masasi Mjini, Geofrey Mwambe kuteketea kwa moto Machi 27, 2022 ni hitilafu katika mfumo wa umeme wa Gari hilo.

Hata hivyo, ameeleza kuwa hakuna madhara kwa watu walikuwamo katika gari hilo.

 
Mbunge wa Masasi Mjini, Geofrey Mwambe na familia yake wamenusurika kifo baada ya gari binafsi aina ya Lange Rover walilokuwa wakisafiria kushika moto na kuteketea kabisa leo Machi 27, 2022.

Mbunge huyo na familia yake walikuwa wakielekea Masasi kwenye msiba wa baba yake mzazi.

Chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.
 
Sio mbaya sana.
Kikubwa wamepona na mbunge husika ni CCM (chama cha majambazi), sioni ubaya wa hiyo mali kuteketea.
Chuki yako kwa tajiri haitaongeza ugali mezani kwa wanao.....acha wivu fatuta pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…