Al-Watan
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 11,891
- 14,583
Jamii za masikini hazina cha kufanya baada ya balehe, hazina shule wala biashara, hazina namna ya kujiliwaza, zinawahi kulala kwa sababu hazina umeme, zikiwahi kulala zinakuwa pweke, zinawahi kuoa.Sio kinyume chake chief...
Jamii masikini zimejikita katika kutegemea uchumi wa kijima unaotaka watoto kama nguvukazi, hivyo kuoa mapema ni tija katika jitihada za kuongeza watoto watakaokuja kuwa watumwa wa wazazi wao kama nguvukazi rahisi.Hususan katika kilimo cha kijima.
Jamii tajiri zinasisitiza elimu.Watu wanasoma sana. Kusoma sana kunachelewesha kuoa/kuolewa.
Kuna jamii fulani ni masikini wa matajiri. Hawa ni masikini wa mjini. Lumpen ploretariat.
Hawana mashamba ya kulima wala hawawezi kumudu kuoa na kuzaa mapema.
Hawa ndio wanaochanganya sana watu kufikiri kwamba kuwahi kuoa ni alama ya kuwa na uwezo.
