Uchaguzi 2020 Mbunge wako amefanya nini kwa miaka hii mitano mpaka sasa?

Uchaguzi 2020 Mbunge wako amefanya nini kwa miaka hii mitano mpaka sasa?

Kuelekea mwaka huu wa uchaguzi,leo hebu tuwaangalie viongozi wetu wa majimbo(wabunge),tuliowapa dhamana ya uongozi ndani ya miaka mitano.Huku nilipo ni ktk jimbo la Ukonga jijini

Dar_es_salaam,na mbunge wa huku ni ndugu Mwita waitara kwasasa ni naibu waziri wa Tamisemi,huyu mtu mpaka sasa tangu anaingia mpaka anatoka hakuna kilichobadilika, kuanzia

kivule,kitunda,gongo la mboto na maeneo yake kama ulongoni changamoto kubwa ilikuwa madaraja na ubovu wa barabara, mvua zikinyesha kama una usafiri inabidi utafute parking sehemu nyingine hakuna madaraja na barabara mbovu,wakati anaanza kampeni kawanunulia sana wazee kahawa za kutosha wakaingia mkenge na vuguvugu lile la mabadiliko.

Baadaye alipounga juhudi ndio hata kurudi jimboni hajawahi,leo hii amerudi kwao huko mara ameanza kampeni za chinichini huku Ukonga anauhakika hapiti tena,huko mlipo wakuu hali ipoje?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mbunge wetu ametununulia King'amuzi cha Azam na TV flat screen pale maskan tunacheki cheki mambo tu bas. jengine jipya hamna, hamna kwa maana ya kwamba hamna, na baadae alinunuliwa akaenda upande ule.
 
Inaonesha ubunge ni kazi moja rahisi sana ila ina malipo makubwa.

Kufikiria kwamba wabunge wana pesa za kutengeneza barabara au kuleta maji au shughuli nyingine za maendeleo ni kutokujua utaratibu. Hayo ni maneno ya kisiasa ambayo yamepitwa na wakati. Na ndiyo maana wanaofikiri wakibadili wabunge mabadiliko yatatokea sio kweli.
 
Sio yeye ni serikali bwana mkubwa.yeye pesa ya kujenga barabara kuvuta maji hana.msipotoshe wananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
wakati anafanya kampeni alituahidi kwamba atatuletea maji.nadhani aliambiwa na wapambe wake kwamba ilo eneo kulikuwa na tatizo sugu la maji na kuna wakati alikua akija kufanya mikutano na wananchi ya ndani na ya hadhara swala la maji likikua linajadiliwa sana.

Wabunge wote waliopita swala la maji walishindwa sasa kama yeye alituhaidi maji kisha serikali ikaleta kama unavyosema ww basi yote heri cha msingi alichoahidi kakitekeleza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kufikiria kwamba wabunge wana pesa za kutengeneza barabara au kuleta maji au shughuli nyingine za maendeleo ni kutokujua utaratibu. Hayo ni maneno ya kisiasa ambayo yamepitwa na wakati. Na ndiyo maana wanaofikiri wakibadili wabunge mabadiliko yatatokea sio kweli.
Nani hajui utaratibu sie au wao wanatoa ahadi?
 
Stanslaus Mabula mbunge wa Nyamagana jiji la Mwanza kapigania sana tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama maeneo sugu kama buhongwa,mahina,kishili bulale,sawa ya chini na ya juu.

Bwana stanslaus mabula imefanikiwa kuionganisha barabara muhimu ya buhongwa kishiri kwa kiwango cha changarawe.
Ameboresha zahanati nyingi kwa kuongeza vifaa tiba na majengo.

Bwana Mabula kajitahidi sana ukilinganisha na wabunge waliopita kwa kuhakikisha vijana wanapata mikopo kupita mfuko wa vijana wa mkoa.kwa kweli Stanslaus Mabula ana mengi mazuri na ana stahili pongezi za dhati,ametufanyia mengi wana nyamagana na anastahili pongezi.

Yapo mengi sana lkn naomba niwasilishe haya machahce

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili jamaaa liongo sana, sijaona barabara ya changarawe kishiri to buhongwa ,mpaka dk hii na hyo mikopo unayosema labda amewapa ndg zake makopo ya maji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amejenga nyumba yake nzuri

Back
Top Bottom