Mbunge wa Mikumi, Ndg.Joseph Haule aka Prof.J afunga ndoa takatifu

Mbunge wa Mikumi, Ndg.Joseph Haule aka Prof.J afunga ndoa takatifu

Huo
Kipindi ninavyowafahamu ni kile cha teenage wakati huo wako 15-16 ndiyo nyumbani mziki kwa sana na wewe ni retired unataka kupumzika.
Huo Ni uoga WA maisha, Kama ndo hivyo mababu Na mabibi wasingelea wajukuu zao. Ukweli kuwahi kuoa Ni fikra za watu mafukara, mwanaume mwenye akili hupaswi kuwa hivyo, unakimbilia nini kufuga ng'ombe wakati maziwa madukani yapo tele, au kuna wanaume wana tatizo la menopause so wanakimbizana Na muda. Mwanaume anapaswa kuzitafuta mtoto akija duniani avikute sio vimkute
 
Mkuu Sky Eclat, inavyoonekana Prof. Jay alishaoa miaka mingi sana. Ninahisi tunachochanganya hapa ni maana ya ndoa. Watu wengi tunaichukulia ndoa ni hadi kwenda kanisani.

Siku utakayotoka kwenu ukaenda kuanzisha maisha na mwenzako hiyo ni ndoa tayari. Prof. Jay kwa maelezo ya wadau humu alishaishi na huyu mwanamke miaka mingi. Walichofanya ni kubariki ndoa kanisani. Huwezi kuoa mtu uliyekuwa unalala naye kitanda kimoja miaka yote hiyo.

Mimi nilijua hakuwa anaishi na mtu kwahiyo ametafuta mchumba akaoa. Kwa alichokifanya ni sawa kabisa na alienda sawa na muda.
Kwa kifupi amekimbia zinaa na kupata baraka za kidini.
 
Kaoa akiwa mkubwa sana. Mimi kipindi nikiwa kidato cha kwanza yeye alikuwa kijana mkubwa kabisa. Nimekua nimeoa yeye ndo amekuja kuoa.

Hongera zake.
We vipi? Dk Many mwenyewe ameoa juzijuzi tu, na akikutana na Prof atamuuliza 'mbona umewahi dogo?'
 
Mkuu upo sahihi.

Nimefanikiwa kufanya kazi na watu weupe hapa bongo.

Wengi wao huoa wakiwa na 35+

Sasa hapa bongo ukifika 30 tu hujaoa ni tatizo
Bongo miaka 30 hujaoa ni tatizo, hasa uwe uswahilini miaka 30 hujaoa utasemwa mambo mengi hadi ujute.

Ni kweli wazungu wengi na watu waliosoma na kufanikiwa miaka ya kuoa huanzia 35+.

Unawahi kuoa ili iweje, watoto waje kukusaidia?

Kama hujajipanga na maisha yako, ndio unawafanya watoto kama non current assets, wakifika miaka 25 wana mzigo wa kumsadia baba ambae hakujipanga hivyo inawabidi waoe ili wakae na mzee nyumbani.
 
Duh! Umeandika maandishi mengi sana mkuu na mimi ni mvivu wa ku-Type.

Mimi nadhani nimemaliza. Sina sababu ya kuanza kujieleza kwa maandishi mengi.
kuwahi kuoa ni kuoa na mda gani?
Katika jamii masikini mtu akiamua kutooa/olewa ana matatizo.

Kumbe kuna wengine maisha yao wameamua kutafuta dawa ya kansa tu.
 
Kaoa akiwa mkubwa sana. Mimi kipindi nikiwa kidato cha kwanza yeye alikuwa kijana mkubwa kabisa. Nimekua nimeoa yeye ndo amekuja kuoa.

Hongera zake.

Mkuu ulikuwa unawashauri nini watu wengine wenye umri sawa na jamaa ambao hawajaoa?
 
Na ukiwahi then ukaharibu ni hiyo hiyo jamii itakayokushangaa pia. Kufanya mambo kwa kuimpress jamii unakuwa unaishi maisha yasiyo yako.
Ukifanya jambo kuwafurahisha watu utateseka sana maishani mwako.

Mimi ni last born kwetu, na mama yangu kanizaa kwenye very late 30s, almost anaelekea monopause.

Sasa mwaka juzi akaniuliza ntaoa lini, asije kufa hajaona mwanangu, nikamwambia kama ni kufa bila kuona mwanangu atakufa ila siwezi kuoa kisa yeye apate kuona mjukuu kabla hajafa maana kama ni wajukuu anao kibao.

Hakunijibu kitu, kisha baadae siku nyingine akaniambia nilimjibu vizuri ndoa ni yangu sio yake, yeye kashamaliza sehemu yake hivyo sio vizuri kufanya jambo kwa ajili ya watu wengine.

That is it. Usifanye jambo kuwafurahisha watu, huishi maisha ya watu wengine, unaishi maisha yako.
 
Tabu ni pale unaposema sijaoa halafu unaisha na Mtu kama mke na watoto mmezaa halafu siku za mbele unakuja kufunga ndoa takatifu! ni bora kuoa mapema kuliko kuishi hivyo.
 
Tabu ni pale unaposema sijaoa halafu unaisha na Mtu kama mke na watoto mmezaa halafu siku za mbele unakuja kufunga ndoa takatifu! ni bora kuoa mapema kuliko kuishi hivyo.
 
Mkuu haya mambo mimi nimeyaona toka kitambo sana. Ni familia chache sana zenye elimu na kipato utakuta mtu amewahi kuoa au kuolewa, wengi ni masikini na wa kipato cha chini sana.

Mwaka flani ckassmate wangu alichaguliwa kusoma chuo kikuu baada ya kujiendeleza huko alikokua maana alienda ualim baada ya kumaliza sekondari. Sasa akafikia kwangu kwa muda, nilikua nimepanga mtaa mmoja kodi ya nyumba kwa mwezi ni sawa na mshahara wake wa miezi 2.

Yeye wakati huo ana watoto 3 na mke wake ana mimba ya mtoto wa 4. Akakaa kama miezi 4, huo mtaa ni wa watu wa kupato cha kati na kikubwa.

Siku moja akaniambia toka amekaa hapo amebahatika kuona watoto wachache sana wa shule za msingi na sekondari katika huo mtaa tofauti na mtaa mwingine ambapo alikua anaishi baba yake mdogo kuna shule za msingi 3, sekondari za serikali 4 na idadi ya watoto umri wa shule ni kubwa sana.

Akaniambia amejifunza kua watu wenye kipato na elimu hawana familia kubwa au hawana kabisa tofauti na watu masikini. Akasema amegundua kua na familia kubwa mapema kumemrudisha nyuma sana na angejua asingeoa mapema, akasema hatakuja kumshauri ndogo wake au mwanae awahi kuoa.

Nikashukuru kua huyo mtu amepata mwanga na inawezekana akawasaidia na wengine kuona mambo kw amtazamo huo.

Ni kweli kua umasikini unachangia sana watu kuwahi kuingia kwenye ndoa maana baada ya balehe hawana cha kufanya, kwa hiyo mtu kwenye late teens au early twenty ana mke na mtoto, ni wachache sana wanafika 30s bila kua na ndoa.

Mbona mimi natoka jamii masikini na sasa hivi nina 30 ila bado sijaoa?
 
Kuwahi kuoa na kuolewa ni tabia ya jamii masikini.
Kuna vitu watu hukosea sana, na hii husababishwa na kurithi utamaduni, huku tukiendelea kuaminishwa lazima tuheshim tamaduni haijalishi uo utamaduni upoje.

Tuna shuhudia hata wenye elim kubwa tu, unakuta msichana anaelim yake kubwa lkn bado anajiona hana aman asipo olewa mapema. Na chazaidi anacho waza watu watamuonaje? wenzake wanaolewa yeye bado anachelewa na uoga wa umri kwenda.

Pamoja na kuwa na elim, lakini kukosa fursa ya kujichanganya na jamii tofauti, kukosa exposure na jamii tangu utotoni, kujifunza huru bado kunafanya vijana wasomi wengi kuishi ktk mfumo uleule unao fanana na ambao hawajasoma. Unashindwa kuona utofauti, cha zaidi labda utofauti utakuwa kwenye uchumi lkn kwenye social life hamna utofauti.

May be inachangiwa pia na kuzungukwa na Wajinga wengi kiasi kwamba unauzoea ujinga na kuwa sehem yao.

Lakini mimi naamini katika kuoa lzm uzingatie vifuatavyo

1. Kwanini unaoa? Je ni kwasababu watu wanaoa? Unataka tu upate watoto?

2. Upo tayari kuoa? (kukubali kubadilisha mfumo wa ubachela) upo tayari kukabiliana na changamoto za ndoa?

3. Unaweza mudu kuendesha familia? hali ya kiuchumi ipoje?

4. Umepata mtu sahihi? Umejihakikishia anakufaa? Umekubaliana na madhaifu yake na yako?

Kuishi kwa uoga ni hatari sana, yani utadhan una guarantee ya kuishi milelel hapa dunian.

Cha muhimu katika maisha ni kujitahidi kuitafuta furaha na aman, kuishi maisha unayoyataka.
 
Una miaka 35+ haujaoa au haukiwai kuoa wewe unamatatizo ya kimaumbile au kisaikologia. Acha kujidanganya ndugu @ nyoka wa makengeza eti maskini ndio wanao oa mapema. Umri sahihi wa kijana rijali aliyepata malezi bora na mwenye heshima na busara huoa kati 25 to 30 year regardless pato lake. Ukizungumzia matajiri basi watazame wanasoka wanaolipwa mabilioni ya pesa wanaoa at 22+ , sijawai msikia mchezaji baada ya kustafu soka ndio anaoa mean at 35+ . please 35+ tuwaachie wagane na divorced kuoa.
 
Kuna vitu watu hukosea sana, na hii husababishwa na kurithi utamaduni, huku tukiendelea kuaminishwa lazima tuheshim tamaduni haijalishi uo utamaduni upoje.

Tuna shuhudia hata wenye elim kubwa tu, unakuta msichana anaelim yake kubwa lkn bado anajiona hana aman asipo olewa mapema. Na chazaidi anacho waza watu watamuonaje? wenzake wanaolewa yeye bado anachelewa na uoga wa umri kwenda.

Pamoja na kuwa na elim, lakini kukosa fursa ya kujichanganya na jamii tofauti, kukosa exposure na jamii tangu utotoni, kujifunza huru bado kunafanya vijana wasomi wengi kuishi ktk mfumo uleule unao fanana na ambao hawajasoma. Unashindwa kuona utofauti, cha zaidi labda utofauti utakuwa kwenye uchumi lkn kwenye social life hamna utofauti.

May be inachangiwa pia na kuzungukwa na Wajinga wengi kiasi kwamba unauzoea ujinga na kuwa sehem yao.

Lakini mimi naamini katika kuoa lzm uzingatie vifuatavyo

1. Kwanini unaoa? Je ni kwasababu watu wanaoa? Unataka tu upate watoto?

2. Upo tayari kuoa? (kukubali kubadilisha mfumo wa ubachela) upo tayari kukabiliana na changamoto za ndoa?

3. Unaweza mudu kuendesha familia? hali ya kiuchumi ipoje?

4. Umepata mtu sahihi? Umejihakikishia anakufaa? Umekubaliana na madhaifu yake na yako?

Kuishi kwa uoga ni hatari sana, yani utadhan una guarantee ya kuishi milelel hapa dunian.

Cha muhimu katika maisha ni kujitahidi kuitafuta furaha na aman, kuishi maisha unayoyataka.

Mangi.

Hayo maswali yako ni ya mtu anayejua umuhimu wa critical thinking na individuality.

Kwetu unaweza kukuta mtu kamaliza chuo kikuu hajui umuhimu wa hayo.

Sehemu ya ku apply critical thinking na individuality ata apply herd mentality, borg like existence na formulaic lazyness.

Ndiyo maana mtu anamaliza Ph.D lakini ukimsikiliza unajiuliza, hivi huyu Ph.D kaioataje kwa mawazo haya mna mpangilio huu wa kujieleza?
 
Back
Top Bottom