Mbunge wa Viti Maalum (CUF), Riziki Lulida aomba kurejea CCM. Asema Rais Magufuli ni msikivu alifuturu naye na kuongea naye kama ndugu

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,509
Reaction score
3,756
Twitter(21).png

Amesema amerudi CCM kwasababu nyingi na ya kwanza ni kuwa Rais Magufuli ni msikivu na atakaposikiliza hoja yake atakuwa msikivu.

Amesema “Mwaka 2015, Rais alinikuta nje akaniuliza nafanya nini. Nilijibu nataka kwenda nyumbani kufuturu. Akaniambia mimi ndio baba watoto twende, nami nikamuambia twende”

Ameongeza kuwa Rais alimchukua hadi nyumbani kwake akafuturu naye huku akiongea naye kama ndugu yake kabisa hivyo kukaa upande wa pili anadhalilika sana ila haikuwa kusudi yake kwani ni maovu aliyotendewa, alishinda na kukatwa bila sababu ya msingi.

Amesema “Leo natangaza rasmi kama utaridhia (Spika Ndugai) mimi leo narudi nyumbani kumenoga. Nimelelewa na CCM ila kwa yaliyojitokeza naomba mnisamehe, kama niliwakwaza na wale walionifanyia maovu hadi nimefikia hapa naomba Mwenyezi Mungu niwasamehe”

Aidha, Spika Ndugai asema kuwa maisha ni mapito ndio maana kuna rafiki zake kama akina Ahonga huwa anawaambia wawe na kiasi kwani siasa ni shule kubwa na katika Vyuo Vikuu ni Bunge. Watu wataenda kulia, kushoto na kati.
 
Mwenda kwao si mtumwa,karibu nyumbani kumenoga tunajua watakutana lakini wasamehe bure!
 
Sishangai kurudi CCM ikiwa alikuchukuwa kufuturu. Kama ulifunga ulitakiwa ufutAri, lakini wewe ilifutUru na yeye.

La pili uwache uwongo wewe, mwaka 2015 ramadhani ilikuwa August kabla ya uchaguzi mkuu.
 
Hahahahahaaaa!
Hivi haiwezekani kuhama Chama kimya kimya?
Manake sababu nyingine hata Mwanangu wa Darasa la 4 hawezi kuzisema mbele za watu.
 
Nani kwa nini sasa? Kwa nini asihame hio 2015 alipo futurishwa matokeo yake amesubiria term ya ubunge iishe ndo ajiengu

semper fidelis
 
Hawa wabunge wa viti maalum wanakula pesa za bure tu, wapo wapo hawajielewi, wanatuchezea akili kutafuna pesa za walipa kodi bila kuzitolea jasho.
 
Kwa hiyo wale wanaokatakata mapanga
Ni wasikivu pia?
Make wakija kukata ugali mnakula nao.

Sababu nyingine Ni utopolo kabisa
 
Wengi wanakimbilia ccm kwasababu ya teuzi na madaraka, Sasa najiuliza wataenea wote au ndio badae watatudi kwenye majuto tu. Tusubiri muda ndio msema kweli
 
Amesema amerudi CCM kwasababu nyingi na ya kwanza ni kuwa Rais Magufuli ni msikivu na atakaposikiliza hoja yake atakuwa msikivu.

Amesema “Mwaka 2015, Rais alinikuta nje akaniuliza nafanya nini. Nilijibu nataka kwenda nyumbani kufuru. Akaniambia mimi ndio baba watoto twende, nami nikamuambia twende”

Ameongeza kuwa Rais alimchukua hadi nyumbani kwake akafuturu naye huku akiongea naye kama ndugu yake kabisa hivyo kukaa upande wa pili anadhalilika sana ila haikuwa kusudi yake kwani ni maovu aliyotendewa, alishinda na kukatwa bila sababu ya msingi.

Amesema “Leo natangaza rasmi kama utaridhia (Spika Ndugai) mimi leo narudi nyumbani kumenoga. Nimelelewa na CCM ila kwa yaliyojitokeza naomba mnisamehe, kama niliwakwaza na wale walionifanyia maovu hadi nimefikia hapa naomba Mwenyezi Mungu niwasamehe”

Aidha, Spika Ndugai asema kuwa maisha ni mapito ndio maana kuna rafiki zake kama akina Ahonga huwa anawaambia wawe na kiasi kwani siasa ni shule kubwa na katika Vyuo Vikuu ni Bunge. Watu wataenda kulia, kushoto na kati.
Itakuwa alipata ndonga huyu mama.
Siyo futari tu
 
Back
Top Bottom