Pre GE2025 Mbunge wa Ushetu apiga magoti kuomba maji ya ziwa Victoria. Waziri amjibu "Samia ametoa pesa mkandarasi anakuja"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani Mkoani Shinyanga amemuangukia Waziri wa Maji Jumaa Aweso akimuomba maji kwani Amesema Wilaya Majimbo yaote ya Mkoa wa Shinyanga yamefikiwa na Mji ya kutoka Ziwa Victoria isipokuwa Jimbo lake.

Akiongea Kwa unyenyekevu, uchungu na masikitiko bwana Cherehani amesema kati ya Kata 15 za Jimbo lake Kata 11 hazina maji hivyo kuwa Changamoto kubwa Kwa Wananchi wake.

Akijibu Maombi hayo Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema tayari Rais Samia amesikia Kilio Cha Wana Ushetu na Serikali Imetoa maelekezo ya kutangazwa tenda haraka ambapo ndani siku 30 mkandarasi atakuwa site kuanza usambazaji wa Maji Kwa Wananchi maji ya uhakika kutoka Ziwa Victoria.

My Take: Kuelekea Uchaguzi tutaona Mengi, wale wote waliopitishwa na Jiwe kama hawakuwa na sifa ndio imekula kwao.
Kwa hiyo mkandarasi asiipokuja na maji kukosekana alaumiwe mama Samia?
 
CCM kwa maigizo, hawajambo? Yaani kama ningekuwepo kwenye huo mkutano ningempa maswali magumu sana huyo mbunge mpk angejiuzulu.
 
Haya mambo ya maji yalipaswa kuwa mwisho miaka ya 95 huko karne ya 21 tunajadili kuzindua mradi wa maji??? Maana yake hadi 2040 tutakuwa bado hatujamaliz haya matatizo,,,
Samia atayamaliza kabla ya 2030
 
Samia atayamaliza kabla ya 2030
Huyuhuyu au tumsubilie mwingine?? Yaani makamba amevuruga pale tones tanesco badala alale nae mbele anamchekea tu!!!tuwe wakweli hakuna mahali ccm itatupeleka labda huyo mama tumvue gamba qhamie nccr mageuzi
 
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani Mkoani Shinyanga amemuangukia Waziri wa Maji Jumaa Aweso akimuomba maji kwani Amesema Wilaya Majimbo yaote ya Mkoa wa Shinyanga yamefikiwa na Mji ya kutoka Ziwa Victoria isipokuwa Jimbo lake.

Akiongea Kwa unyenyekevu, uchungu na masikitiko bwana Cherehani amesema kati ya Kata 15 za Jimbo lake Kata 11 hazina maji hivyo kuwa Changamoto kubwa Kwa Wananchi wake.

Akijibu Maombi hayo Waziri wa Maji Jumaa Aweso amesema tayari Rais Samia amesikia Kilio Cha Wana Ushetu na Serikali Imetoa maelekezo ya kutangazwa tenda haraka ambapo ndani siku 30 mkandarasi atakuwa site kuanza usambazaji wa Maji Kwa Wananchi maji ya uhakika kutoka Ziwa Victoria.

My Take: Kuelekea Uchaguzi tutaona Mengi, wale wote waliopitishwa na Jiwe kama hawakuwa na sifa ndio imekula kwao.

View: https://www.instagram.com/p/C16S-qIrvkt/?igsh=MXJzdXVjOGE5ZGEwbQ==

View: https://twitter.com/Mastermark45/status/1746839996823121983?t=fUm6aLkac7ZHth28VY9mWg&s=19
 
Kwamba asingepiga magoti angepata jibu tofauti
 
Back
Top Bottom