Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ajiuzulu nafasi ya Mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ajiuzulu nafasi ya Mnadhimu wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni

Uliahidi ndani ya bunge kwamba kama Ben asipopatikana utahakikisha unawaunganisha wazee wa Rombo ili wahakikishe mtoto wao anapatikana , lakini muda ukapita bila muunganiko huo kufanyika .

Kwa bahati mbaya mambo yakakuharibikia zaidi ukaondolewa kwenye uenyekiti wa kanda ya Kaskazini kidemokrasia , umekasirika na kufura , sasa umeanza visa , tunakuomba kabla ya Usaliti mwingine hakikisha unatimiza ahadi yako
"MUNGU IBARIKI CHADEMA" 😎
 
Mimi naomba tu kumuuliza swali rafiki yangu, Erythro, ambaye ninamtambua kwamba ni CHADEMA damu damu,akiwakilisha chama hicho kwenye jukwaa hili la JF Siasa.

Mkuu Erythro, huyu Mbunge naye anatambulika huko chamani kama mpiganaji? Mpambanaji?

Naomba tu jibu rahisi rafiki yangu.

Kama mnao watu kama huyu, robo tu ndani ya chama, mnayo mategemeo yoyote ya kuiongoza nchi hii?
 
kiufupi huko chadema kuna fukuta sana,time will tell
Umehitimisha kwamba "kiufupi huko chadema kuna fukutasana..."; hapo hapo unakana hitimisho lako na kuanza kuutegemea wakati..."time will tell."

Sasa wewe ni lipi unalolisimamia! Matamanio yako ya CHADEMA kusambaratika hauwezi kuwa ndio ukweli utakavyokuwa. Hayo ni matamanio yako tu, kama wengi wanavyotamani CCM isambaratikie mbali. Hakuna ajuae kwa uhakika ni lipi litatokea.

Tunaomba tu wananchi wapewe fursa ya kuitumia haki yao ya kuamua hatma ya taifa lao kwa kura zao kutochezewa na mtu yeyote.

Hapo tutajua mbivu na mbichi, CHADEMA au CCM?
 
seriously mkuu chadema kuna mfumo?
achana tu na mfumo imara...

Unamteua mtu bila kumthibitisha mwaka mzima huo ni mfumo imara??

uteuzi wa wabunge viti maalum unafuataga mfumo gani?

kumteua Lowassa kuwa mgombea ulitumika mfump gani?

chadema ikija kuwa na mfumo namimi nachukua kadi.. kwa sasa bado ni NGO ya watu binafsi

Sent using Jamii Forums mobile app

Una hoja za hapa na pale, lakini hoja kuu hapa mnaikosa maana angekuwa mtu mwingine mngesema kwakuwa sio mchaga. Kwa bahati mbaya hayo yamemkuta mchanga, hivyo hoja yenu kuu inakosa nguvu so inabidi muokoteze sababu.
 
Naam, rangi halisi ya chadema tunaiona sasa, chuki yote dhidi ya Magufuli ilikuwa ni kuficha chuki waliokuwa nayo dhidi yao wao wenyewe, Warombo vs Machame + Marangu.
Swadaktaaa !...na ndiyo ule usemi " Toa kwanza boriti ndani ya jicho lako ndipo utaona kibanzi kwenye jicho la mwezio" unapoleta maana !
 
kwa hiyo hili ni suala la KIMSIMAMO. Ni bora kutokuwa na mnadhimu wa upinzani kuliko kuhalalisha shambulizi la kigaidi dhidi ya TL na ukatili aliotendewa baada ya hapo.
Nyie watu ni watu wa ajabu sana
Kanuni haisemi mnadhimu akipigwa risasi nafasi yake isizibww,kazi lazima zifanyike
 
Selasini kawavumilia sana! Nilisema uchaguzi uliopita umeipasua zaidi Chadema! Mnyika kawekwa mtegoni sababu ya kutafuta huruma kirahisi lakini hakuna kuaminiana wala uaminifu tena!

Sent using Jamii Forums mobile app

Huenda unachosema kikawa na ukweli, lakini Selasini kamvumilia nani sana? Amevumilia sana kutokutangazwa mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani! Ni kipi anashindwa kukitekeleza akiwa mbunge, lakini angeweza kukitekeleza vizuri akitangazwa mnadhimu mkuu wa upinzani? Je chaguzi nchi hii zinanajisiwa, na hao cdm wanafanyiwa uhuni wa wazi na dola kisa ni yeye hajatangazwa mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni? Kwa hiyo katika matatizo makubwa anayokutana nayo Selasini na kumbidi aivumilie sana cdm ni hiyo kutokutangazwa nafasi ya mnadhimu? Katika matatizo ambayo wananchi wa rombo yeye kama mbunge yanashindwa kutatuliwa, ni kwakuwa hajatangazwa rasmi kuwa mnadhimu? Hapa naona unachoma tu mahindi kwa tochi.

Haya mambo madogo madogo yanaletwa na wanaccm humu jukwaani, lengo hasa ni kuonyesha cdm ina matatizo makubwa na ndio itakuwa sababu ya kushindwa uchaguzi. Kwani ule ushenzi wa juzi wa kunajisi uchaguzi wa SM za mitaa ni kwa sababu cdm kuna kutokuelewana kunakosemwa? Huo uchaguzi mkuu wa 2020 nao utanajisiwa ili ccm wajitangaze washindi, kisa Selasini amekataliwa kutangazwa mnadhimu huko bungeni?
 
Kimchezo mchezo hiki chama nacho kinaenda kuwa vile vyama vyenye mwenyekiti tu. Mungu tuepushe na hili janga

Cdm kitafikia huko kisa Selasini hajatangazwa mnadhimu wa kambi ya upinzani?
 
Uliahidi ndani ya bunge kwamba kama Ben asipopatikana utahakikisha unawaunganisha wazee wa Rombo ili wahakikishe mtoto wao anapatikana , lakini muda ukapita bila muunganiko huo kufanyika .

Kwa bahati mbaya mambo yakakuharibikia zaidi ukaondolewa kwenye uenyekiti wa kanda ya Kaskazini kidemokrasia , umekasirika na kufura , sasa umeanza visa , tunakuomba kabla ya Usaliti mwingine hakikisha unatimiza ahadi yako
Team Mbowe kazini!
Kujiuzulu tu uandhimu mnapeleka mashambulizi?
Ila huyu 30 na Mbowe wanajua alipo saa nane
Kwenye uchaguzi wa 2015,saa 8 akielekea Rombo kwenye kura za maoni,alitengenezewa ajali alipifika kibaha maili moja,aliokua nao walikufa saa nane alipeta,alipofika Rombo akaambiwa sorry you are late brother!
 
Selasini amemwandikia barua Mbowe leo Januari 13 2020 na kuwapa Nakala ya barua hiyo Spika wa Bunge Job Yustimo Ndugai na Katibu wa Bunge Steven Kagaigai.

Selasini ameweka wazi sababu za kujiuzulu nafasi hiyo kuwa kukaimishwa kwa muda mrefu bila kuthibitishwa Japo hajawahi kuonywa kwa namna yoyote ille kuashiria kushindwa kuimudu nafasi hiyo.

Hili ni tukio lingine linalothibitisha madhara ya mwendelezo wa ubabe wa Mnowe ndani ya CHADEMA.

Mods unganisheni huu uzi na ule mwingine, kule kuna majibu stahiki ya hizi mbwembwe.
 
Nyie watu ni watu wa ajabu sana
Kanuni haisemi mnadhimu akipigwa risasi nafasi yake isizibww,kazi lazima zifanyike

..hebu tueleze kanuni zinasemaje mbunge akishambuliwa ktk eneo linalolindwa na serikali.
 
Sasa uhalisia wa wanaojiita Wachaga unaanza kujitokeza, Wamarangu na Warombo ni Mbwa na Paka na hawawezi kukaa sehemu moja hata siku moja, chadema ni ya Wamarangu + Machame, hivyo ni Mrombo hawezi kubali kuongozwa na Mmarangu, na kinyume chake.

Ni chuki ya ajabu!

Hapa naona unachomeka uchaga ili kutakatisha tuhuma ya usukuma iliyo wazi. Rudi shule ukajifunze propaganda dogo.
 
Back
Top Bottom