Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Ndiyo maana Mwigulu anatakiwa kujitengenezea mazingira ya ama kuachana na siasa kwa wakati huu au kufikiria kuwapigia magoti wapinzani ili JPM akimkata awe na tawi la mti mwingine alishike. Harakati hizo azionesha sasa naawe Mwanaume wa shoka asiwe mnyonge kwa JPM.
Mkuu huu ushauri unaoutoa kwa Mwigulu ni kama unamdanganya tu, Mwigulu hana uwezo wowote wa kuwa na maisha ya juu nje ya siasa za mbeleko za ccm. Na hana uanaume wowote kama hana mbeleko ya vyombo vya dola. Mwigulu uliyekuwa unamuona jasiri ni kwakuwa alikuwa anazungukwa na vyombo vya dola, na alikuwa anaweza kuagiza kufanyika ukatili wowote kutokana na madaraka yake. Nje ya madaraka Mwigulu ni sawa na kasichana ka shule ya awali. Atajijinyenyekeza kwa Magufuli taka asitake, kwani anajua aliyoyafanya kaburi likifukuliwa atakuwa mpishi huko jela.