Mkuu haya mambo mimi nimeyaona toka kitambo sana. Ni familia chache sana zenye elimu na kipato utakuta mtu amewahi kuoa au kuolewa, wengi ni masikini na wa kipato cha chini sana.
Mwaka flani ckassmate wangu alichaguliwa kusoma chuo kikuu baada ya kujiendeleza huko alikokua maana alienda ualim baada ya kumaliza sekondari. Sasa akafikia kwangu kwa muda, nilikua nimepanga mtaa mmoja kodi ya nyumba kwa mwezi ni sawa na mshahara wake wa miezi 2.
Yeye wakati huo ana watoto 3 na mke wake ana mimba ya mtoto wa 4. Akakaa kama miezi 4, huo mtaa ni wa watu wa kupato cha kati na kikubwa.
Siku moja akaniambia toka amekaa hapo amebahatika kuona watoto wachache sana wa shule za msingi na sekondari katika huo mtaa tofauti na mtaa mwingine ambapo alikua anaishi baba yake mdogo kuna shule za msingi 3, sekondari za serikali 4 na idadi ya watoto umri wa shule ni kubwa sana.
Akaniambia amejifunza kua watu wenye kipato na elimu hawana familia kubwa au hawana kabisa tofauti na watu masikini. Akasema amegundua kua na familia kubwa mapema kumemrudisha nyuma sana na angejua asingeoa mapema, akasema hatakuja kumshauri ndogo wake au mwanae awahi kuoa.
Nikashukuru kua huyo mtu amepata mwanga na inawezekana akawasaidia na wengine kuona mambo kw amtazamo huo.
Ni kweli kua umasikini unachangia sana watu kuwahi kuingia kwenye ndoa maana baada ya balehe hawana cha kufanya, kwa hiyo mtu kwenye late teens au early twenty ana mke na mtoto, ni wachache sana wanafika 30s bila kua na ndoa.