TANZIA Mbunge wa zamani, Nimrod Mkono amefariki dunia nchini Marekani

TANZIA Mbunge wa zamani, Nimrod Mkono amefariki dunia nchini Marekani

Tena anavuta kitu brand new syo reconditioned

Ova
Huyu mtu achana naye, amejenga masecondary Butiama kwa pesa zake binafsi akazipa majina ya machifu wa kizanaki na kuzikabidhi shule zote serikalini ni Mali ya serikali, Hakuna hata shule moja amejipa jina lake, siyo Utapeli kama wa kina Gertrude Lwakatare na Saint Marys zake kumbe zilitakiwa kusomesha yatima bure.

Leo kuna majitu yanapenda tu vitu vya umma kupachika majina yao kiholela tu.
 
Busegwe ndio yalikuwa makao makuu ya Wasabato Tanzania ndio kijijini kwa Nimrod Mkono, palikuwa na airstrip hapo Busegwe na Nimrod Mkono alikuwa na jeuri ya kupark ndege yake binafsi hapo.
"Ndege Ndogo ya Nimrod Mkono ndiyo inawasili muda si mrefu kutokea jijini Dar es Es salaam"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini na Butiama na pia Wakili maarufu Nchini Nimrod Mkono amefariki asubuhi ya leo kwa saa za Marekani.

Akiongea na @ayotv_ kwa njia ya simu Mdogo wa Marehemu, Zadock Mkono amethibitisha kutokea kifo cha Kaka yake.

“Nimepewa taarifa na Shemeji (Mke wa Wakili Mkono) kwamba Mzee amefariki nimempigia Shemeji alikuwa analia tu ameshindwa kuongea vizuri, Mzee aliondoka Tanzania tangu mwaka 2018 akaelekea Marekani kwa matibabu kwasababu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la kusahausahau, kumbukumbu zilikuwa zinapotea”

“Mimi nipo Tanzania kwa sasa ninachoweza kuthibitisha ni kwamba kweli amefariki taarifa zaidi za kama alikuwa anaugua ugonjwa mwingine na kama alikuwa Hospitali au amefariki ghafla hizo bado sijajua, nitawapa taarifa zaidi baadaye”

View attachment 2592241
Wazuri hawafi, alipata kusema mlamba asali mmoja. RIP Mzee Mkono.
 
Huyu mtu achana naye, amejenga masecondary Butiama kwa pesa zake binafsi akazipa majina ya machifu wa kizanaki na kuzikabidhi shule zote serikalini ni Mali ya serikali, Hakuna hata shule moja amejipa jina lake, siyo Utapeli kama wa kina Gertrude Lwakatare na Saint Marys zake kumbe zilitakiwa kusomesha yatima bure.

Leo kuna majitu yanapenda tu vitu vya umma kupachika majina yao kiholela tu.
kweli hapa Nimrod Amenishangaza shule hata moja haina jina lake kama mafisadi na wanasiasa makanjanja wapendavyo kuandika majina yao katika taasisi. kwa Advocate Mkono ni tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ilikuwaje mkuu back ground? hivi ni kweli Mbowe alinusuriwa na Nimrod Mkono?

Sent using Jamii Forums mobile app
Zito na Mbowe walishutumiwa kuhusika kwenye kifo cha Wangwe, ndipo Mzee mkono akatoa gari lake likiwa na bendera ya bunge ili kuwatorosha eneo la tukio na kuwapeleka Mwanza.
Baada ya mzee kufanya uungwana huo, basi ccm napo wakaanza kumshutumu kwamba anaifadhili chadema kwa kuipa pesa.
 
Kitu cha kusikitisha sana Nimrod Mkono alikuwa anakaa Nyumbani kwa Baba yake kwa kuogopa kufanya maendeleo Busegwe kumhofia Nyerere.

Ni mpaka Nyerere alipokufa ndio Nimrod Mkono akahama Nyumbani kwa baba yake na Kujenga nyumba ya hadhi yake.

Chifu wa Wazanaki Butiama hakuwa na usafiri ni Nimrod Mkono ndio alimpa pick up Ford Ranger brand new kilometre zero na hapo Chifu ndio heshima ikarudi hasa kwa wadoea lift za kwenda Musoma mjini kutokea Butiama.

Ikumbukwe Nimrod Mkono alikimbia nchi mpaka akaombea kwa Nyerere ndio akakubaliwa kurudi Tanzania.
 
Back
Top Bottom