Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
Amesema amerudi CCM kwasababu nyingi na ya kwanza ni kuwa Rais Magufuli ni msikivu na atakaposikiliza hoja yake atakuwa msikivu.
Amesema “Mwaka 2015, Rais alinikuta nje akaniuliza nafanya nini. Nilijibu nataka kwenda nyumbani kufuturu. Akaniambia mimi ndio baba watoto twende, nami nikamuambia twende”
Ameongeza kuwa Rais alimchukua hadi nyumbani kwake akafuturu naye huku akiongea naye kama ndugu yake kabisa hivyo kukaa upande wa pili anadhalilika sana ila haikuwa kusudi yake kwani ni maovu aliyotendewa, alishinda na kukatwa bila sababu ya msingi.
Amesema “Leo natangaza rasmi kama utaridhia (Spika Ndugai) mimi leo narudi nyumbani kumenoga. Nimelelewa na CCM ila kwa yaliyojitokeza naomba mnisamehe, kama niliwakwaza na wale walionifanyia maovu hadi nimefikia hapa naomba Mwenyezi Mungu niwasamehe”
Aidha, Spika Ndugai asema kuwa maisha ni mapito ndio maana kuna rafiki zake kama akina Ahonga huwa anawaambia wawe na kiasi kwani siasa ni shule kubwa na katika Vyuo Vikuu ni Bunge. Watu wataenda kulia, kushoto na kati.