TANZIA Mbunge wa zamani, Nimrod Mkono amefariki dunia nchini Marekani

TANZIA Mbunge wa zamani, Nimrod Mkono amefariki dunia nchini Marekani

Atakumbukwa kwa aina ya kofia yake hiyo!
EfrwV1eXgAY-3R7.jpg
 
Umeacha alama kwa maisha yako kwa kujenga shule nyingi Mkoani Mara na sasa watoto wengi wa masikini wanazitumia walau kumezea definition ya photosynthesis.

Pia kuna chuo kikuu cha kilimo pale Butuguri nadhan ulichangia kusukuma kijengwe!

Ila hadi sasa wapo popo tu wanalala.


R.I.P Mzee, sote njia mojaa
 
Aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini na Butiama na pia Wakili maarufu Nchini Nimrod Mkono amefariki asubuhi ya leo kwa saa za Marekani.

Akiongea na @ayotv_ kwa njia ya simu Mdogo wa Marehemu, Zadock Mkono amethibitisha kutokea kifo cha Kaka yake.

“Nimepewa taarifa na Shemeji (Mke wa Wakili Mkono) kwamba Mzee amefariki nimempigia Shemeji alikuwa analia tu ameshindwa kuongea vizuri, Mzee aliondoka Tanzania tangu mwaka 2018 akaelekea Marekani kwa matibabu kwasababu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la kusahausahau, kumbukumbu zilikuwa zinapotea”

“Mimi nipo Tanzania kwa sasa ninachoweza kuthibitisha ni kwamba kweli amefariki taarifa zaidi za kama alikuwa anaugua ugonjwa mwingine na kama alikuwa Hospitali au amefariki ghafla hizo bado sijajua, nitawapa taarifa zaidi baadaye”

View attachment 2592241

Hivi masumbuko Lamwai yupo wapi?
 
Back
Top Bottom