HERY HERNHO
Senior Member
- Mar 4, 2022
- 110
- 458
Mbunge mmoja wa Ujerumani ametoa mito wa kufukuzwa nchini humo vikosi vya jeshi la Marekani ambavyo vimekuwepo nchini humo kwa karibu miongo minane.
Sevim Dagdelen wa chama cha mrengo wa Kushoto katika Bunge la Ujerumani (Bundestag) amesema kuna haja kwa serikali ya Berlin kuangalia upya uhusiano wake wa kigeni na Marekani. Amesema sera za nje za Washington zimegubikwa na ukanyagaji wa sheria za kimataifa.
Mtunga sheria huyo wa Bunge la Federali la Ujerumani ameeleza bayana kuwa, "Baada ya miaka 78, wakati umefika sasa kwa wanajeshi wa Marekani kwenda nyumbani."
Sevim Dagdelen amesema Marekani inatumia kambi zake za kijeshi zilizoko katika nchi hiyo mwanachama wa Umoja wa Ulaya kuanzisha vita ughaibuni, na pia kuendeshea operesheni zake 'hatarishi' za ndege zisizo na rubani (droni).
Kadhali Mbunge huyo amekosoa mikutano inayofanyika mara kwa mara ya Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Marekani wa Ramstein huko nchini Ujerumani. Amesema mijadala yote kuhusu kuizatiti kwa silaha Ukraine inafanyika kwenye kambi hiyo.
Haya yanajiri siku chache baada ya Boris Pistorius, Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani kutahadharisha kuwa, jeshi la nchi hiyo halina uwezo wa kuilinda nchi iwapo kutatokea vita dhidi ya taifa hilo.
Alisisitiza kuwa, iwapo vita vitatokea dhidi ya Ujerumani, jeshi la taifa hilo litashindwa kuipigania nchi kutokana na udhaifu wa zana za kijeshi na ukosefu mkubwa wa vikosi vya ulinzi.