Mbunge wa Ujerumani ataka kufukuzwa nchini humo jeshi la US

Mbunge wa Ujerumani ataka kufukuzwa nchini humo jeshi la US

HERY HERNHO

Senior Member
Joined
Mar 4, 2022
Posts
110
Reaction score
458
Mbunge mmoja wa Ujerumani ametoa mito wa kufukuzwa nchini humo vikosi vya jeshi la Marekani ambavyo vimekuwepo nchini humo kwa karibu miongo minane.
4bvfd17bf1773b1rer7_800C450.jpg

Sevim Dagdelen wa chama cha mrengo wa Kushoto katika Bunge la Ujerumani (Bundestag) amesema kuna haja kwa serikali ya Berlin kuangalia upya uhusiano wake wa kigeni na Marekani. Amesema sera za nje za Washington zimegubikwa na ukanyagaji wa sheria za kimataifa.

Mtunga sheria huyo wa Bunge la Federali la Ujerumani ameeleza bayana kuwa, "Baada ya miaka 78, wakati umefika sasa kwa wanajeshi wa Marekani kwenda nyumbani."

Sevim Dagdelen amesema Marekani inatumia kambi zake za kijeshi zilizoko katika nchi hiyo mwanachama wa Umoja wa Ulaya kuanzisha vita ughaibuni, na pia kuendeshea operesheni zake 'hatarishi' za ndege zisizo na rubani (droni).

Kadhali Mbunge huyo amekosoa mikutano inayofanyika mara kwa mara ya Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Marekani wa Ramstein huko nchini Ujerumani. Amesema mijadala yote kuhusu kuizatiti kwa silaha Ukraine inafanyika kwenye kambi hiyo.

Haya yanajiri siku chache baada ya Boris Pistorius, Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani kutahadharisha kuwa, jeshi la nchi hiyo halina uwezo wa kuilinda nchi iwapo kutatokea vita dhidi ya taifa hilo.

Alisisitiza kuwa, iwapo vita vitatokea dhidi ya Ujerumani, jeshi la taifa hilo litashindwa kuipigania nchi kutokana na udhaifu wa zana za kijeshi na ukosefu mkubwa wa vikosi vya ulinzi.
 
Napata picha US wana power kiasi gani dunia hii., Marekani amewekeza vibaya sana tena muda mrefu sana mpaka Ujerumani kudumba watalazimika msaada wa US kikamilifu endapo watalazimika kuingia vitani
 
Kwenye nchi yenye uhuru wa Mawazo hilo siyo jambo la kushangaa! West ni tofauti kabisa na Russia ambapo mtu akipinga kauli/mawazo ya Puttin anachinjwa au rupango maisha. Na ndiyo maana ya bunge la vyama vyenye maono tofauti
 
Warusi wa Buza wanashangaa sana haya mambo

Juz msemaji wa ikulu ya Marekan akisema Marekan haitauruhusu Ukraine ikubaliane na mpango wa aman wa China, kuna mwanaharaki mmoja wa kupinga vita alinyanyuka akauliza kama nyinyi hamkubaliani na mpango wa amani wa china nchin Ukraine, uo mpango wenu huko wapi?
.kilichofuata alinyanyuliwa mzobe mzobe na askari na kutolewa nje kabisa
 
Kwenye nchi yenye uhuru wa Mawazo hilo siyo jambo la kushangaa! West ni tofauti kabisa na Russia ambapo mtu akipinga kauli/mawazo ya Puttin anachinjwa au rupango maisha. Na ndiyo maana ya bunge la vyama vyenye maono tofauti
Kama haitoshi kuna mwandishi wa habar wa kichina alikuwa ukumbini na msemaji wa umoja wa maraifa, msemaji wa umoja wa mataifa alikuwa anatoa matamko ya kulaani kitendo cha urusi cha kuvunja sheria za kimataifa kwa kuingiza jeshi lake katika mipaka ya Ukraine! Mwandishi wa habari alimuulisa yule msemaji!

Ni sawa marekani kuingiza wanajeshi wake nchini Syria ila si sawa kwa Urusi kufanya hivo kwa Ukraine?

Msemaji alijibu anazungumzia issue ya Urusi na Ukraine!

Mwandishi alienda mbali na kumkumbusha kuwa anazungumzia sheria za kimataifa za Ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi, maana Marekani hakuitwa wala kupewa mwaliko na serikali ya Syria ila mpaka sasa ana bikosi vya kijeshi nchini Syria!

Msemaji alijibu ye hajui kama Marekani ana vikosi vya kijeshi nchini Syria!

Umoja wa kimataifa ulitoa picha gani hapa kwa ulimwengu?
 
Hii habari ni uwongo na ina mrengo fulani ya kuonyesha kwamba Russia wana ushawishi, Germany sio Tanzania ndege za kivita za Euro fighter jet ni mkono wa mjerumani

Vifaru chapa leopard 2 vinavyo ogopeka duniani, na aina nyingine nyingi za silaha zinatengenezwa Germany so unapoamua kuleta habari basi punguza mahaba

Hatukatai kwamba Germany hawawezi kushindwa vita endapo itatokea vita leo, Germany huko nyuma tayari walishashindwa vita mara kibao tu mbona

Kama jeshi la Ukraine limeweza kulinda Kyiv up to now mbele ya super power Russia, wachambuzi mnatakiwa mbadilike, vita siyo mahaba na ushindi katika vita haupatikani kwa ukubwa wa nch, ukubwa wa jeshi nk
 
Ningekuwa mimi huyo msemaji ningeuliza ukiwa mwizi ukakamatwa na polisi ukapelekwa mahakamani unaweza kujitetea mbele ya hakimu mbona Juma ni jambazi lakini hakamatwi wala kufikishwa mahakamani kwa sababu anawahonga polisi halafu utetezi wako ukawa na mashiko mbele ya hakimu.
Kama haitoshi kuna mwandishi wa habar wa kichina alikuwa ukumbini na msemaji wa umoja wa maraifa, msemaji wa umoja wa mataifa alikuwa anatoa matamko ya kulaani kitendo cha urusi cha kuvunja sheria za kimataifa kwa kuingiza jeshi lake katika mipaka ya Ukraine! Mwandishi wa habari alimuulisa yule msemaji!

Ni sawa marekani kuingiza wanajeshi wake nchini Syria ila si sawa kwa Urusi kufanya hivo kwa Ukraine?

Msemaji alijibu anazungumzia issue ya Urusi na Ukraine!

Mwandishi alienda mbali na kumkumbusha kuwa anazungumzia sheria za kimataifa za Ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi, maana Marekani hakuitwa wala kupewa mwaliko na serikali ya Syria ila mpaka sasa ana bikosi vya kijeshi nchini Syria!

Msemaji alijibu ye hajui kama Marekani ana vikosi vya kijeshi nchini Syria!

Umoja wa kimataifa ulitoa picha gani hapa kwa ulimwengu?
 
Hii habari ni uwongo na ina mrengo fulani ya kuonyesha kwamba Russia wana ushawishi, Germany sio Tanzania ndege za kivita za Euro fighter jet ni mkono wa mjerumani...
Umekaa nyumbani unaangalia udaku tu utajuaje mambo mazito kama haya? Fuatilia bundestag kama hakuongea huyo bungeni uje hapa uweke namba yako nikutumie laki tano cash chap chap ..kama kaongea jipige kifuani sema hakika mimi kubwa jinga la udaku
 
Back
Top Bottom