Mzee Kigogo
JF-Expert Member
- Jun 3, 2018
- 9,968
- 16,680
He was dead
He died
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
He was dead
Mbona Chuki / Usununu hivi? Alikudhulumu chochote kile labda ili Wanawe ( hasa Uncle's ) wake tukurejeshee?Akakutane sasa na mfumo wa haki. I hope amebeba pesa za kutosha kuhonga huko aendako maana huko utasomewa kila shitaka hadi la kulamba sukari utotoni kisha ukasema "sio mimi".
Wanadamu huwa tunaviburi sana ila tunasahau kuwa maisha and the days tunaishi hapa huwa hatuna uwezo wa kurenew uzee ukishatufika.
Kwa lugha nyingine inaitwa kifutio.Vanga inasahaulisha eh?[emoji38]
Masahihisho kidogo siyo zote zina Majina ya Machifu kwa mfano ile ya Oswald Mang'ombe ( Baba yake Mkubwa mwana JamiiForums mkubwa, machachari na maarufu mno hapa ) hakuwa Mtemi ila alikuwa ni Mtoto wa Mtemi wa Watuguri Mang'ombe ( Omary ) Isyesya.Huyu mtu achana naye, amejenga masecondary Butiama kwa pesa zake binafsi akazipa majina ya machifu wa kizanaki na kuzikabidhi shule zote serikalini ni Mali ya serikali, Hakuna hata shule moja amejipa jina lake, siyo Utapeli kama wa kina Gertrude Lwakatare na Saint Marys zake kumbe zilitakiwa kusomesha yatima bure.
Leo kuna majitu yanapenda tu vitu vya umma kupachika majina yao kiholela tu.
Huyu Hendrew Chenge ndiyo nani? Watanzania wengi tunayemju ni Andrew Chenge pekee.ndio ataenda kuuleta mwili wa Marehem Marekani akishirikiana na Hendrew Chenge
Sent using Jamii Forums mobile app
Baba yake mkubwa aliyepewa Pole ya huu Msiba na Bujibuji Simba Nyamaume katika Uzi huuOswald Mang'ombe.
Apumzike kwa amani.
Bange / Bangi unayovuta haipo duniani.Hivi masumbuko Lamwai yupo wapi?
Kama Cha mzee smallAlikua anapenda kuvaa kikofia chekundu kina kishungi cheus kinaning'inia
Apumzike kwa amani mwendo ameumaliza
Mkono alizaliwa Agosti 18, 1943 katika Kijiji cha Busegwe, Kata ya Busegwe, Wilaya ya Butiama mkoani Mara.
Mkono ni miongoni mwa matajiri wachache nchini waliojitoa kwa hali na mali kusaidia maendeleo ya kijamii.
Katika Jimbo la Musoma Vijijini na baadaye Butiama, Mkono amejenga shule za msingi na sekondari nyingi. Baadhi ya shule hizo ni Chifu Ihunyo, Chifu Wazangi, Oswald Mang’ombe, Shule ya Sekondari Butuguri na Shule ya Sekondari Kasoma.
Shule zote hizi zimegharimu mabilioni ya shilingi. Shule mbili – Oswald Mang’ombe na Busegwe aliikabidhi serikali. Chifu Wanzagi inaendeshwa na madhehebu ya dini.
Jimbo la Musoma Vijijini lililokuwa na kata 36 na vijiji 119, hakuna sehemu ambayo haikupata kufikiwa na Mkono kimaendeleo.
Pamoja na shule, Mkono amechimba visima vingi katika vijiji vingi. Amejenga vyumba vya madarasa na maabara, amefungua barabara zote za enzi ya utawala wa wakoloni na mpya, amejenga mabweni katika shule nyingi kuanzia Busekela (magharibi) hadi Kyagata na Sirori Simba (mashariki). Amejenga zahanati, vituo vya afya, wodi, vituo vya polisi na majengo ya utawala sehemu nyingi.
Pia amejenga na kukarabati mabwawa na ameshirikiana na serikali kufanikisha kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Mwalimu Nyerere. Majengo ya Sekondari ya Oswald Mang’ombe yamekubaliwa yatumike kuanzisha chuo hicho.
Mmbunge wa Rombo enzi hizo,kilikua kichwa sana,Lawyer naye,udingo unakula vichwa,mwanamke mzuri kama Whitney Houstoni nae kafa,udongo unakula vinono.Aliishafariki kipindi kile cha Covid 19
Umesoma kwa makini comments za pacha wa Gentamycine?Rest well Mzee Mkono
Pole kwa familia na wote walioguswa na msiba huu
Umesoma kwa makini comments za pacha wa Gentamycine?
Sasa rudi kwenye thread ya Le Mutuz na Neema Ngwilulupi hivi ndivyo alivyotaka kumalizwa Baharia akastukia mchezo mapema.
Hivi tajiri kama Mkono ni wa kwenda kutunzwa nyumba za wazee?
Aisee wanawake mnaupiga mwingi mpaka unamwagika aisee, nimeogopa sana.
R.i.p taikon wewe ni jabali la siasa za bongo....Aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini na Butiama na pia Wakili maarufu Nchini Nimrod Mkono amefariki asubuhi ya leo kwa saa za Marekani.
Akiongea na @ayotv_ kwa njia ya simu Mdogo wa Marehemu, Zadock Mkono amethibitisha kutokea kifo cha Kaka yake.
“Nimepewa taarifa na Shemeji (Mke wa Wakili Mkono) kwamba Mzee amefariki nimempigia Shemeji alikuwa analia tu ameshindwa kuongea vizuri, Mzee aliondoka Tanzania tangu mwaka 2018 akaelekea Marekani kwa matibabu kwasababu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la kusahausahau, kumbukumbu zilikuwa zinapotea”
“Mimi nipo Tanzania kwa sasa ninachoweza kuthibitisha ni kwamba kweli amefariki taarifa zaidi za kama alikuwa anaugua ugonjwa mwingine na kama alikuwa Hospitali au amefariki ghafla hizo bado sijajua, nitawapa taarifa zaidi baadaye”
View attachment 2592241
Yule shetani alikuwa na uwezo wa kufanya ushetani wake wote lakini siyo kumgusa Mkono ambaye ana mahusiano ya moja kwa moja na familia ya Mwalimu.Licha ya maradhi, kwa mwaka huo, isijekuwa pia alimkibia bwana yule.
Hahahaha, eti Hadi mrisho Gambo fisadi wa juzi tuu, kawaibia wahindi kina Tanga general na bulk mavifaa ya ujenzi, nae ana shule inaitwa mrisho Gambo tena ya governmentkweli hapa Nimrod Amenishangaza shule hata moja haina jina lake kama mafisadi na wanasiasa makanjanja wapendavyo kuandika majina yao katika taasisi. kwa Advocate Mkono ni tofauti.
Sent using Jamii Forums mobile app