TANZIA Mbunge wa zamani, Nimrod Mkono amefariki dunia nchini Marekani

TANZIA Mbunge wa zamani, Nimrod Mkono amefariki dunia nchini Marekani

Aliyekuwa Mbunge wa Musoma Vijijini na Butiama na pia Wakili maarufu Nchini Nimrod Mkono amefariki asubuhi ya leo kwa saa za Marekani.

Akiongea na @ayotv_ kwa njia ya simu Mdogo wa Marehemu, Zadock Mkono amethibitisha kutokea kifo cha Kaka yake.

“Nimepewa taarifa na Shemeji (Mke wa Wakili Mkono) kwamba Mzee amefariki nimempigia Shemeji alikuwa analia tu ameshindwa kuongea vizuri, Mzee aliondoka Tanzania tangu mwaka 2018 akaelekea Marekani kwa matibabu kwasababu alikuwa anasumbuliwa na tatizo la kusahausahau, kumbukumbu zilikuwa zinapotea”

“Mimi nipo Tanzania kwa sasa ninachoweza kuthibitisha ni kwamba kweli amefariki taarifa zaidi za kama alikuwa anaugua ugonjwa mwingine na kama alikuwa Hospitali au amefariki ghafla hizo bado sijajua, nitawapa taarifa zaidi baadaye”

Pumzika kwa amani mkono
 
Huyu mtu achana naye, amejenga masecondary Butiama kwa pesa zake binafsi akazipa majina ya machifu wa kizanaki na kuzikabidhi shule zote serikalini ni Mali ya serikali, Hakuna hata shule moja amejipa jina lake, siyo Utapeli kama wa kina Gertrude Lwakatare na Saint Marys zake kumbe zilitakiwa kusomesha yatima bure.

Leo kuna majitu yanapenda tu vitu vya umma kupachika majina yao kiholela tu.
Nadhani ni yeye pekee hakupenda jiinua.
Unakuta Mkuu wa Wilaya analazimisha shule iitwe jina lake
 
Mzee Mkono kitaa anaitwa "Article Don".

Alitoa kiwanja Mbezi Beach watu wajenge kanisa.

Hicho ni kipande kidogo tu cha ukarimu wake.

RIP.
Niliumia Mguu Shuleni kwa Kucheza Mpira ( mwaka 1993 Michuano ya Umisseta nikiwa na Mchezaji wa Simba SC zamani Wyclif Keto tukisama Shule moja ) na Kulazimika kwenda Kulazwa Dar Group Hospital.

Mzee Mkono alipoambiwa Mwanae ( Mpwawe ) Mimi nimelazwa Naumwa haraka sana akaja na Baba yangu Kuniona.

Alipokuja tu na Kuniona ( kwani tulikuwa tunashibana mno ) akamwambia Mzee wangu ( Baba ) kuwa nitoke / nitolewe hapo na nihamishiwe Agha Khan Hospital na Gharama zote juu yake.

Kweli Kesho nilitolewa pale Dar Group Hospital na kuhamishiwa Agha Khan Hospital ambapo nilipatiwa VIP Treatment kiasi kwamba niliingia nikiwa na Kilo zangu 45 na baada ya Kukaa pale Mwezi Kimatibabu nilitoka na Kilo 67 ( Kunenepeana ) na Bili ilikuwa ni Kubwa sana ( ya Mamilioni ) ila Marehemu Mzee Mkono aliipa / alinilipia.

Akhsante Uncle Mkono R.I.P sana tu.

Cc: Bujibuji Simba Nyamaume na Dr Matola PhD
 
Kitaifa

Mkono afariki dunia akiwa Marekani​

Jumanne, Aprili 18, 2023
mkono-pic.jpg

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Butiama mkoani Mara, Nimrod Mkono enzi za uhai wake. Picha na mtandao
By Beldina Nyakeke
Mwandishi wa Habari
Mwananchi

Muktasari:​

  • Aliyewahi kuwa Mbunge wa Butiama mkoani Mara, Nimrod Mkono amefariki dunia akiwa nchini Marekani alikokuwa akitibiwa tangu mwaka 2018.
Musoma. Aliyewahi kuwa Mbunge wa Butiama mkoani Mara, Nimrod Mkono amefariki dunia akiwa nchini Marekani alikokuwa akitibiwa tangu mwaka 2018.

Akizungumza kwa simu na Mwananchi leo Aprili 18, mdogo wa Marehemu, Zadock Mkono amethibitisha kutokea kwa kifo hicho akisema kimetokea Florida nchini Marekani.
“Taarifa ni za kweli, hata mimi nimezungumza na binti yake na mkewe wamesema kuwa amefariki leo (jana) saa za aubuhi huko Amerika. Alikuwa anatibiwa nchini Marekani katika jimbo la Florida miaka minne iliyopita na sasa unaingia mwaka wa tano,” amesema

Amesema Mkono alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer).
“Nimeongea na ndugu kule wanasema mwili utaletwa kuzikwa Tanzania, japo utachelewa,” amesema.
Mkono, aliyezaliwa Agosti 18, 1948, Busegwe Mkoani Mara alikuwa mwanasheria na mwanasiasa maarufu.
Akizungumzia msiba huo, Mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa wa Mara, Samuel Kiboye maarufu Namba tatu amesema kuwa chama hicho kimepoteza kada mtiifu na mpenda maendeleo wa kweli.
Akizungumza na Mwananchi digital, Kiboye amesema kuwa katika kipindi chake cha ubunge Mkono alifanya mambo mengi ya kimaendeleo katika sekta mbambali ikiwemo sekta ya elimu.
"Mkono amejenga shule za kisasa kule Butiama na hadi sasa wapo wanafunzi wanasoma na hata pale kilipo chuo kikuu cha Mwalimu Julius Nyerere cha Kilimo na Teknolojia ni shule aliyojenga yeye," amesema.
Amesema kwa ushiriki wa Mkono katika maendeleo ya chama pia haukuwa wa wasiwasi kwani ameshiriki mambo mengi ya kimaendeleo ya chama hicho kaunzia ngazi ya wilaya hadi mkoa.
"Ofisi za CCM mkoa kwa sasa zipo kwenye jengo alilojenga Mkono kwa pesa yake mwenyewe, lakini pia ni miongoni mwa watu waliofanikisha harambee ya chama chetu mwaka 2005 vile vile ametoa michango ya fedha taslimu kwa jumuiya za chama kwaajili ya maendeleo," amesema.

Promoted Link
 
Wananchi wa Jimbo lake nao walichaguaje mtu ambaye anapoteza kumbukumbu.

Na nani aliwatetea Bungeni tokea huo Mwaka 2018.

Bure Kabisa.
Inaonesha wewe ni kijana mdogo usiyejitambua...bado una nafasi ya kuijua dunia na maajabu yake.
Kumbuka, "Hujafa hujaumbika".

Kama ni mtu mwenye umri wa kuitwa 'mtu mzima', basi kuna shida mahali.
 
Niliumia Mguu Shuleni kwa Kucheza Mpira ( mwaka 1993 Michuano ya Umisseta nikiwa na Mchezaji wa Simba SC zamani Wyclif Keto tukisama Shule moja ) na Kulazimika kwenda Kulazwa Dar Group Hospital.

Mzee Mkono alipoambiwa Mwanae ( Mpwawe ) Mimi nimelazwa Naumwa haraka sana akaja na Baba yangu Kuniona.

Alipokuja tu na Kuniona ( kwani tulikuwa tunashibana mno ) akamwambia Mzee wangu ( Baba ) kuwa nitoke / nitolewe hapo na nihamishiwe Agha Khan Hospital na Gharama zote juu yake.

Kweli Kesho nilitolewa pale Dar Group Hospital na kuhamishiwa Agha Khan Hospital ambapo nilipatiwa VIP Treatment kiasi kwamba niliingia nikiwa na Kilo zangu 45 na baada ya Kukaa pale Mwezi Kimatibabu nilitoka na Kilo 67 ( Kunenepeana ) na Bili ilikuwa ni Kubwa sana ( ya Mamilioni ) ila Marehemu Mzee Mkono aliipa / alinilipia.

Akhsante Uncle Mkono R.I.P sana tu.

Cc: Bujibuji Simba Nyamaume na Dr Matola PhD
Pole Kwa msiba
 
Back
Top Bottom